|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu wetu katika yote...
Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetuAsante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu
Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni Neema yako yatutosha Mungu wetu..!
“Ufuatao ni mwongozo wa ibada kuhusu sadaka za amani ambazo mtu aweza kumtolea Mwenyezi-Mungu. Ikiwa mtu anatoa sadaka hiyo ya kumshukuru Mungu, basi, ataitoa pamoja na maandazi yasiyotiwa chachu yaliyopakwa mafuta, mikate myembamba iliyopakwa mafuta na maandazi ya unga laini uliochanganywa na mafuta.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti, Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
Pamoja na sadaka hiyo yake ya amani ya kumshukuru Mungu, ataleta maandazi yaliyotiwa chachu. Kutokana na maandazi hayo, atamtolea Mwenyezi-Mungu andazi moja kutoka kila sadaka; maandazi hayo yatakuwa yake kuhani anayeirashia madhabahu damu ya sadaka za amani.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama inavyokupendeza wewe Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...
Nyama ya sadaka hiyo ya amani ya kumshukuru Mungu italiwa siku hiyohiyo inapotolewa; hataacha hata sehemu yake hadi asubuhi.
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao Nuru yako ikaangaze katika maisha yao Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele Amina....!!!
Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana kwakuwanami/kunisoma Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea kama inavyompendeza yeye Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba ukae nanyi daima.... Nawapenda. |
Methali zaidi za Solomoni
1Hizi nazo ni methali nyingine za mfalme Solomoni walizonakili watu wa Hezekia, mfalme wa Yuda.
2Mungu hutukuzwa kwa kuficha mambo,
lakini mfalme hutukuzwa kwa yale anayoeleza.
3Kama zilivyo mbali mbingu na kirefu kina cha ardhi
ndivyo zisivyochunguzika akili za mfalme.
4Toa takataka katika fedha,
na mhunzi atakutengenezea chombo kizuri.
5Waondoe waovu mbele ya mfalme,
na utawala wake utaimarika katika haki.
6Usijipendekeze kwa mfalme,
wala usijifanye mtu mkubwa,
7maana ni heri kuambiwa, “Njoo huku mbele”,
kuliko kuporomoshwa mbele ya mkuu.
Mambo uliyoyaona kwa macho yako,
8usiharakishe kuyapeleka mahakamani;
maana utafanya nini hapo baadaye,
shahidi mwingine akibatilisha hayo usemayo?
9Suluhisha ugomvi na mwenzako peke yake,
na kila mmoja wenu asitoe siri ya mwenzake;
10watu wasije wakajua kuna siri,
ukajiharibia jina lako daima.
11Neno lisemwalo wakati unaofaa,
ni kama nakshi za dhahabu juu ya madini ya fedha.
12Onyo la mwenye hekima kwa mtu msikivu,
ni bora kuliko pete au vito vya dhahabu safi.
13Mjumbe mwaminifu humfurahisha yule aliyemtuma,
kama maji baridi wakati wa joto la mavuno.
14Kama vile mawingu na upepo bila mvua,
ndivyo alivyo mtu anayejigamba kutoa zawadi asiitoe.
15Kwa uvumilivu mtawala huweza kushawishika;
ulimi laini huvunja mifupa.
16Upatapo asali kula kiasi cha kukutosha,
usije ukaikinai na kuitapika.
17Usimtembelee jirani yako mara kwa mara,
usije ukamchosha naye akakuchukia.
18Mtu atoaye ushahidi wa uongo dhidi ya mwenziwe,
ni hatari kama rungu, upanga au mshale mkali.
19Kumtegemea mtu asiyeaminika wakati wa taabu,
ni kama jino bovu au mguu ulioteguka.
20Kumwimbia mtu mwenye huzuni,
ni kama kuvua nguo wakati wa baridi,
au kutia siki katika kidonda.
21Adui yako akiwa na njaa, mpe chakula;
akiwa na kiu, mpe maji ya kunywa.
22Hivyo utafanya apate aibu kali,
kama makaa ya moto kichwani pake,
naye Mwenyezi-Mungu atakutuza.
23Upepo wa kusi huleta mvua,
hali kadhalika masengenyo huleta chuki.
24Afadhali kuishi pembeni juu ya paa,
kuliko kuishi nyumbani pamoja na mwanamke mgomvi.
25Kama vile maji baridi kwa mwenye kiu,
ndivyo habari njema kutoka mbali.
26Mwadilifu akubaliye kufuata mambo ya mwovu,
ni chemchemi iliyochafuliwa au kisima kilichotibuliwa.
27Si vizuri kula asali nyingi mno;
kadhalika haifai kujipendekeza mno.25:27 kadhalika … mno: Maana katika Kiebrania si dhahiri.
28Mtu asiyeweza kuzuia hasira yake,
ni kama mji usio na ulinzi unaposhambuliwa.
Methali25;1-28
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.
No comments:
Post a Comment