|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu wetu katika yote...
Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetuAsante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu
Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni Neema yako yatutosha Mungu wetu..!
Lakini Petro alisimama pamoja na wale kumi na mmoja akaanza kuwahutubia watu kwa sauti kubwa: “Ndugu Wayahudi nanyi nyote mnaokaa hapa Yerusalemu, sikilizeni kwa makini maneno yangu. Watu hawa hawakulewa kama mnavyodhani; mbona ni saa tatu tu asubuhi?
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti, Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
Ukweli ni kwamba jambo hili ni lile alilosema nabii Yoeli: ‘Katika siku zile za mwisho, asema Bwana, nitawamiminia binadamu wote Roho wangu. Watoto wenu wa kiume na wa kike watatoa unabii, vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe
Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama inavyokupendeza wewe Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...
Naam, hata watumishi wangu wa kiume na kike, nitawamiminia Roho wangu siku zile, nao watatoa unabii.
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao Nuru yako ikaangaze katika maisha yao Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele Amina....!!!
Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana kwakuwanami/kunisoma Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea kama inavyompendeza yeye Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba ukae nanyi daima.... Nawapenda. |
Moabu inaomba msaada kutoka Yerusalemu
1Pelekeni wanakondoo kwa mtawala wa nchi,
pelekeni kutoka Sela jangwani mpaka mlimani Siyoni.
2Kama ndege wanavyohangaika na kurukaruka,
wakiwa wamefukuzwa kutoka viota vyao,
ndivyo walivyo mabinti wa Moabu
kwenye vivuko vya Arnoni.
3Wamoabu wanawaambia watu wa Yuda,
“Tupeni mwongozo, tuamulieni.
Enezeni ulinzi wenu juu yetu,
kama vile usiku uenezavyo kivuli chake.
Tuficheni sisi wakimbizi;
msitusaliti sisi tuliofukuzwa.
4Wakimbizi wa Moabu waishi kwenu,
muwe kimbilio lao mbali na mwangamizi.”
Mdhalimu atakapokuwa ametoweka,
udhalimu utakapokuwa umekoma,
na wavamizi kutoweka nchini,
5utawala adili utazinduliwa katika maskani ya Daudi,
mtawala apendaye kutenda haki,
na mwepesi wa kufanya yaliyo sawa;
atatawala humo kwa uaminifu.
6Watu wa Yuda wanasema hivi:
“Tumesikia juu ya kiburi cha Moabu,
tunajua jinsi alivyojivuna mno;
tumesikia juu ya majivuno, kiburi na ufidhuli wake;
lakini majivuno yake hayo ni bure.”
7Sasa Wamoabu wanalia;
wote wanaomboleza juu ya nchi yao.
Ombolezeni kwa pigo hilo kubwa,
na juu ya maandazi ya zabibu za Kir-haresethi.
8Mashamba ya Heshboni yamefifia.
Kadhalika na zabibu za Sibma
ambazo ziliwalevya wakuu wa mataifa
zikafika Yazeri na kusambaa hata jangwani,
chipukizi zake zikafika hata ngambo ya bahari.
9Kwa hiyo ninalia pamoja na Yazeri
kwa ajili ya mizabibu ya Sibma.
Machozi yananitoka kwa ajili yenu,
enyi miji ya Heshboni na Eleale;
maana vigelegele vya mavuno ya matunda,
vigelegele vya mavuno ya nafaka vimetoweka.
10Furaha na shangwe zimetoweka katika shamba la rutuba.
Kwenye mizabibu hakuna kuimba tena,
wala kupiga vigelegele.
Hakuna tena kukamua zabibu shinikizoni,
sauti za furaha za mavuno zimekomeshwa.
11Hivyo, nafsi yangu yalilia Moabu kama kinubi,
na moyo wangu kwa ajili ya mji wa Kir-heresi.
12Watu wa Moabu wanapojitokeza kuabudu mungu wao,
wanapojichosha huko juu mahali pa ibada,
wanapokwenda mahali pao patakatifu kusali,
hawatakubaliwa.
13Hili ndilo jambo alilosema Mwenyezi-Mungu wakati uliopita kuhusu Moabu. 14Lakini sasa Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Baada ya miaka mitatu kamili, ikihesabiwa kama mfanyakazi anavyohesabu siku zake, fahari ya Moabu itakwisha. Ingawa watu wake ni wengi, watakaobaki hai watakuwa wachache na wanyonge.”
Isaya16;1-14
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.
No comments:
Post a Comment