Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 15 July 2019

Kikombe Cha Asubuhi ; Methali 18...

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Haleluyah ni siku/wiki nyingine tena Mungu wetu ametuchagua

na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Si kwamba sisi tumetenda mema sana wala si kwa nguvu zetu
si kwa utashi wetu wala si kwa akili zetu si kwamba sisi
ni wazuri mno si kwa uwezo wetu sisi kuwa hivi tulivyo leo hii
Ni kwa rehema/neema zake ni kwa mapenzi yake Mungu wetu....

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari kwa majukumu yetu
Sifa na Utukufu tunakurudshia Mungu wetu....!!

Mpigeni mawe mpaka afe! Kwa sababu amejaribu kukuvutia mbali na Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, aliyekutoa utumwani nchini Misri. Hivyo, Waisraeli wote watasikia na kuogopa, na kamwe hawatafanya uovu kama huo.
Tazama jana imepita ee Mungu wetu leo ni siku mpya na kesho ni siku nyingine Jehovah tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
 Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Jehovah usitutie majaribu Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote
Yahweh tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona
Kwakupigwa kwake sisi tumepata kupona...

“Mtakapoishi katika miji ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, anawapa, huenda mkasikia kuwa watu fulani mabaradhuli miongoni mwenu, wamewashawishi watu wa mji wakisema, ‘Twende tukaabudu miungu mingine,’ miungu ambayo bado hamjawahi kuijua,
Yahweh tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe

Baba wa Mbinguni tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu
Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu
Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu
Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...

basi mtapeleleza na kufanya uchunguzi na kuuliza kwa makini; na kama ni kweli kuwa jambo la kuchukiza limetendeka kati yenu, hamna budi kuwaua kwa upanga watu wa mji huo; mtauangamiza kabisa mji huo na kuwaua ng'ombe wote kwa upanga.
Mungu wetu tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
 kila mmoja na mahitaji yake 
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe
Baba wa Mbinguni ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia zako
wakasimaie Neno lako nalo likaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kuomba kwetu
Mungu wetu ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina...!!


Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami
Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea 
kama inavyompendeza yeye....
Nawapenda.

1Anayetafuta yake tu hujitenga na wenzake;
hukasirika akipewa shauri lolote jema.
2Mpumbavu hapendezwi na busara;
kwake cha maana ni maoni yake tu.
3Ajapo mwovu huja pia dharau;
pamoja na aibu huja fedheha.
4Maneno yaweza kuwa chemchemi ya hekima;
yenye kilindi kama bahari, kama kijito kinachobubujika.
5Si vizuri kumpendelea mtu mwovu,
na kumnyima haki mtu mwadilifu.
6Maneno ya mpumbavu huleta ugomvi;
kila anachosema husababisha adhabu.
7Kinywa cha mpumbavu humwangamiza mwenyewe;
mdomo wake ni mtego wa kumnasa yeye mwenyewe.
8Maneno ya msengenyaji ni kama kitoweo kitamu;
ambacho hushuka moja kwa moja mpaka tumboni.
9Mtu mvivu kazini mwake
ni ndugu yake mharibifu.
10Jina la Mwenyezi-Mungu ni mnara imara;
mwadilifu huukimbilia akawa salama.
11Lakini tajiri hudhani mali ni ngome yake;
anafikiri hayo ni ukuta mrefu unaomlinda.
12Majivuno ya moyoni huleta maangamizi,
lakini unyenyekevu huleta heshima.
13Kujibu kabla ya kusikiliza
ni upumbavu na jambo la aibu.
14Roho ya mtu huweza kustahimili ugonjwa,
lakini ukiwa umevunjika moyo, utastahimilije?
15Mtu mwenye akili hujipatia maarifa,
sikio la mwenye busara hutafuta maarifa.
16Zawadi humfungulia mtu milango;
huweza kumfikisha mtu mbele ya mkuu.
17Ajiteteaye kwanza huonekana msema kweli,
mpaka hapo mpinzani wake atakapoanza kumhoji.
18Kura hukomesha ubishi;
huamua kati ya wakuu wanaopingana.
19Ndugu aliyeudhiwa ni mgumu kuliko mji wa ngome;18:19 Ndugu … ngome: Maana katika Kiebrania si dhahiri.
magomvi hubana kama makufuli ya ngome.
20Maneno ya mtu yaweza kumshibisha;
hutosheka kwa matokeo ya maneno yake.
21Ulimi una nguvu ya kufanya hai na kuua;
wanaopenda kuutumia watakula matunda yake.
22Anayempata mke amepata bahati njema;
hiyo ni fadhili kutoka kwa Mwenyezi-Mungu.
23Maskini huomba kwa unyenyekevu,
bali tajiri hujibu kwa ukali.
24Marafiki wengi waweza kumwangusha mtu,18:24 Marafiki wengi … kumwangusha mtu: Maana yake katika makala ya Kiebrania si dhahiri.
lakini wapo marafiki waaminifu kuliko ndugu.

Methali18;1-24

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: