Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 12 June 2019

Kikombe Cha Asubuhi ;Zaburi 145...


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante  Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu


Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni

Neema yako yatutosha  Mungu wetu..!

Kama mkimcha Mwenyezi-Mungu, na kumtumikia, na kusikiliza sauti yake bila kuiasi amri yake, kama nyinyi wenyewe pamoja na mfalme anayewatawala mkimfuata Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, basi mtafanikiwa. Lakini kama hamtasikiliza sauti ya Mwenyezi-Mungu, mkaasi amri yake, basi yeye atapambana nanyi pamoja na mfalme wenu.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa  Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

Kwa hiyo basi, tulieni na kulitazama jambo hilo kubwa ambalo Mwenyezi-Mungu atatenda mbele yenu. Je, sasa si wakati wa kuvuna ngano? Lakini mimi nitamwomba Mwenyezi-Mungu alete radi na mvua, nanyi mtatambua na kuona kuwa uovu wenu mliotenda mbele ya Mwenyezi-Mungu kwa kujitakia mfalme, ni mkubwa.”
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe

Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu  wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo 

Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...

Basi, Samueli akamwomba Mwenyezi-Mungu, naye akatuma radi na mvua katika siku hiyo. Watu wote wakamwogopa sana Mwenyezi-Mungu na Samueli. Hivyo wakamwambia Samueli, “Tafadhali utuombee sisi watumishi wako kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ili tusife; kwa sababu tumezidisha dhambi zetu kwa uovu huo wa kujitakia mfalme.”
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba
 ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!


Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....

Nawapenda.

Wimbo wa kumsifu Mungu
(Wimbo wa sifa wa Daudi)
1Nitakutukuza, ee Mungu wangu na mfalme wangu;
nitalitukuza jina lako daima na milele.
2Nitakutukuza kila siku;
nitalisifu jina lako daima na milele.
3Mwenyezi-Mungu ni mkuu, astahili sifa nyingi;
ukuu wake hauwezi kuchunguzika.
4Kizazi hata kizazi, sifa za matendo yako zitasimuliwa,
watu watatangaza matendo yako makuu.
5Nitanena juu ya utukufu na fahari yako,
nitayatafakari matendo yako ya ajabu.
6Watu watatangaza ukuu wa matendo yako ya ajabu,
nami nitatangaza ukuu wako.
7Watatangaza sifa za wema wako mwingi,
na kuimba juu ya uadilifu wako.
8Mwenyezi-Mungu ni mwenye huruma na rehema;
hakasiriki ovyo, amejaa fadhili.
9Mwenyezi-Mungu ni mwema kwa wote,
ni mwenye huruma kwa viumbe vyake vyote.
10Viumbe vyako vyote vitakushukuru, ee Mwenyezi-Mungu,
nao waaminifu wako watakutukuza.
11Watasema juu ya utukufu wa ufalme wako,
na kutangaza juu ya nguvu yako kuu,
12ili kila mtu ajue matendo yako makuu,
na fahari tukufu ya ufalme wako.
13Ufalme wako ni ufalme wa milele;
mamlaka yako yadumu vizazi vyote.
Mwenyezi-Mungu ni mwaminifu katika ahadi zake zote,
ni mwema katika matendo yake yote.145:13 Makala ya Kiebrania haina mistari hii miwili. Lakini iko katika hati moja ya kale, katika tafsiri ya Kigiriki (Septuaginta) na nyingine.
14Mwenyezi-Mungu huwategemeza wote wanaoanguka;
huwainua wote waliokandamizwa.
15Viumbe vyote vinakutazama kwa hamu,
nawe wavipa chakula chao kwa wakati wake.
16Waufumbua mkono wako kwa ukarimu,
watosheleza mahitaji ya kila kiumbe hai.
17Mwenyezi-Mungu ni mwadilifu katika njia zake zote;
ni mwema katika matendo yake yote.
18Mwenyezi-Mungu yuko karibu na wote wanaomwomba,
wote wanaomwomba kwa moyo mnyofu.
19Huwapatia mahitaji yao wote wanaomcha;
husikia kilio chao na kuwaokoa.
20Mwenyezi-Mungu huwalinda wote wanaompenda;
lakini atawaangamiza waovu wote.
21Nitatangaza sifa za Mwenyezi-Mungu;
viumbe vyote vilisifu jina lake takatifu,
milele na milele.

Zaburi145;1-21

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: