Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 20 November 2019

Kikombe Cha Asubuhi;Isaya 59....



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante  Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu



Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni

Neema yako yatutosha  Mungu wetu..!




Mwenyezi-Mungu ndiye aliyeumba dunia kwa nguvu yake, aliyeuimarisha ulimwengu kwa hekima yake, na kwa maarifa yake akazitandaza mbingu. Anapotoa sauti yake maji hutitima mbinguni, hufanya ukungu upande kutoka mipaka ya dunia. Hufanya umeme umulike wakati wa mvua huvumisha upepo kutoka ghala zake.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,
tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako

Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa  Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

Kila mtu ni mpumbavu bila maarifa, kila mhunzi anaaibishwa na vinyago vyake; maana sanamu zake ni udanganyifu mtupu, wala hazina pumzi ndani yake. Hazina thamani, ni udanganyifu mtupu; wakati watakapoadhibiwa, nazo zitaangamia.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe



Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu  wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo 

Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...

Mungu aliye hazina ya Yakobo si kama hizo, maana yeye ndiye aliyeviumba vitu vyote, na Israeli ni kabila lililo mali yake; Mwenyezi-Mungu wa Majeshi, ndilo jina lake.
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba
 ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!


Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....

Nawapenda.

Nabii azilaani dhambi za watu
1Msifikiri mkono wa Mungu ni mfupi,
hata asiweze kuwaokoeni;
au masikio yake yamezibika,
hata asiweze kuwasikieni.
2Dhambi zenu ndizo zinazowatenga na Mungu wenu,
dhambi zenu zimemfanya ajifiche mbali nanyi
hata asiweze kuwasikieni.
3Maana mikono yenu imetiwa najisi kwa mauaji,
na vidole vyenu kwa matendo maovu.
Midomo yenu imesema uongo,
na ndimi zenu husema uovu.
4Hakuna atoaye madai yake kwa haki,
wala anayeshtaki kwa uaminifu.
Mnategemea hoja batili;
mnasema uongo.
Mnatunga hila na kuzaa uovu.
5Mnaangua mayai ya joka lenye sumu,
mnafuma utando wa buibui.
Anayekula mayai yenu hufa,
na yakipasuliwa nyoka hutokea.
6Utando wenu haufai kwa mavazi,
watu hawawezi kujifunikia mnachofuma.
Kazi zenu ni kazi za uovu,
matendo yenu yote ni ukatili mtupu.
7Mko mbioni kutenda maovu,
mnaharakisha kumwaga damu isiyo na hatia.
Mawazo yenu ni mawazo ya uovu,
popote mwendapo mnaacha ukiwa na uharibifu.
8Njia ya amani hamwijui kamwe;
njia zenu zote ni za dhuluma.
Mmejifanyia njia potovu,
yeyote anayepitia humo hapati amani.
Watu wanakiri dhambi yao
9Ndio maana haki iko mbali nasi,
maongozi ya uadilifu hayapo kwetu.
Tunatazamia kupata mwanga kumbe ni giza tupu,
twatazamia mwangaza, lakini twatembea gizani.
10Kama vipofu twapapasapapasa ukuta;
tunasitasita kama watu wasio na macho.
Tunajikwaa mchana kana kwamba ni usiku,
miongoni mwa wenye nguvu sisi ni kama wafu.
11Twanguruma kama dubu,
twaomboleza tena na tena kama hua.
Twatazamia hukumu ya haki, lakini haipo,
twatazamia wokovu, lakini uko mbali nasi.
12Makosa yetu mbele yako ni mengi mno,
dhambi zetu zashuhudia dhidi yetu.
Naam, makosa yetu tunaandamana nayo,
tunayajua maovu yetu.
13Tumekuasi na kukukana ee Mwenyezi-Mungu,
tumekataa kukufuata ewe Mungu wetu.
Udhalimu na uasi ndivyo tunavyopania,
mioyoni mwetu twatunga na kutoa maneno ya uongo.
14Haki imewekwa kando,
uadilifu uko mbali;
ukweli unakanyagwa mahakamani,
uaminifu haudiriki kuingia humo.
15Ukweli umekosekana,
naye anayeacha uovu hunyanyaswa.
Mungu ajiandaa kuwakomboa watu wake
Mungu aliona mambo hayo, akachukizwa,
alichukizwa kwamba hakuna haki.
16Aliona kwamba hakuna mtu aliyejali,
akashangaa kwamba hakuna aliyeingilia kati.
Basi akaamua kunyosha mkono wake mwenyewe,
uadilifu wake ukamhimiza.
17Alivaa uadilifu kama vazi la kujikinga kifuani,
na wokovu kama kofia ya chuma kichwani.
Atajivika kisasi kama vazi,
na kujifunika wivu kama joho.
18Atawaadhibu maadui kadiri ya matendo yao,
naam, ghadhabu yake na kisasi vitawapata maadui zake;
atawaadhibu hata wakazi wa nchi za mbali.
19Toka magharibi hadi mashariki,
kila mtu atamcha Mwenyezi-Mungu
na kutambua utukufu wake.
Maana atakuja kama mto uendao kasi,
mto unaosukumwa kwa upepo wa Mwenyezi-Mungu.
20Naye atakuja Siyoni kama Mkombozi,
Mkombozi wa wazawa wa Yakobo
ambao wataachana na makosa yao.
Asema Mwenyezi-Mungu.
21Mwenyezi-Mungu asema:
“Mimi nafanya nanyi agano hili:
Roho yangu niliyowajazeni,
maneno niliyoyaweka mdomoni mwenu,
hayataondoka kwenu kamwe,
wala kwa watoto na wajukuu zenu,
tangu sasa na hata milele.”


Isaya59;1-21

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: