Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday, 12 July 2019

Kikombe Cha Asubuhi ; Methali 17...

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante  Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu


Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni

Neema yako yatutosha  Mungu wetu..!

Lakini nabii huyo au mtabiri wa ndoto atauawa, kwa sababu atakuwa amewafundisha uasi dhidi ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, aliyewatoa katika nchi ya Misri na kuwakomboa kutoka utumwani, ili muiache njia ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu aliwaamuru muifuatea. Hivyo ndivyo mtakavyokomesha uovu miongoni mwenu.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa  Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

“Ikiwa ndugu yako wa tumbo moja, au mtoto wako wa kiume au wa kike, au mke wako umpendaye sana, au rafiki yako mwandani, atakushawishi kwa siri akisema, ‘Twende tukaabudu miungu mingine’, miungu ambayo wewe wala babu zenu hamuijui, au baadhi ya miungu ya watu wanaoishi karibu nanyi, au miungu ya watu waishio mbali toka ncha moja ya dunia hadi nyingine,
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe



Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu  wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo 

Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...

usikubali kushawishiwa, wala usimsikilize au kumhurumia, wala usimwachilie wala kumficha; bali utamuua. Wewe utakuwa wa kwanza kuchukua hatua ya kumuua, kisha watu wengine wote watafuata.
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba
 ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!


Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....
Nawapenda.

1Afadhali mkate mkavu kwa amani,
kuliko karamu katika nyumba ya ugomvi.
2Mtumwa mwenye busara atachukua nafasi ya mwana mpumbavu,
atapata sehemu ya urithi wa jamaa hiyo.
3Ubora wa dhahabu ama fedha hupimwa kwa moto,
lakini Mwenyezi-Mungu ndiye apimaye mioyo ya watu.
4Mtenda maovu husikiliza maneno mabaya,
mwongo hutegea sikio ulimi mdanganyifu.
5Anayemdhihaki maskini anamtukana Muumba wake;
anayefurahia maafa hatakosa kuadhibiwa.
6Wazee huwaonea fahari wajukuu zao;
watoto huwaonea fahari wazazi wao.
7Maneno mazuri si kawaida kinywani mwa mpumbavu,
sembuse maneno ya uongo kinywani mwa kiongozi!
8Kwa mhongaji, hongo ni kama hirizi;
kila afanyacho hufanikiwa.
9Anayesamehe makosa hujenga urafiki,
lakini anayekumbusha makosa hutenga rafiki.
10Onyo kwa mwenye busara lina maana,
kuliko mapigo mia kwa mpumbavu.
11Afanyalo mtu mwovu ni kuasi tu;
mjumbe mkatili atatumwa dhidi yake.
12Afadhali kukutana na dubu jike aliyenyanganywa watoto wake,
kuliko kukutana na mpumbavu katika upumbavu wake.
13Mwenye kulipiza mema kwa mabaya,
mabaya hayataondoka nyumbani mwake.
14Kuanzisha ugomvi ni kama kufanya ufa kwenye bwawa;
achana na ugomvi kabla haujafurika.
15Kumsamehe mwenye hatia na kumwadhibu asiye na hatia
yote mawili ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu.
16Ya nini mpumbavu kuwa na fedha mkononi kununulia hekima,
wakati yeye mwenyewe hana akili?
17Rafiki wa kweli ni rafiki siku zote,
ndugu huzaliwa asaidie wakati wa taabu.
18Si jambo la akili kuweka rehani,
na kuwa mdhamini wa mtu mwingine.
19Anayependa ugomvi anapenda dhambi;
anayejigamba17:19 anayejigamba: Neno kwa neno; ainuaye sana mlango wake. anajitafutia maangamizi.
20Mwenye moyo mpotovu hafanikiwi,
na msema uongo hupatwa na maafa.
21Mtoto mpumbavu ni huzuni kwa baba yake,
na baba wa mpumbavu hana furaha.
22Moyo mchangamfu ni dawa,
bali moyo wenye huzuni hudhoofisha mwili.
23Mtu mbaya hupokea hongo kwa siri
ili apate kupotosha haki.
24Mtu mwenye busara lengo lake ni hekima,
lakini mpumbavu hupania kila kitu duniani.
25Mtoto mpumbavu ni huzuni kwa baba yake,
na uchungu kwa mama yake mzazi.
26Si vizuri kumtoza faini mtu asiye na hatia;
ni kosa kumchapa viboko muungwana.
27Asiyesema sana ana maarifa;
mtu mtulivu ni mwenye busara.
28Hata mpumbavu akinyamaza huonekana ana hekima;
akifunga mdomo wake huonekana kuwa mwenye akili.

Methali17;1-28

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: