Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday, 13 September 2019

Kikombe Cha Asubuhi;Isaya 11....


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante  Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu


Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni

Neema yako yatutosha  Mungu wetu..!

Lakini nyinyi ni ukoo mteule, makuhani wa Mfalme, taifa takatifu; watu wake Mungu mwenyewe, mlioteuliwa kutangaza matendo makuu ya Mungu aliyewaiteni kutoka gizani, akawaingizeni katika mwanga wake mkuu.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa  Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe



Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu  wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo 

Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...

Wakati mmoja nyinyi hamkuwa watu wa Mungu, lakini sasa nyinyi ni watu wake; wakati mmoja hamkupewa huruma ya Mungu, lakini sasa mmepokea huruma.
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba
 ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!


Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....

Nawapenda.

Ufalme wa amani

1 11:1 Taz Ufu 5:5; 22:16 
Kutatokea chipukizi katika kisiki cha Yese,
tawi litachipua mizizini mwake.
2Roho ya Mwenyezi-Mungu itakaa kwake,
roho ya hekima na maarifa,
roho ya shauri jema na nguvu,
roho ya ujuzi na ya kumcha Mwenyezi-Mungu.
3Atafurahia kumcha Mwenyezi-Mungu.
Hatahukumu kadiri ya mambo ya njenje,
wala kuamua kufuatana na yale anayosikia.
4 11:4 Taz 2Thes 2:8 Atawapatia haki watu maskini,
atawaamulia sawasawa wanyonge nchini.
Kwa neno lake ataiadhibu dunia,
kwa tamko lake atawaua waovu.
5 11:5 Taz Efe 6:14 Haki itakuwa kama mkanda wa kujifunga,
uaminifu utakaa naye kama mkanda kiunoni.
6 11:6-9 Taz Isa 65:25 Mbwamwitu ataishi pamoja na mwanakondoo,
chui watapumzika pamoja na mwanambuzi.
Ndama na wanasimba watakula pamoja,
na mtoto mdogo atawaongoza.
7Ngombe na dubu watakula pamoja,
ndama wao watapumzika pamoja;
na simba atakula majani kama ng'ombe.
8Mtoto mchanga atacheza kwenye shimo la nyoka
mtoto ataweza kutia mkono shimoni mwa nyoka wa sumu.
9 11:9 Taz Hab 2:14 Katika mlima mtakatifu wa Mungu
hakutakuwa na madhara wala uharibifu.
Maana kumjua Mwenyezi-Mungu kutaenea pote nchini,
kama vile maji yajaavyo baharini.
Walio uhamishoni watarudi
10 11:10 Taz Roma 15:12 Siku ile chipukizi wa Yese atakuwa ishara kwa mataifa; mataifa yatamtafuta na makazi yake yatatukuka. 11Siku hiyo, Bwana ataunyosha mkono wake tena kuwarejesha watu wake waliosalia huko Ashuru, Misri, Pathrosi, Kushi, Elamu, Shinari, Hamathi na sehemu za pwani.
12Naye atatweka bendera kuwaashiria mataifa,
kuwakusanya Waisraeli waliodharauliwa,
kuwaleta pamoja watu wa Yuda waliotawanywa,
na kuwarudisha toka pembe nne za dunia.
13Wivu wa Efraimu juu ya Yuda utakoma,
hakutakuwa tena na uadui kati ya Yuda na Efraimu.
14Wote pamoja watawavamia Wafilisti walio magharibi,
pamoja watawapora watu wakaao mashariki.
Watawashinda Waedomu na Wamoabu,
nao Waamoni watawatii.
15Mwenyezi-Mungu atakausha ghuba ya bahari ya Shamu,11:15 bahari ya Shamu: Kiebrania: Bahari ya Misri.
kwa pumzi yake ichomayo atakausha mto Eufrate,
nao utagawanyika katika vijito saba,
watu wavuke humo miguu mikavu.
16Tena, kutakuwa na barabara kuu toka Ashuru
kwa ajili ya watu wake waliobaki humo
kama ilivyokuwa kwa Waisraeli
wakati walipotoka nchini Misri.

Isaya11;1-16

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: