|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu wetu katika yote...
Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetuAsante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu
Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni Neema yako yatutosha Mungu wetu..!
Malaika wa Mwenyezi-Mungu aliondoka Gilgali, akaenda Bokimu, akawaambia Waisraeli, “Niliwatoa nchini Misri na kuwaleta katika nchi ambayo niliwaahidi kwa kiapo babu zenu. Nilisema kwamba sitalivunja agano langu nanyi kamwe. Na kwa upande wenu niliwaamuru msifanye agano na wenyeji wa nchi hii na kwamba madhabahu zao mtazibomoa. Lakini nyinyi hamkuitii amri yangu. Kwa nini mambo haya?
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza, tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti, Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
Kwa hiyo sasa nasema: Sitawafukuza tena wakazi wa nchi hii bali watawataabisha, nayo miungu yao itakuwa mtego kwenu.” Malaika wa Mwenyezi-Mungu alipowaambia watu wote wa Israeli maneno haya, walipaza sauti zao na kulia. Wakapaita mahali hapo Bokimu. Hapo wakamtolea sadaka Mwenyezi-Mungu.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe
Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama inavyokupendeza wewe Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...
Baada ya Yoshua kuwaaga Waisraeli, kila mmoja alikwenda kwenye eneo lake alilogawiwa ili kuimiliki nchi. Waisraeli walimtumikia Mwenyezi-Mungu siku zote za maisha ya Yoshua na baada ya kifo chake muda wote walioishi wale wazee waliosalia ambao waliyaona matendo makuu ambayo Mwenyezi-Mungu aliwatendea Waisraeli.
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao Nuru yako ikaangaze katika maisha yao Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele Amina....!!!
Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana kwakuwanami/kunisoma Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea kama inavyompendeza yeye Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba ukae nanyi daima.... Nawapenda. |
1“Wewe Beli umeanguka;
Nebo umeporomoka.
Wakati mmoja watu walibeba sanamu zenu.
Sasa wanazibeba mgongoni mwa wanyama,
hao wanyama wachovu wamelemewa.
2Nyinyi mmeanguka na kuvunjika,
hamwezi kuviokoa vinyago vyenu;
nyinyi wenyewe pia mtapelekwa uhamishoni!
3“Sikilizeni enyi wazawa wa Yakobo,
nisikilizeni enyi mabaki ya watu wangu wa Israeli.
Mimi niliwatunzeni tangu mlipozaliwa;
niliwabebeni tangu tumboni mwa mama yenu.
4Mimi ni yuleyule hata katika uzee wenu;
hata katika uzee wenu mimi nitawabeba.
Nilifanya hivyo kwanza,
nitafanya hivyo tena.
Nitawabeba nyinyi na kuwaokoa.
5“Mtanifananisha na nani, tufanane?
Je, mwaweza kunilinganisha na nani, tulingane?
6Watu humimina dhahabu kutoka mifuko yao,
hupima fedha kwenye mizani zao,
wakamwajiri mfua dhahabu atengeneze sanamu
kisha huisujudu na kuiabudu!
7Hujitwisha sanamu hiyo mabegani, wakaibeba,
kisha huiweka mahali pake, ikakaa papo hapo;
kamwe haiwezi hata kusogea kutoka hapo ilipo.
Mtu akiililia, haiwezi kumwitikia,
wala haiwezi kumwokoa mtu katika taabu zake.
8“Kumbukeni jambo hili na kutafakari,
liwazeni akilini mwenu enyi wakosefu.
9Kumbukeni mambo niliyotenda hapo kale!
Mimi ndimi Mungu na hakuna mwingine;
naam, mimi ni Mungu, wala hakuna mwingine kama mimi.
10Nilitangaza mambo ya mwisho tangu mwanzo,
tangu kale nilitangaza mambo yatakayotukia.
Lengo langu litatimia;
mimi nitatekeleza nia yangu yote.
11Ninamwita tai wangu kutoka mashariki,
naam, msiri wangu kutoka nchi ya mbali.
Mimi nimenena na nitayafanya;
mimi nimepanga nami nitatekeleza.
12“Nisikilizeni, enyi wenye vichwa vigumu,
nisikilizeni enyi mlio mbali na ukombozi.
13Siku ya kuwakomboa naileta karibu,
haiko mbali tena;
siku ya kuwaokoeni haitachelewa.
Nitauokoa mji wa Siyoni,
kwa ajili ya Israeli, fahari yangu.
Isaya46;1-13
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.
No comments:
Post a Comment