Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday, 22 November 2019

Kikombe Cha Asubuhi;Isaya 61....


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante  Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu


Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni

Neema yako yatutosha  Mungu wetu..!


Tweka bendera ya vita duniani, piga tarumbeta kati ya mataifa; yatayarishe mataifa kupigana naye; ziite falme kuishambulia; falme za Ararati, Mini na Ashkenazi. Weka majemadari dhidi yake; walete farasi kama makundi ya nzige. Yatayarishe mataifa kupigana naye vita; watayarishe wafalme wa Medi, watawala na mawakili wao, tayarisheni nchi zote katika himaya yake.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,
tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako

Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa  Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

Nchi inatetemeka na kugaagaa kwa maumivu, maana nia ya Mwenyezi-Mungu kuhusu Babuloni ni thabiti: Ataifanya nchi ya Babuloni kuwa jangwa, ataifanya iwe bila watu. Askari wa Babuloni wameshindwa kupigana, wamebaki katika ngome zao; nguvu zao zimewaishia, wamekuwa kama wanawake. Nyumba za Babuloni zimechomwa moto, malango yake ya chuma yamevunjwa.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe



Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu  wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo 

Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...


Tarishi baada ya tarishi wanapiga mbio, mjumbe mmoja anamfuata mjumbe mwingine, kumpasha habari mfalme wa Babuloni kwamba mji wake umevamiwa kila upande. Vivuko vya mto vimetekwa, ngome zimechomwa moto, askari wamekumbwa na hofu. Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli asema hivi: “Babuloni ni kama uwanja wa kupuria nafaka wakati unapotayarishwa. Lakini bado kidogo tu, wakati wa mavuno utaufikia.”
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba
 ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!


Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....

Nawapenda.

Habari njema ya wokovu
1Bwana Mwenyezi-Mungu amenijaza roho yake,
maana Mwenyezi-Mungu ameniweka wakfu,61:1 ameniweka wakfu: Neno kwa neno Kiebrania: Amenipaka mafuta; Taz Orodha ya Maneno chini ya Paka mafuta.
akanituma niwaletee wanaokandamizwa habari njema,
niwatibu waliovunjika moyo,
niwatangazie mateka kwamba watapata uhuru,
na wafungwa kwamba watafunguliwa.
2Amenituma niutangaze mwaka wake wa neema,
na siku ya Mungu wetu ya kulipiza kisasi;
niwafariji wote wanaoomboleza;
3niwape wale wanaoomboleza katika Siyoni
taji la maua badala ya majivu,
mafuta ya furaha badala ya maombolezo,
vazi la sifa badala ya moyo mzito.
Nao wataitwa mialoni madhubuti,
aliyopanda Mwenyezi-Mungu kuonesha utukufu wake.
4Watayajenga upya magofu ya zamani,
wataisimika miji iliyoharibiwa hapo kwanza;
wataitengeneza miji iliyobomolewa,
uharibifu wa vizazi vingi vilivyopita.
5Wageni watakuwa hapo kuwachungia mifugo yenu;
watawalimia na kuwatunzia mizabibu yenu.
6Nanyi mtaitwa: “Makuhani wa Mwenyezi-Mungu”,
Mtaitwa: “Watumishi wake Mungu wetu”.
Mtafaidika kwa utajiri wa mataifa,
mtatukuka kwa mali zao.
7Kwa vile mlipata aibu maradufu,
watu wakaona kuwa fedheha ni majaliwa yenu,
sasa mtapata eneo maradufu kuwa mali yenu,
na furaha yenu itadumu milele.
8“Mimi Mwenyezi-Mungu napenda haki;
nachukia unyanganyi na uhalifu.
Nitawatuza watu wangu kwa uaminifu,
nitafanya nao agano la milele.
9Wazawa wao watakuwa maarufu kati ya mataifa;
watajulikana kuwa maarufu kati ya watu wengine.
Kila atakayewaona atakiri kwamba
wao ni watu aliowabariki Mwenyezi-Mungu.”
10Nitafurahi sana kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu,
nafsi yangu itashangilia kwa sababu ya Mungu wangu.
Maana amenivika vazi la wokovu,
amenivalisha vazi la uadilifu,
kama bwana arusi ajipambavyo kwa shada la maua,
kama bibi arusi ajipambavyo kwa johari zake.
11Hivyo, kama vile ardhi ioteshavyo mimea,
na shamba lichipushavyo mbegu zilizopandwa humo,
Mwenyezi-Mungu atasababisha uadilifu na sifa
kuchomoza mbele ya mataifa yote.


Isaya61;1-11

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: