Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 8 July 2019

Kikombe Cha Asubuhi ; Methali 13...


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Haleluyah ni siku/wiki nyingine tena Mungu wetu ametuchagua

na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Si kwamba sisi tumetenda mema sana wala si kwa nguvu zetu
si kwa utashi wetu wala si kwa akili zetu si kwamba sisi
ni wazuri mno si kwa uwezo wetu sisi kuwa hivi tulivyo leo hii
Ni kwa rehema/neema zake ni kwa mapenzi yake Mungu wetu....

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari kwa majukumu yetu
Sifa na Utukufu tunakurudshia Mungu wetu....!!



Baba hamhukumu mtu yeyote; shughuli yote ya hukumu amemkabidhi Mwana, ili watu wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana hamheshimu Baba ambaye amemtuma.

Tazama jana imepita ee Mungu wetu leo ni siku mpya na kesho ni siku nyingine Jehovah tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
 Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Jehovah usitutie majaribu Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote
Yahweh tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona
Kwakupigwa kwake sisi tumepata kupona...
“Kweli nawaambieni, anayesikia neno langu, na kumwamini yule aliyenituma, anao uhai wa milele. Hatahukumiwa kamwe, bali amekwisha pita kutoka kifoni na kuingia katika uhai. Kweli nawaambieni, wakati unakuja, tena umekwisha fika, ambapo wafu wataisikia sauti ya Mwana wa Mungu, nao watakaoisikia, wataishi.

Yahweh tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe

Baba wa Mbinguni tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu
Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu
Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu
Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...

Kama vile Baba alivyo asili ya uhai, ndivyo pia alivyomjalia Mwanae kuwa asili ya uhai. Tena amempa mamlaka ya kuhukumu kwa sababu yeye ni Mwana wa Mtu. Msistaajabie jambo hili; maana wakati unakuja ambapo wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake, nao watafufuka: Wale waliotenda mema watafufuka na kuishi, na wale waliotenda maovu watafufuka na kuhukumiwa.

Mungu wetu tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
 kila mmoja na mahitaji yake 
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe
Baba wa Mbinguni ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia zako
wakasimaie Neno lako nalo likaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kuomba kwetu
Mungu wetu ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina...!!


Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami
Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea 
kama inavyompendeza yeye....
Nawapenda.

1Mtoto mwenye hekima husikia maagizo ya baba yake,
lakini mwenye dharau hasikilizi maonyo.
2Mtu mwema hupata mema kutokana na maneno yake,
lakini wadanganyifu huishi kwa ukatili.
3Achungaye mdomo wake huyahifadhi maisha yake,
anayeropoka ovyo hujiletea maangamizi.
4Mvivu hutamani lakini hapati chochote,
hali mwenye bidii hujaliwa riziki kwa wingi.
5Mwadilifu huuchukia uongo,
lakini mwovu hutenda kwa aibu na fedheha.
6Uadilifu huwalinda wenye mwenendo mnyofu,
lakini dhambi huwaangusha waovu.
7Baadhi hujidai kuwa matajiri kumbe hawana kitu;
wengine hujiona kuwa maskini hali wana mali tele.
8Fidia ya mtu ni mali yake,
lakini maskini hana cha kutishwa.
9Mwadilifu hungaa kama taa iwakayo vizuri,
lakini waovu ni kama taa inayozimika.
10Kiburi husababisha tu ugomvi,
lakini kwa wanaokubali shauri jema mna hekima.
11Mali ya harakaharaka hutoweka,
lakini akusanyaye kidogokidogo ataiongeza.
12Tumaini la kungojangoja huumiza moyo,
lakini tazamio linalotimia ni mti wa uhai.
13Anayedharau mawaidha anajiletea maangamizi,
lakini anayetii amri atapewa tuzo.
14Mafundisho ya wenye hekima ni chemchemi ya uhai;
humwezesha mtu kuiepa mitego ya kifo.
15Kuwa na akili huleta fadhili,
lakini njia ya waovu ni ya taabu13:15 aya ya 15 Kiebrania si dhahiri.
16Mwenye busara hutenda kila kitu kwa akili,
lakini mpumbavu hutembeza upumbavu wake.
17Mjumbe mbaya huwatumbukiza watu taabuni,13:17 huwatumbukiza watu taabuni: Au huanguka taabuni.
lakini mjumbe mwaminifu huleta nafuu.
18Umaskini na fedheha humpata asiyejali mafundisho,
lakini mwenye kusikia maonyo huheshimiwa.
19Inafurahisha upatapo kile unachotaka,
kwa hiyo wapumbavu huchukia kuepa uovu.
20Anayeandamana na wenye hekima hupata hekima,
lakini anayejiunga na wapumbavu atapata madhara.
21Watendao dhambi huandamwa na balaa,
lakini waadilifu watatuzwa mema.
22Mtu mwema huwaachia urithi uzao wake,
lakini mali ya mwenye dhambi imerundikiwa waadilifu.
23Shamba la maskini hutoa mazao mengi,
lakini bila haki hunyakuliwa.13:23 aya 23 Kiebrania si dhahiri.
24Asiyemwadhibu mtoto wake hampendi;
lakini ampendaye mwanawe humrudi mapema.
25Mwadilifu anacho chakula cha kumtosheleza,
lakini tumbo la waovu hutaabika kwa njaa.


Methali13;1-25

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: