Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 16 October 2019

Kikombe Cha Asubuhi;Isaya 34....


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante  Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu


Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni

Neema yako yatutosha  Mungu wetu..!

Msifuni Mwenyezi-Mungu! Nitamshukuru Mwenyezi-Mungu kwa moyo wangu wote, nikijumuika na jamii ya watu waadilifu. Matendo ya Mwenyezi-Mungu ni makuu mno! Wote wanaoyafurahia huyatafakari. Kila afanyacho kimejaa utukufu na fahari; uadilifu wake wadumu milele.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,
tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako

Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa  Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

Amesababisha matendo yake ya ajabu yakumbukwe; Mwenyezi-Mungu ni mwema na mwenye huruma. Huwapa chakula wenye kumcha; hasahau kamwe agano lake. Amewaonesha watu wake nguvu ya matendo yake, amewapa nchi za mataifa mengine ziwe mali yao. Matendo yake ni ya haki na ya kuaminika; kanuni zake zote ni za kutegemewa.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe



Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu  wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo 

Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...

Amri zake zadumu daima na milele; zimetolewa kwa haki na uadilifu. Aliwakomboa watu wake na kufanya nao agano la milele. Yeye ni mtakatifu na wa kutisha mno! Kumcha Mwenyezi-Mungu ni msingi wa hekima; wote wanaozitii amri zake hujaliwa busara. Sifa zake zadumu milele.
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba
 ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!


Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....

Nawapenda.

Mungu atawaadhibu maadui zake
1Karibieni mkasikilize enyi mataifa,
tegeni sikio enyi watu.
Sikiliza ee dunia na vyote vilivyomo,
ulimwengu na vyote vitokavyo humo!
2Mwenyezi-Mungu ameyakasirikia mataifa yote,
ameghadhabika dhidi ya majeshi yao yote.
Ameyapangia mwisho wao,
ameyatoa yaangamizwe.
3Maiti zao zitatupwa nje;
harufu ya maiti zao itasambaa;
milima itatiririka damu yao.
4 34:4 Taz Mat 24:29; Marko 13:25; Luka 21:26; Ufu 6:13-14 Jeshi lote la angani litaharibika,
anga zitakunjamana kama karatasi.
Jeshi lake lote litanyauka,
kama majani ya mzabibu yanyaukavyo,
naam, kama tunda la mtini linyaukavyo.
5 34:5-17 Taz Isa 63:1-6; Yer 49:7-22; Eze 25:12-14; 35:1-15; Amo 1:11-12; Oba Upanga wa Mungu uko tayari juu mbinguni.
Tazama, washuka kuwaadhibu Waedomu,
watu ambao ameamua kuwaangamiza.
6Upanga utalowa damu na kutapakaa mafuta,
kama kwa damu ya kondoo na mbuzi,
na mafuta ya figo za kondoo dume.
Maana Mwenyezi-Mungu atatoa kafara huko Bosra,
kutakuwa na mauaji makubwa nchini Edomu.
7Nyati wataangamia pamoja nao,
ndama kadhalika na mafahali.
Nchi italoweshwa damu,
udongo utarutubika kwa mafuta yao.
8Maana Mwenyezi-Mungu anayo siku ya kisasi;
mwaka wa kulipiza maadui wa Siyoni.
9Vijito vya Edomu vitatiririka lami,
udongo wake utakuwa madini ya kiberiti;
ardhi yake itakuwa lami iwakayo.
10 34:10 Taz Ufu 14:11; 19:3 Itawaka usiku na mchana bila kuzimika,
moshi wake utafuka juu milele.
Nchi itakuwa jangwa siku zote,
hakuna atakayepitia huko milele.
11Itakuwa makao ya kozi na nungunungu,
bundi na kunguru wataishi humo.
Mwenyezi-Mungu atawaletea ghasia,
na timazi la fujo kwa wakuu wake.
12Nchi itaitwa “Nchi bila Mfalme;”
wakuu wake wote wametoweka.
13Miiba itaota katika ngome zake,
viwavi na michongoma mabomani mwao.
Itakuwa makao ya mbwamwitu, maskani yao mbuni.
14Pakamwitu na fisi watakuwa humo,
majini34:14 majini: Taz 13:21 na maelezo. yataitana humo;
kwao usiku utakuwa mwanga,
na humo watapata mahali pa kupumzikia.
15Humo bundi watataga mayai na kuyaatamia,
wataangua vifaranga na kuviweka kivulini mwao.
Humo vipanga watakutania,
kila mmoja na mwenzake.
16Someni katika kitabu cha Mwenyezi-Mungu:
“Hakuna hata kiumbe kimoja kitakachokosekana,
kila kimoja kitakuwako na mwenzake.”
Maana Mwenyezi-Mungu mwenyewe ametamka hivyo,
roho yake itawakusanya hao wote.
17Mwenyezi-Mungu amepanga sehemu ya kila mmoja wao,
ametumia kamba kuwapimia nchi hiyo;
wataimiliki milele na milele,
wataishi humo kizazi hata kizazi.


Isaya34;1-17

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: