|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu wetu katika yote...
Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetuAsante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu
Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni Neema yako yatutosha Mungu wetu..!
Mimi Paulo, mfungwa kwa ajili ya Kristo Yesu, na ndugu Timotheo, ninakuandikia wewe Filemoni mpendwa, mfanyakazi mwenzetu, na kanisa linalokutana nyumbani kwako, na wewe dada Afia, na askari mwenzetu Arkipo. Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti, Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
Kila wakati ninaposali, nakukumbuka wewe Filemoni, na kumshukuru Mungu, maana nasikia habari za imani yako kwa Bwana Yesu na upendo wako kwa watu wote wa Mungu.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama inavyokupendeza wewe Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...
Naomba ili imani hiyo unayoshiriki pamoja nasi ikuwezeshe kuwa na ujuzi mkamilifu zaidi wa baraka zote tunazopata katika kuungana kwetu na Kristo. Ndugu, upendo wako umeniletea furaha kubwa na kunipa moyo sana! Nawe umeichangamsha mioyo ya watu wa Mungu.
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao Nuru yako ikaangaze katika maisha yao Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele Amina....!!!
Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana kwakuwanami/kunisoma Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea kama inavyompendeza yeye Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba ukae nanyi daima.... Nawapenda. |
1Divai huleta dhihaka na kileo huleta ugomvi;
yeyote anayevutiwa navyo hana hekima.
2Ghadhabu kali ya mfalme ni kama simba angurumaye;
anayemkasirisha anayahatarisha maisha yake.
3Ni jambo la heshima kuepa ugomvi;
wapumbavu ndio wanaogombana.
4Mvivu halimi wakati wa kulima;
wakati wa mavuno atatafuta asipate chochote.
5Fikira za mtu zimefichika kama kilindi cha maji;
lakini mtu mwenye busara ajua kuzichota humo.
6Watu wengi hujivunia kuwa wema,
lakini mwaminifu wa kweli apatikana wapi?
7Mtu mwadilifu akiishi kwa unyofu;
watoto wake atakaowaacha watabarikiwa.
8Mfalme mwema aketipo kutoa hukumu,
huupepeta uovu wote kwa macho yake.
9Nani athubutuye kusema: “Nimeutakasa moyo wangu;
mimi nimetakasika dhambi yangu?”
10Mizani ya udanganyifu na vipimo vya udanganyifu,
vyote ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu.
11Hata mtoto hujulikana kwa matendo yake,
kama tabia yake ni njema na aminifu.
12Sikio lisikialo na jicho lionalo,
yote mawili kayafanya Mwenyezi-Mungu.
13Usipende kulala tu usije ukawa maskini;
uwe macho nawe utakuwa na chakula kingi.
14“Hakifai, hakifai”, mnunuzi hulalamika,
lakini akiondoka hujisifu amepunguziwa bei.
15Kuna dhahabu na wingi wa mawe ya thamani kubwa;
lakini cha thamani kubwa zaidi ni maneno ya busara!
16Mtu akiahidi mbele yako kumdhamini mgeni,
chukua nguo yake;
mfanye awajibike kwa kuwadhamini wageni.
17Chakula kipatikanacho kwa udanganyifu ni kitamu,
lakini baadaye huwa kama mchanga kinywani.
18Mipango mizuri hufanyika kwa kushauriana;
ukitaka kuanza vita lazima kutafakari kwanza.
19Mpiga domo hafichi siri,
kwa hiyo mwepe mtu wa kuropoka.
20Anayemlaani baba yake au mama yake,
mwanga wa uhai wake utazimwa kama taa gizani.
21Mali iliyopatikana kwa haraka mwanzoni,
haitakuwa ya heri mwishoni.
22Usiseme, “Nitalipiza ubaya niliotendewa.”
Mtegemee Mwenyezi-Mungu naye atakusaidia.
23Mizani ya udanganyifu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu,
na vipimo visivyo halali ni kitu kibaya.
24Hatua za mtu huongozwa na Mwenyezi-Mungu;
awezaje binadamu kujua njia ya kwenda?
25Ni hatari kusema kwa mzaha “Usiahidi kumpa Mungu kitu bila kufikiri,
la sivyo utaanza kusikitika baada ya nadhiri yako.”
26Mfalme mwenye busara huwapepeta waovu;
huwaadhibu bila huruma.
27Dhamiri ya mtu ni taa ya Mwenyezi-Mungu;
huchunguza nafsi yake mtu mpaka ndani kabisa.
28Wema na uaminifu humkinga mfalme;
utawala wake huimarishwa kwa uadilifu.
29Fahari ya vijana ni nguvu zao,
uzuri wa vikongwe ni mvi za uzee.
30Mapigo yanayoumiza ni dawa ya kuondoa uovu;
viboko husafisha nafsi mpaka ndani kabisa.
Methali20;1-30
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.
No comments:
Post a Comment