|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu katika yote....
Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana Mungu wa walio hai,Mungu mwenye huruma,Mungu wa upendo Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...Asante kwa wema na fadhili zako kwetu Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!
Samueli akawajibu, “Msiogope; ingawa mmefanya uovu huu, msiache kumfuata Mwenyezi-Mungu, ila mtumikieni kwa moyo wenu wote. Msiifuate miungu ya uongo isiyo na faida wala haiwezi kuwaokoa, maana ni ya uongo.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizo zifanya Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
Kwa heshima ya jina lake kuu, Mwenyezi-Mungu hatawatupa watu wake kwa sababu amependa kuwafanya nyinyi muwe watu wake. Tena kwa upande wangu haitatokea niache kuwaombea kwa Mwenyezi-Mungu; kufanya hivyo itakuwa kumkosea Mwenyezi-Mungu. Nitaendelea kuwafundisha njia njema na ya haki.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe....Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Yahweh ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...
Basi, nyinyi mcheni Mwenyezi-Mungu na kumtumikia kwa uaminifu kwa moyo wenu wote. Kumbukeni yale mambo makuu aliyowatendea. Lakini kama mkiendelea kutenda maovu, mtaangamia nyinyi wenyewe pamoja na mfalme wenu.”
Mungu wetu tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu, wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali Jehovah ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu kila mmoja na mahitaji yake... Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe Yahweh tunaomba ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia zako nazo zikawaweke huru... Nuru yako ikaangaze katika maisha yao.... Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako, Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele.... Amina..! Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami, Mungu Baba aendelee kuwatendea sawasawa na mapezni yake... Nawapenda. |
Sifa kwa Mungu Mwokozi
1Msifuni Mwenyezi-Mungu!
Umsifu Mwenyezi-Mungu, ee nafsi yangu!
2Nitamsifu Mwenyezi-Mungu maisha yangu yote;
nitamwimbia Mungu wangu muda wote niishipo.
3Msiwategemee wakuu wa dunia;
hao ni binadamu tu, hawawezi kuokoa.
4Binadamu akitoa pumzi yake ya mwisho,
anarudi mavumbini alimotoka;
na hapo mipango yake yote hutoweka.
5Heri mtu anayesaidiwa na Mungu wa Yakobo,
mtu aliyeweka tumaini lake kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wake,
6 Taz Mate 4:24; 14:15 aliyeumba mbingu na dunia,
bahari na vyote vilivyomo.
Yeye hushika ahadi yake milele.
7Yeye huwapatia wanaoonewa haki zao,
huwapa wenye njaa chakula.
Mwenyezi-Mungu huwapa wafungwa uhuru,
8huwafungua macho vipofu.
Mwenyezi-Mungu huwainua waliokandamizwa;
huwapenda watu walio waadilifu.
9Mwenyezi-Mungu huwalinda wageni,
huwategemeza wajane na yatima;
lakini huipotosha njia ya waovu.
10Mwenyezi-Mungu atawala milele,
Mungu wako, ee Siyoni, ni mfalme vizazi vyote!
Msifuni Mwenyezi-Mungu!
Zaburi146;1-10
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.
No comments:
Post a Comment