|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu wetu katika yote...
Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetuAsante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu
Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni Neema yako yatutosha Mungu wetu..!
“Basi sasa, ewe Mwenyezi-Mungu, liimarishe milele neno lako ulilosema kunihusu mimi mtumishi wako na kuhusu jamaa yangu. Nalo jina lako litatukuzwa milele, nao watu watasema, ‘Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, ndiye Mungu wa Israeli!’ Na jamaa yangu, mimi Daudi mtumishi wako, itaimarika mbele yako.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti, Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
Maana ee Mungu wangu nimepata ujasiri kukuomba kwa sababu wewe, umenifunulia ukisema ya kwamba utanijengea nyumba. Sasa ee Mwenyezi-Mungu, wewe ndiwe Mungu, umeniahidi mimi mtumishi wako jambo hili jema;
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe
Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama inavyokupendeza wewe Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...
kwa hiyo nakuomba uibariki nyumba yangu, mimi mtumishi wako, ili idumu milele mbele yako; kwani unachobariki wewe, huwa kimebarikiwa milele.”
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao Nuru yako ikaangaze katika maisha yao Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele Amina....!!!
Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana kwakuwanami/kunisoma Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea kama inavyompendeza yeye Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba ukae nanyi daima.... Nawapenda. |
Misri haitaweza kusaidia
1Ole wao wale waendao Misri kuomba msaada,
ole wao wanaotegemea farasi,
wanaotegemea wingi wa magari yao ya vita,
na nguvu za askari wao wapandafarasi,
nao hawamtegemei Mtakatifu wa Israeli,
wala hawamwombi Mwenyezi-Mungu shauri!
2Mungu ni mwenye busara na huleta maangamizi.
Habadilishi tamko lake;
ila yuko tayari kuwakabili watu waovu
kadhalika na wasaidizi wa watendao mabaya.
3Wamisri ni binadamu tu wala si Mungu;
farasi wao nao ni wanyama tu, si roho.
Mwenyezi-Mungu akiunyosha mkono wake,
taifa linalotoa msaada litajikwaa,
na lile linalosaidiwa litaanguka;
yote mawili yataangamia pamoja.
Mungu ataulinda mji wa Yerusalemu
4Mwenyezi-Mungu aliniambia:
“Kama vile simba au mwanasimba angurumavyo
kuyakinga mawindo yake,
hata kundi la wachungaji likiitwa kumkabili,
yeye hatishiki kwa kelele zao,
wala hashtuki kwa sauti zao.
Ndivyo atakavyoshuka Mwenyezi-Mungu wa majeshi
kupigana juu ya mlima Siyoni na kilima chake.
5Kama ndege arukavyo juu ya viota vyake,
ndivyo Mwenyezi-Mungu atakavyoulinda Yerusalemu,
ataulinda na kuukomboa,
atauhifadhi na kuuokoa.
6Enyi Waisraeli,
mrudieni huyo mliyemsaliti vibaya.
7Wakati utafika ambapo nyote
mtavitupilia mbali vinyago vyenu
vya fedha na dhahabu ambavyo
mmejitengenezea kwa mikono yenu,
vikawakosesha.
8Hapo Waashuru watauawa kwa upanga,
lakini si kwa upanga wa binadamu;
naam, wataangamizwa kwa upanga
ambao ni zaidi ya ule wa binadamu.
Waashuru watakimbia
na vijana wao watafanyizwa kazi za kitumwa.
9Mfalme wao atatoroka kwa hofu,
na maofisa wao wataiacha bendera yao kwa woga.
Hayo ameyatamka Mwenyezi-Mungu
ambaye moto wake umo mjini Siyoni,
naam, tanuri lake limo mjini Yerusalemu.”
Isaya31;1-9
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.
No comments:
Post a Comment