|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu katika yote....
Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana Mungu wa walio hai,Mungu mwenye huruma,Mungu wa upendo Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...Asante kwa wema na fadhili zako kwetu Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!
Enyi watumishi wa nyumbani, watiini wakuu wenu kwa heshima yote, wawe wema na wapole au wenye kuchukiza. Maana kama mnavumilia maumivu ya mateso msiyostahili kwa sababu mwajua kwamba Mungu anataka hivyo, basi Mungu atawafadhili. Maana, mtapata tuzo gani mkivumilia mapigo mnayostahili kwa sababu ya makosa yenu? Lakini kama mnavumilia mateso hata ingawa mmetenda mema, Mungu atawapeni baraka kwa ajili hiyo.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
Hayo ndiyo mliyoitiwa; maana Kristo mwenyewe aliteseka kwa ajili yenu, akawaachieni mfano, ili mfuate mwenendo wake. Yeye hakutenda dhambi, wala neno la udanganyifu halikusikika mdomoni mwake. Alipotukanwa yeye hakujibu kwa tukano; alipoteseka yeye hakutoa vitisho, bali aliyaweka matumaini yake kwa Mungu, hakimu mwenye haki.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomna ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe...
Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Yahwe ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona,masikio ya kusikia sauti yako na kuitii.. Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako,tukasimamie Neno lako,amri na sheria zako siku zote za maisha yetu... Ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu,ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....
Yeye mwenyewe alizibeba dhambi zetu katika mwili wake juu ya msalaba, tupate kufa kuhusu dhambi, na kuishi kwa ajili ya uadilifu. Kwa majeraha yake, nyinyi mmeponywa. Nyinyi mlikuwa kama kondoo waliokuwa wamepotea; lakini sasa mmemrudia Mchungaji na Mlinzi wa roho zenu.
Tazama watoto wako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu kila mmoja na mahitaji yake Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipo kwenda kinyume nawe Yahweh tunaomba ukawape neema ya kuweza kujiombea,kufuata njia zako nazo zikawaweke huru... Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele... Amina...!!
Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,Baba wa Mbinguni aendelee kuwatendea sawasawa na mapenzi yake... Nawapenda. |
Mungu ataiadhibu Babuloni
1 13:1--14:23 Taz Isa 47:1-15; Yer 50:1--51:64
Kauli ya Mungu dhidi ya Babuloni ambayo Isaya, mwana wa Amozi, alipewa katika maono:
2Mungu asema:
“Twekeni bendera juu ya mlima usio na miti.
Wapaazieni sauti askari
wapungieni watu mkono
waingie malango ya mji wa wakuu.
3Mimi nimewaamuru wateule wangu,
nimewaita mashujaa wangu,
hao wenye kunitukuza wakishangilia,
waje kutekeleza lengo la hasira yangu.”
4Sikilizeni kelele milimani
kama za kundi kubwa la watu!
Sikilizeni kelele za falme,
na mataifa yanayokusanyika!
Mwenyezi-Mungu wa majeshi
analikagua jeshi linalokwenda vitani.
5Wanakuja kutoka nchi za mbali,
wanatoka hata miisho ya dunia:
Mwenyezi-Mungu na silaha za hasira yake
anakuja kuiangamiza dunia.
6 13:6 Taz Yoe 1:15 Lieni maana siku ya Mwenyezi-Mungu imekaribia;
inakuja kama maafa kutoka kwa Mungu Mwenye Nguvu.
7Kwa hiyo mikono ya kila mtu italegea,
kila mtu atakufa moyo.
8Watu watafadhaika,
watashikwa na hofu na maumivu,
watakuwa na uchungu kama mama anayejifungua.
Watatazamana kwa mashaka,
nyuso zao zitawaiva kwa haya.
9Siku ya Mwenyezi-Mungu inakuja,
siku kali, ya ghadhabu na hasira kali.
Itaifanya nchi kuwa uharibifu,
itawaangamiza wenye dhambi wake.
10 13:10 Taz Eze 32:7; Mat 24:29; Marko 13:24-25; Luka 21:25; Ufu 6:12-13 Nyota na vilimia vyake angani hazitaangaza;
jua linapochomoza litakuwa giza,
na mwezi hautatoa mwanga wake.
11Mwenyezi-Mungu asema hivi:
“Nitauadhibu ulimwengu kwa uovu wake,
waovu kwa sababu ya makosa yao.
Nitakikomesha kiburi cha wenye majivuno,
na kuporomosha ubaradhuli wa watu katili.
12Nitawafanya watu kuwa wachache kuliko dhahabu safi;
binadamu watakuwa wachache kuliko dhahabu ya Ofiri.
13Nitazitetemesha mbingu
nayo nchi itatikisika katika misingi yake
kwa sababu ya ghadhabu yangu Mwenyezi-Mungu
siku ile ya hasira yangu kali.
14“Kama swala anayewindwa,
kama kondoo wasio na mchungaji,
kila mmoja atajiunga na watu wake
kila mtu atakimbilia nchini mwake.
15Yeyote atakayeonekana atatumbuliwa,
atakayekamatwa atauawa kwa upanga.
16Watoto wao wachanga watapondwapondwa mbele yao,
watanyanganywa nyumba zao,
na wake zao watanajisiwa.
17“Ninawachochea Wamedi dhidi yao;
watu ambao hawajali fedha
wala hawavutiwi na dhahabu.
18Mishale yao itawaua vijana,
hawatakuwa na huruma kwa watoto,
wala kuwahurumia watoto wachanga.
19 13:19 Taz Mwa 19:24 Babuloni johari ya falme zote
na umaarufu wa kiburi cha Wakaldayo
utakuwa kama Sodoma na Gomora,
wakati Mungu alipoiangamiza.
20Kamwe hautakaliwa tena na watu,
watu hawataishi humo katika vizazi vyote.
Hakuna Mwarabu atakayepiga hema lake humo,
wala mchungaji atakayechunga wanyama wake humo.
21 13:21 Taz Isa 34:14; Sef 2:14; Ufu 18:2 Badala yake watakuwamo wanyama wakali wa porini,
bundi watajaa katika nyumba zake.
Mbuni13:21 Mbuni: Au pepo wabaya. wataishi humo,
na majini13:21 majini: Au Ibilisi; namna ya pepo wa hadithi za Babuloni. yatachezea humo.
22Mbwamwitu watalia ndani ya ngome zake,
mbweha wataonekana ndani ya nyumba zao za anasa.
Wakati wa Babuloni umekaribia,
wala siku zake hazitaongezwa.”
Isaya13;1-22
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.
No comments:
Post a Comment