|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu katika yote....
Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana Mungu wa walio hai,Mungu mwenye huruma,Mungu wa upendo Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...Asante kwa wema na fadhili zako kwetu Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!
Baada ya siku kumi, neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia Yeremia. Basi, Yeremia akamwita Yohanani mwana wa Karea, na makamanda wote wa majeshi pamoja na watu wote, wadogo kwa wakubwa, akawaambia,
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
“Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli ambaye mlinituma kwake nipeleke maombi yenu, asema hivi: Kama mtabaki katika nchi hii, basi, nitawajenga, wala sitawabomoa; nitawaotesha wala sitawangoa; kwa maana nitabadili nia kwa sababu ya maafa niliyowatenda.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomna ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe... Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Yahwe ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona,masikio ya kusikia sauti yako na kuitii.. Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako,tukasimamie Neno lako,amri na sheria zako siku zote za maisha yetu... Ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu,ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....
Msimwogope mfalme wa Babuloni mnayemwogopa; naam, msimwogope hata kidogo. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Mimi niko pamoja nanyi kuwaokoeni na kuwasalimisha kutoka mikononi mwake. Nitawahurumieni na kumfanya mfalme awahurumie na kuwaacha nchini mwenu.
Tazama watoto wako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu kila mmoja na mahitaji yake Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipo kwenda kinyume nawe Yahweh tunaomba ukawape neema ya kuweza kujiombea,kufuata njia zako nazo zikawaweke huru... Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele... Amina...!!
Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,Baba wa Mbinguni aendelee kuwatendea sawasawa na mapenzi yake... Nawapenda. |
Mungu ajua yote, aongoza yote
(Kwa Mwimbishaji. Zaburi ya Daudi)
1Ee Mwenyezi-Mungu, wewe umenichunguza;
wewe wanijua mpaka ndani.
2Nikiketi au nikisimama, wewe wajua;
wajua kutoka mbali kila kitu ninachofikiria.
3Watambua nikienda au nikipumzika;
wewe wazijua shughuli zangu zote.
4Kabla sijasema neno lolote,
wewe, ee Mwenyezi-Mungu, walijua kabisa.
5Uko kila upande wangu, mbele na nyuma;
waniwekea mkono wako kunilinda.
6Maarifa yako yapita akili yangu;
ni makuu mno, siwezi kuyaelewa.
7Nikimbilie wapi ambako roho yako haiko?
Niende wapi ambako wewe huko?
8Nikipanda juu mbinguni, wewe upo;
nikijilaza chini kuzimu, wewe upo.
9Nikiruka hadi mawio ya jua,
au hata mipakani mwa bahari,
10hata huko upo kuniongoza;
mkono wako wa kulia utanitegemeza.
11Kama ningeliomba giza linifunike,
giza linizunguke badala ya mwanga,
12kwako giza si giza hata kidogo,
na usiku wangaa kama mchana;
kwako giza na mwanga ni mamoja.
13Wewe umeniumba, mwili wangu wote;
ulinitengeneza tumboni mwa mama yangu.
14Nakusifu maana nimefanywa kwa namna ya ajabu,
matendo yako ni ya ajabu;
wewe wanijua kabisakabisa.
15Umbo langu halikufichika kwako
nilipotungwa kwa siri na ustadi ndani ya dunia.
16Wewe uliniona hata kabla sijazaliwa,
uliandika kila kitu kitabuni mwako;
siku zangu zote ulizipanga,
hata kabla ya kuweko ile ya kwanza.
17Ee Mungu, mawazo yako ni makuu mno;
hayawezi kabisa kuhesabika.
18Ningeyahesabu yangekuwa mengi kuliko mchanga.
Niamkapo, bado nipo pamoja nawe.
19Laiti, ee Mungu, ungewaua watu waovu!
Laiti watu wauaji wangeondoka kwangu!
20Wanasema vibaya juu yako;
wanasema maovu juu ya jina lako!
21Ee Mwenyezi-Mungu, nawachukia wanaokuchukia;
nawadharau sana wale wanaokuasi!
22Maadui zako ni maadui zangu;
ninawachukia kabisakabisa.
23Unichunguze, ee Mungu, unijue moyo wangu,
unipime, uyajue mawazo yangu.
24Uangalie kama mwenendo wangu ni mbaya,
uniongoze katika njia ya milele.
Zaburi139;1-24
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.
No comments:
Post a Comment