|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu wetu katika yote...
Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetuAsante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu
Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni Neema yako yatutosha Mungu wetu..!
Kwa hiyo basi, mwambie mtumishi wangu Daudi: ‘Mwenyezi-Mungu wa majeshi anasema hivi: Nilikutoa malishoni ulipokuwa unawachunga kondoo, ili uwe mkuu wa watu wangu Israeli. Tangu wakati huo nimekuwa pamoja nawe kokote ulikokwenda na nimewaangamiza maadui zako wote mbele yako. Nitakufanya kuwa maarufu kama wakuu wengine wa dunia.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza, tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti, Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
Nami nitawachagulia watu wangu wa Israeli mahali pa kuishi niwapandikize, ili waishi mahali pao wenyewe, wasisumbuliwe tena. Nao watu wakatili wanaotumia nguvu hawatawatesa tena kama hapo awali, tangu wakati nilipowateua waamuzi juu ya watu wangu Israeli; mimi nitawashinda maadui zako wote. Zaidi ya yote, mimi Mwenyezi-Mungu nakutangazia kuwa nitakujengea nyumba.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe
Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama inavyokupendeza wewe Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...
Siku zako zitakapotimia za kujiunga na babu zako, nitamfanya mmoja wa watoto wako, wewe mwenyewe awe mfalme; nami nitauimarisha ufalme wake. Yeye ndiye atakayenijengea nyumba; nami nitahakikisha kwamba ufalme wake unadumu milele. Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu; lakini sitamwondolea fadhili zangu kama vile nilivyomwondolea Shauli aliyekutangulia. Bali nitamwimarisha katika nyumba yangu na katika ufalme wangu milele, na kiti chake cha enzi kitakuwa imara daima.’” Nathani alimwelezea Daudi mambo yote haya kulingana na maono yote.
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao Nuru yako ikaangaze katika maisha yao Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele Amina....!!!
Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana kwakuwanami/kunisoma Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea kama inavyompendeza yeye Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba ukae nanyi daima.... Nawapenda. |
Ujumbe dhidi ya Yerusalemu
1Ole wako Yerusalemu, madhabahu ya Mungu;29:1 madhabahu ya Mungu; ni tafsiri ya neno la Kiebrania Arieli ambalo katika Ezekieli 43:15,16 linamaanisha sehemu ya juu ya madhabahu. Arieli hapa ni jina la kishairi la Yerusalemu!
mji ambamo Daudi alipiga kambi yake!
Miaka yaja na kupita,
na sikukuu zako zaendelea kufanyika;
2lakini mimi Mungu nitauhuzunisha Yerusalemu,
nako kutakuwa na vilio na maombolezo,
mji wenyewe utakuwa kama madhabahu
iliyolowa damu ya watu waliouawa.
3Mimi nitapanga jeshi dhidi ya Yerusalemu,
nami nitauzingira na kuushambulia.
4Utaangushwa mbali sana ndani ya ardhi;
kutoka huko mbali utatoa sauti;
maneno yako yatatoka huko chini mavumbini;
sauti yako itatoka ardhini kama ya mzimu.
5Kundi la maadui zako litakuwa kama vumbi laini,
waliokutendea ukatili watakuwa kama makapi.
Hayo yatafanyika ghafla.
6Mwenyezi-Mungu wa majeshi atakuja kukusaidia;
atakuja na ngurumo, tetemeko la ardhi na sauti kubwa;
atakuja na kimbunga, tufani na moto uunguzao.
7Hapo, kundi la mataifa yote yanayoshambulia Yerusalemu,
wote wanaoshambulia ngome yake na kuutia wasiwasi,
watatoweka kama ndoto, kama maono ya usiku.
8Mataifa yote yanayoushambulia mji wa Yerusalemu
yatakuwa kama mtu mwenye njaa anayeota anakula
lakini aamkapo bado anaumwa na njaa!
Au mtu mwenye kiu anayeota kuwa anakunywa,
lakini anaamka mdhaifu, bado ana kiu.
Hatari ya kupuuza maonyo
9Endeleeni kuwa wapumbavu na kuduwaa!
Jipofusheni na kuwa vipofu!
Leweni lakini si kwa divai;
pepesukeni lakini si kwa pombe.
10Mwenyezi-Mungu amewamiminia hali ya usingizi mzito;
ameyafumba macho yenu enyi manabii,
amefunika vichwa vyenu enyi waonaji.
11Basi, kwenu nyinyi maono yote haya ni kama ujumbe ulioandikwa katika kitabu kilichofungwa kwa mhuri. Ukimpelekea mtu yeyote ajuaye kusoma, ukamwambia, “Hebu nisomee kitabu hiki,” atasema, “Siwezi kukisoma kwani kimefungwa kwa mhuri.” 12Na ukimpa mtu yeyote asiyejua kusoma, ukamwambia, “Hebu nisomee kitabu hiki,” atakuambia, “Sijui kusoma.”
13 29:13 Taz Mat 15:8-9 Marko 7:6-7 Bwana asema,
“Watu hawa huja kuniabudu kwa maneno matupu,
hali mioyo yao iko mbali nami.
Wananiheshimu kulingana na mapokeo ya watu tu,
jambo walilojifunza wao wenyewe.
14Hivyo, nitawatenda tena watu hawa maajabu,
mambo ya ajabu na ya kushangaza.
Nao wenye hekima wao wataishiwa hekima,
na busara ya wenye busara wao itatoweka.
Tumaini siku za usoni
15“Ole mnaomficha Mwenyezi-Mungu mipango yenu,
mnaotenda matendo yenu gizani
na kusema: ‘Hamna atakayetuona;
nani awezaye kujua tunachofanya?’
16 29:16 Taz Isa 45:9; Rom 9:20 Nyinyi mnafanya mambo kinyume kabisa!
Je, mfinyanzi na udongo ni hali moja?
Chombo hakiwezi kumwambia aliyekitengeneza:
‘Wewe hukunitengeneza.’
Kilichofinyangwa hakiwezi kumwambia aliyekiumba,
‘Wewe hujui chochote.’”
Marekebisho makubwa
17Bado kidogo tu,
msitu wa Lebanoni utageuzwa kuwa shamba lenye rutuba,
na shamba lenye rutuba kuwa msitu.
18Siku hiyo viziwi watasikia ujumbe ukisomwa kitabuni
na kutoka gizani vipofu wataanza kuona.
19Wanyofu watapata furaha mpya kwa Mwenyezi-Mungu,
na maskini wa watu watashangilia kwa furaha
kwa sababu ya Mungu, Mtakatifu wa Israeli.
20Majitu makatili yataangamizwa,
wenye kumdhihaki Mungu watakwisha,
wote wanaootea kutenda maovu watatokomezwa.
21Watatoweka wale wanaopotosha kesi ya mtu mahakamani,
watu wanaowafanyia hila mahakimu
na wasemao uongo kuwanyima haki yao wasio na hatia.
22Kwa hiyo, Mwenyezi-Mungu aliyemkomboa Abrahamu,
asema hivi kuhusu wazawa wa Yakobo:
“Wazawa wa Yakobo hawataaibishwa tena,
hawatainamisha vichwa vyao tena kwa aibu.
23Watakapowaona watoto wao,
watoto niliowajalia mimi mwenyewe,
watalitukuza jina langu mimi Mtakatifu wa Yakobo;
watakuwa na uchaji kwangu mimi Mungu wa Israeli.
24Waliopotoka rohoni watapata maarifa
na wenye kununa watakubali kufunzwa.”
Isaya29;1-24
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.
No comments:
Post a Comment