Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 23 September 2019

Kikombe Cha Asubuhi;Isaya 17....


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Haleluyah ni siku/wiki nyingine tena Mungu wetu ametuchagua

na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Si kwamba sisi tumetenda mema sana wala si kwa nguvu zetu
si kwa utashi wetu wala si kwa akili zetu si kwamba sisi
ni wazuri mno si kwa uwezo wetu sisi kuwa hivi tulivyo leo hii
Ni kwa rehema/neema zake ni kwa mapenzi yake Mungu wetu....

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...
Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari kwa majukumu yetu
Sifa na Utukufu tunakurudshia Mungu wetu....!!

Nitatenda miujiza juu angani, na ishara chini duniani; kutakuwa na damu, moto na moshi mzito; jua litatiwa giza, na mwezi utakuwa mwekundu kama damu, kabla ya kutokea ile siku kuu na tukufu ya Bwana. Hapo, yeyote atakayeomba kwa jina la Bwana, ataokolewa.’
Tazama jana imepita ee Mungu wetu leo ni siku mpya na kesho ni siku nyingine Jehovah tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
 Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Jehovah usitutie majaribu Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote
Yahweh tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona
Kwakupigwa kwake sisi tumepata kupona....

“Wananchi wa Israeli, sikilizeni maneno haya! Yesu wa Nazareti alikuwa mtu ambaye mamlaka yake ya kimungu yalithibitishwa kwenu kwa miujiza, maajabu na ishara Mungu alizofanya kati yenu kwa njia yake, kama mnavyojua.
Yahweh tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe

Baba wa Mbinguni tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu
Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu
Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu
Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...

Kufuatana na mpango wake mwenyewe Mungu alikwisha amua kwamba Yesu angetiwa mikononi mwenu; nanyi mkamuua kwa kuwaachia watu wabaya wamsulubishe. Lakini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, akamwokoa katika maumivu ya kifo kwa maana haingewezekana kabisa kifo kimfunge.
Mungu wetu tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
 kila mmoja na mahitaji yake 
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe
Baba wa Mbinguni ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia zako
wakasimamie Neno lako nalo likaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kuomba kwetu
Mungu wetu ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina...!!

Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami
Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea 
kama inavyompendeza yeye....
Nawapenda.

Mungu ataadhibu Ashuru na Israeli
1 Kauli ya Mungu dhidi ya Damasko.
“Damasko utakoma kuwa mji;
utakuwa rundo la magofu.
2Mitaa yake imeachwa mahame milele.
Itakuwa makao ya makundi ya wanyama,
wala hakuna mtu atakayewatisha.
3Ngome za kujihami za Efraimu zitatoweka,
na utawala wa Damasko utakwisha.
Waashuru ambao watabaki hai,
watakuwa na fedheha kama wazawa wa Israeli.
Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimenena.
Watakaosalia katika Israeli
4“Siku hiyo, fahari ya Yakobo itaporomoshwa,
na unono wake ataupoteza.
5Atakwisha kama shamba lililovunwa,
atafanyiwa kama mvunaji avunavyo nafaka,
atakuwa kama shamba lililovunwa bondeni Refaimu.
6Atabakiziwa wachache kama vile baada ya zeituni:
Zeituni mbili, tatu katika tawi la juu;
nne, tano katika matawi ya mti uzaao sana.17:6 uzaao sana: Kufuatana na hati ya Kumrani; Kiebrania: Juu ya tawi lake, aliyezaa sana.
Mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nimenena.”
Mwisho wa kuabudu sanamu
7Siku hiyo, watu watamwangalia Muumba wao, na kuelekeza macho yao kwa huyo Mtakatifu wa Israeli. 8Hawatazielekea tena madhabahu ambazo ni kazi za mikono yao wenyewe, wala kuzitazamia tena kazi za mikono yao wenyewe, yaani sanamu za mungu Ashera na madhabahu za kufukizia ubani.
9Siku hiyo miji yao imara itaachwa mahame, kama miji ambayo Wahivi na Waamori17:9 Waamori: Kadiri ya Septuaginta; Kiebrania: Kama magofu ya msitu na kilele cha mlima. waliihama walipokuwa wakiwakimbia wazawa wa Israeli. Kila kitu kitakuwa uharibifu.
10Maana wewe Israeli umemsahau Mungu aliyekuokoa,
hukumkumbuka Mwamba wa usalama wako.
Kwa hiyo, hata mkipanda mimea ya Baali,17:10 ya Baali: Kiebrania: Ya yule mzuri; labda jina la sifa la Baali.
na kuiweka wakfu kwa mungu wa kigeni;
11hata mkiifanya ikue siku hiyohiyo mliyoipanda
na kuifanya ichanue asubuhi hiyohiyo,
mavuno yenu yatatoweka
siku hiyo ya balaa na maumivu yasiyoponyeka.
Mataifa adui yanashindwa
12Lo! Ngurumo ya watu wengi!
Wananguruma kama bahari.
Lo! Mlio wa watu wa mataifa!
Yanatoa mlio kama wa maji mengi.
13Mataifa yananguruma kama ngurumo ya maji mengi,
lakini Mungu atayakemea, nayo yatakimbilia mbali.
Yatafukuzwa kama makapi mlimani mbele ya upepo;
kama vumbi litimuliwalo na kimbunga.
14Wakati wa jioni yanaleta hofu kuu,
lakini kabla ya asubuhi yametoweka!
Hilo ndilo litakalowapata wanaonyakua mali yetu,
ndilo litakalowapata wanaotupora.

Isaya17;1-14

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: