|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu katika yote....
Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana Mungu wa walio hai,Mungu mwenye huruma,Mungu wa upendo Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...Asante kwa wema na fadhili zako kwetu Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!
Mfalme Ahasuero alitoza kodi watu wa bara na pwani. Matendo yake yote makuu na ya ajabu, pamoja na simulizi kamili kuhusu jinsi alivyompandisha cheo Mordekai na kumtunukia heshima kuu, yote yameandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za wafalme wa Media na Persia.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona.... Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomna ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe...
Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Yahwe ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona,masikio ya kusikia sauti yako na kuitii.. Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako,tukasimamie Neno lako,amri na sheria zako siku zote za maisha yetu... Ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu,ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....
Mordekai, Myahudi, alikuwa wa kwanza chini ya mfalme Ahasuero katika madaraka. Alipendwa na kuheshimiwa na Wayahudi, maana aliwafanyia mema watu wake na kuwatakia amani wazawa wao wote.
Tazama watoto wako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu kila mmoja na mahitaji yake Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipo kwenda kinyume nawe Yahweh tunaomba ukawape neema ya kuweza kujiombea,kufuata njia zako nazo zikawaweke huru... Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele... Amina...!!
Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,Baba wa Mbinguni aendelee kuwatendea sawasawa na mapenzi yake... Nawapenda. |
Maafa kwa mwangamizi
1Ole wako ewe mwangamizi,
unayeangamiza bila wewe kuangamizwa!
Ole wako wewe mtenda hila,
ambaye hakuna aliyekutendea hila!
Utakapokwisha kuangamiza
wewe utaangamizwa!
Utakapomaliza kuwatendea watu hila
wewe utatendewa hila.
2Ee Mwenyezi-Mungu, utuonee huruma,
kwako tumeliweka tumaini letu.
Uwe kinga yetu kila siku,
wokovu wetu wakati wa taabu.
3Kwa kishindo cha sauti yako watu hukimbia;
unapoinuka tu, mataifa hutawanyika.
4Maadui zao wanakusanya mateka,
wanayarukia kama panzi.
5Mwenyezi-Mungu ametukuka,
yeye anaishi juu mbinguni.
Ameujaza Siyoni haki na uadilifu.
6Enyi watu wa Yerusalemu,
Mwenyezi-Mungu atawajalieni usalama,
atawaokoa na kuwapa hekima na maarifa.
Hazina yenu kuu ni kumcha Mwenyezi-Mungu.
7Haya, mashujaa wao wanalia,
wajumbe wa amani wanaomboleza.
8Barabara kuu zimebaki tupu;
hamna anayesafiri kupitia humo.
Mikataba inavunjwa ovyo,
mashahidi wanadharauliwa.
Hamna anayejali tena maisha ya binadamu.
9Nchi inaomboleza na kunyauka;
misitu ya Lebanoni imekauka,
bonde zuri la Sharoni limekuwa jangwa,
huko Bashani na mlimani Karmeli
miti imepukutika majani yake.
Mwenyezi-Mungu awaonya maadui zake
10Mwenyezi-Mungu asema hivi:
“Sasa mimi nitainuka;
sasa nitajiweka tayari;
sasa mimi nitatukuzwa.
11Mipango yenu yote ni kama makapi,
na matokeo yake ni takataka tupu.
Pumzi yangu33:11 Pumzi yangu: Kadiri ya hati kadhaa za kale; makala ya Kiebrania ina pumzi yenu. itawaangamiza kama moto.
12Watu watakuwa kama wamechomwa kuwa majivu,
kama miiba iliyokatwa na kuteketezwa motoni.
13Sikilizeni mambo mliyofanya enyi mlio mbali,
nanyi mlio karibu kirini uwezo wangu.”
14Wenye dhambi katika Siyoni wanaogopa,
wasiomcha Mungu wanatetemeka na kusema:
“Nani awezaye kuukaribia moto huu mkali?
Nani awezaye kustahimili miali ya moto wa milele?”
15Ni mtu aishiye kwa uadilifu na asemaye ukweli;
mtu anayedharau kabisa utajiri wa dhuluma,
anayekataa hongo kata kata,
asiyekubali kamwe kusikia mipango ya mauaji,
wala hakubali macho yake yaone maovu.
16Mtu wa namna hiyo anaishi juu,
mahali salama penye ngome na miamba;
chakula chake atapewa daima,
na maji yake ya kunywa hayatakosekana.
Wakati mzuri ujao
17Mtaweza kumwona mfalme katika fahari yake,
mtaiona nchi anayotawala, kubwa na pana.
18Mtafikiria tisho lililopita na kujiuliza,
“Wako wapi wale waliokadiria na kukisia kodi?
Wako wapi wale waliopeleleza ulinzi wetu?”
19Hamtawaona tena watu wale wenye kiburi,
wanaozungumza lugha isiyoeleweka.
20Tazameni Siyoni tunamofanya sikukuu zetu;
tazameni mji Yerusalemu, makao matulivu, hema imara;
vigingi vyake havitangolewa kamwe,
kamba zake hazitakatwa hata moja.
21Humo Mwenyezi-Mungu atatuonesha ukuu wake.
Kutakuwa na mito mikubwa na vijito,
ambamo meli za vita hazitapita,
wala meli kubwa kuingia.
22Maana Mwenyezi-Mungu ni hakimu wetu,
yeye ni mtawala wetu;
Mwenyezi-Mungu ni mfalme wetu,
yeye ndiye anayetuokoa.
23Ewe Siyoni, kamba zako zimelegea,
haziwezi kushikilia matanga yake,
wala kuyatandaza.
Lakini nyara nyingi zitagawanywa;
hata vilema wataweza kuchukua sehemu yao.
24Hakuna atakayesema tena ni mgonjwa;
watu watasamehewa uovu wao wote.
Isaya33;1-24
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.
No comments:
Post a Comment