Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday, 7 November 2019

Kikombe Cha Asubuhi;Isaya 50....




Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu katika yote....

Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi
Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana
Mungu wa walio hai,Mungu  mwenye huruma,Mungu wa upendo
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...
Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu

Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!

Baada ya kusema hivyo, mzozo mkali ulitokea kati ya Mafarisayo na Masadukayo na mkutano ukagawanyika sehemu mbili. Kisa chenyewe kilikuwa hiki, Masadukayo hushikilia kwamba wafu hawafufuki, hakuna malaika, na roho nazo hazipo. Lakini Mafarisayo husadiki hayo yote matatu.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,
tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako

Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote 
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema
ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe
na yule mwovu na kazi zake zote
Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu
ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

Kelele ziliongezeka na baadhi ya waalimu wa sheria wa kikundi cha Mafarisayo walisimama na kutoa malalamiko yao kwa nguvu: “Hatuoni chochote kilicho kiovu katika mtu huyu; huenda ikawa kwamba roho au malaika ameongea naye.”
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomna ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe...


Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Yahwe ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona,masikio ya kusikia sauti yako na kuitii..
Baba wa Mbinguni  tunaomba ukatupe neema ya kufuata
njia zako,tukasimamie Neno lako,amri na sheria zako
siku zote za maisha yetu...
Ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu,ukatufanye chombo chema
ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....

Mzozo ulizidi kuwa mwingi hata mkuu wa jeshi akaogopa kwamba Paulo angeraruliwa vipandevipande. Kwa hiyo, aliwaamuru askari wake kuingia kati ya lile kundi, wamtoe Paulo na kumrudisha ndani ya ngome. Usiku uliofuata, Bwana alisimama karibu na Paulo, akamwambia, “Jipe moyo! Umenishuhudia hapa Yerusalemu, utafanya vivyo hivyo mjini Roma.”
Tazama watoto wako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
kila mmoja na mahitaji yake
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipo kwenda kinyume nawe
Yahweh tunaomba ukawape neema ya kuweza kujiombea,kufuata njia zako nazo zikawaweke huru...
Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele...
Amina...!!


Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,Baba wa Mbinguni aendelee kuwatendea sawasawa na mapenzi yake...
Nawapenda.

1Mwenyezi-Mungu asema hivi:
“Kama nimempa talaka mama yako Yerusalemu,
hati ya talaka iko wapi?
Au kama niliwauza utumwani,
yuko wapi basi, huyo niliyemwuzia?
Kumbukeni mliuzwa utumwani kwa maovu yenu,
mama yenu alifukuzwa kwa makosa yenu.
2“Nilipokuja kwa nini sikukuta mtu?
Nilipoita mbona hamkuitikia?
Je, mkono wangu ni mfupi nisiweze kuwaokoeni?
Je, sina nguvu ya kuwakomboa?
Tazama! Kwa kuikemea kidogo bahari hukauka,
na mito nikaifanya kuwa jangwa,
samaki wake wakafa na kunuka kwa kukosa maji.
3Mimi hulivika anga giza,
na kulivalisha vazi la kuomboleza.”
Mtumishi wa Mwenyezi-Mungu
4Bwana Mungu amenipa ufasaha wa lugha,
niwatie moyo wale waliochoka.
Kila asubuhi hunipa hamu
ya kusikiliza anayotaka kunifunza.
5Bwana Mungu amenifanya msikivu,
nami sikuwa mkaidi
wala kugeuka mbali naye.
6 50:6 Taz Mat 26:67; Marko 14:65 Mgongo wangu niliwaachia walionipiga,
mashavu yangu waliozingoa ndevu zangu;
walioniaibisha na kunitemea mate,
sikujificha mbali nao.
7Bwana Mungu hunisaidia,
kwa hiyo siwezi kufadhaika.
Uso wangu nimeukaza kama jiwe;
najua kwamba sitaaibishwa.
8Mtetezi wangu yuko karibu.
Ni nani atakayepingana nami?
Na aje tusimame mahakamani.
Adui yangu ni nani?
Na ajitokeze mbele basi.
9Tazama Bwana Mungu hunisaidia.
Ni nani awezaye kusema nina hatia?
Maadui zangu wote watachakaa kama vazi,
nondo watawatafuna.
10Nani kati yenu amchaye Mwenyezi-Mungu?
Nani anayetii maneno ya mtumishi wake?
Kama yupo atembeaye gizani bila taa,
amtumainie Mwenyezi-Mungu,
na kumtegemea Mungu wake.
11Lakini nyinyi mnaowasha moto,
na kujifanyia silaha za mienge,
tembeeni kwa mwanga wa moto huo,
miali ya moto mliowasha nyinyi wenyewe.
Mtakachopata kutoka kwa Mwenyezi-Mungu ni hiki:
Nyinyi mtalala chini na mateso makali.


Isaya50;1-11

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: