|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu wetu katika yote...
Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetuAsante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu
Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni Neema yako yatutosha Mungu wetu..!
Kisha Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Moyo wa Farao umekuwa mgumu. Anakataa kuwaacha Waisraeli waondoke. Basi, nenda ukakutane naye kesho asubuhi, wakati anapokwenda mtoni Nili. Mngojee kando ya mto. Chukua mkononi mwako ile fimbo iliyogeuka kuwa nyoka.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza, tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti, Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
Kisha mwambie hivi, Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Waebrania, amenituma kwako, naye asema hivi, ‘Waache watu wangu waende zao ili wanitumikie jangwani, lakini mpaka sasa wewe hupendi kutii.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe
Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama inavyokupendeza wewe Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...
Basi, Mwenyezi-Mungu asema kwamba sasa utamtambua yeye ni nani. Nitayapiga maji ya mto Nili kwa fimbo hii, na maji yote yatageuka kuwa damu. Samaki waliomo mtoni Nili watakufa, mto wote utanuka vibaya, na Wamisri watachukia kabisa kunywa maji yake.’”
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao Nuru yako ikaangaze katika maisha yao Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele Amina....!!!
Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana kwakuwanami/kunisoma Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea kama inavyompendeza yeye Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba ukae nanyi daima.... Nawapenda. |
Mwenyezi-Mungu ataiadhibu dunia
1Sasa Mwenyezi-Mungu anaiharibu dunia
na kuifanya tupu.
Atausokota uso wa dunia
na kuwatawanya wakazi wake.
2Kila mtu atapatwa na mambo yaleyale:
Mtu wa kawaida na kuhani;
mtumwa na bwana wake;
mjakazi na bibi yake;
mnunuzi na mwuzaji;
mkopeshaji na mkopaji;
mdai na mdaiwa.
3Dunia itaharibiwa kabisa na kuangamizwa;
Mwenyezi-Mungu ametamka hayo.
4Dunia inakauka na kunyauka;
ulimwengu unafadhaika na kunyauka;
mbingu zinafadhaika pamoja na dunia.
5Watu wameitia najisi dunia
maana wamezivunja sheria za Mungu,
wamezikiuka kanuni zake,
wamelivunja agano lake la milele.
6Kwa sababu hiyo laana inaitokomeza dunia,
wakazi wake wanateseka kwa makosa yao.
Wakazi wa dunia wamepungua,
ni watu wachache tu waliosalia.
7Mizabibu inanyauka,
divai inakosekana.
Wote waliokuwa wenye furaha
sasa wanasononeka kwa huzuni.
8Mdundo wa vigoma umekoma,
nderemo na vifijo vimetoweka;
midundo ya vinubi imekomeshwa.
9Hakuna tena kunywa divai na kuimba;
mvinyo umekuwa mchungu kwa wanywaji.
10Mji uliohamwa umejaa uharibifu;
kila nyumba imefungwa asiingie mtu.
11Kuna kilio barabarani kwa kukosa divai;
shangwe yote imekoma,
furaha imetoweka duniani.
12Mji ni magofu matupu;
malango yake yamevunjwavunjwa.
13Kama vile zeituni chache tu juu ya mzeituni
au tini chache tu juu ya mtini
baada ya kumaliza mavuno,
ndivyo itakavyokuwa katika nchi zote:
Watu wachache watabakia hai.
14Watakaosalia watapaza sauti,
wataimba kwa shangwe.
Kutoka magharibi watatangaza ukuu wa Mwenyezi-Mungu,
15nao wakazi wa mashariki watamsifu.
Watu wa mbali watalisifu
jina la Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli.
16Tunasikia nyimbo za sifa kutoka miisho ya dunia,
nyimbo za kumsifu Mungu aliye mwadilifu.
Lakini mimi ninanyongonyea,
naam, ninanyongonyea.
Ole wangu mimi!
Wasaliti wanaendelea kuwa wasaliti,
usaliti wao unazidi kuwa mbaya zaidi.
17Hofu, mashimo na mitego,
hivi ndivyo vinavyowangojeni enyi wakazi wa dunia.
18Atakayeikimbia hofu atatumbukia shimoni;
atakayetoka shimoni atanaswa mtegoni.
Madirisha ya mbinguni24:18 Madirisha ya mbinguni: Yaani tufani au gharika, Taz Mwa 7:11; 8:2. yamefunguliwa,
misingi ya dunia inatikisika.
19Dunia inavunjikavunjika,
inapasuka na kutikiswatikiswa.
20Inapepesuka kama mlevi,
inayumbayumba kama kibanda.
Imelemewa na mzigo wa dhambi zake
nayo itaanguka wala haitainuka tena.
21Siku ile Mwenyezi-Mungu ataliadhibu jeshi la angani24:21 jeshi la angani: Yaani jua, mwezi na nyota ambavyo baadhi ya watu wa nyakati hizo walifikiri kuwa pepo wabaya.
kadhalika na wafalme wa duniani.
22Wote watakusanywa kama wafungwa shimoni;
watafungwa gerezani pamoja kwa miaka mingi,
na baada ya muda huo atawaadhibu.
23Kisha mwezi utaaibishwa,
nalo jua litaona aibu kuangaza,
kwa kuwa Mwenyezi-Mungu wa majeshi
atatawala huko Yerusalemu katika mlima Siyoni;
ataonesha wazee wa watu wake utukufu wake.
Isaya24;1-23
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.
No comments:
Post a Comment