|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu katika yote....
Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana Mungu wa walio hai,Mungu mwenye huruma,Mungu wa upendo Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...Asante kwa wema na fadhili zako kwetu Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!
“Akitokea nabii au mtabiri wa ndoto miongoni mwenu, akawaahidi na kuwapa ishara au maajabu fulani, halafu ishara au maajabu hayo yatokee, kisha aseme: ‘Tufuate miungu mingine na kuitumikia, (miungu ambayo hamjapata kuijua)’,
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
msisikilize maneno yake nabii huyo au mtabiri wa ndoto, kwa maana Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu anawatumia wao kuwajaribu, ili ajue kama mnampenda yeye Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa moyo wenu wote na kwa roho yenu yote.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomna ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe... Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Yahwe ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona,masikio ya kusikia sauti yako na kuitii.. Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako,tukasimamie Neno lako,amri na sheria zako siku zote za maisha yetu... Ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu,ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....
Mfuateni na kumcha Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kushika amri zake na kuitii sauti yake; mtumikieni na kuambatana naye.
Tazama watoto wako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu kila mmoja na mahitaji yake Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipo kwenda kinyume nawe Yahweh tunaomba ukawape neema ya kuweza kujiombea,kufuata njia zako nazo zikawaweke huru... Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele... Amina...!!
Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,Baba wa Mbinguni aendelee kuwatendea sawasawa na mapenzi yake... Nawapenda. |
1Binadamu hupanga mipango yake,
lakini kauli ya mwisho ni yake Mwenyezi-Mungu.
2Matendo ya mtu huonekana kwake kuwa sawa,
lakini Mwenyezi-Mungu hupima nia ya mtu.
3Mwekee Mwenyezi-Mungu kazi yako,
nayo mipango yako itafanikiwa.
4Mwenyezi-Mungu ameumba kila kitu kwa kusudi lake;
hata waovu kwa ajili ya siku ya maangamizi.
5Kila mwenye kiburi ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu;
hakika mtu wa namna hiyo hataacha kuadhibiwa.
6Kwa utii na uaminifu mtu huondolewa dhambi,
kwa kumcha Mwenyezi-Mungu huepuka uovu.
7Mwenyezi-Mungu akipendezwa na mwenendo wa mtu,
huwageuza hata adui zake kuwa marafiki.
8Afadhali mali kidogo kwa uadilifu,
kuliko mapato mengi kwa udhalimu.
9Mtu aweza kufanya mipango yake,
lakini Mwenyezi-Mungu huongoza hatua zake.
10Mfalme huamua kwa maongozi ya Mungu;
anapotoa hukumu hakosei.
11Mwenyezi-Mungu hutaka kipimo na mizani halali;
mawe yote mfukoni ya kupimia ni kazi yake.
12Ni chukizo kubwa wafalme kutenda uovu,
maana msingi wa mamlaka yao ni haki.
13Mfalme hupendelea mtu asemaye kwa unyofu;
humpenda mtu asemaye ukweli.
14Hasira ya mfalme ni kama mjumbe wa kifo;
mtu mwenye busara ataituliza.
15Uso wa mfalme ukingaa kuna uhai;
wema wake ni kama wingu la masika.
16Kupata hekima ni bora kuliko dhahabu;
kupata akili ni chaguo bora kuliko fedha.
17Njia ya wanyofu huepukana na uovu;
anayechunga njia yake huhifadhi maisha yake.
18Kiburi hutangulia maangamizi;
majivuno hutangulia maanguko.
19Afadhali kuwa mnyenyekevu na kuwa maskini,
kuliko kugawana nyara na wenye kiburi.
20Anayezingatia mafundisho atafanikiwa;
heri mtu yule anayemtumainia Mwenyezi-Mungu.
21Mwenye hekima moyoni huitwa mwenye akili;
neno la kupendeza huwavutia watu.
22Hekima ni chemchemi ya uhai kwake aliye nayo,
bali upumbavu ni adhabu ya wapumbavu.
23Moyo wa mwenye hekima humwezesha kusema kwa busara;
huyafanya maneno yake yawe ya kuvutia.
24Maneno mazuri ni kama asali;
ni matamu rohoni na yenye kuupa mwili afya.
25 Taz Meth 14:12 Mtu aweza kuona njia yake kuwa sawa,
lakini mwishowe humwongoza kwenye kifo.
26Hamu ya chakula humhimiza mfanyakazi,
maana njaa yake humsukuma aendelee.
27Mtu mwovu hupanga uovu;
maneno yake ni kama moto mkali.
28Mtu mpotovu hueneza ugomvi,
mfitini hutenganisha marafiki.
29Mtu mkatili humshawishi jirani yake;
humwongoza katika njia mbaya.
30Anayekonyeza jicho kwa hila amepanga maovu;
anayekaza midomo amekwisha nuia mabaya.
31Kuwa na mvi za uzee ni taji la utukufu;
hupatikana kwa maisha ya uadilifu.
32Asiye mwepesi wa hasira ni bora kuliko mwenye nguvu;
aitawalaye nafsi yake ni bora kuliko autekaye mji.
33Kura hupigwa kujua yatakayotukia,
lakini uamuzi ni wake Mwenyezi-Mungu.
Methali16;1-33
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.
No comments:
Post a Comment