|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Haleluyah ni siku/wiki Nyingine tena Mungu wetu ametuchagua na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Si kwamba sisi tumetenda mema sana wala si kwa nguvu zetu si kwa utashi wetu wala si kwa akili zetu si kwamba sisi ni wazuri mno si kwa uwezo wetu sisi kuwa hivi tulivyo leo hii Ni kwa rehema/neema zake ni kwa mapenzi yake Mungu wetu....
Tumshukuru Mungu wetu katika yote... Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari kwa majukumu yetu Sifa na Utukufu tunakurudshia Mungu wetu....!!
Mfalme Nebukadneza wa Babuloni aliuharibu na kuuponda mji wa Yerusalemu aliuacha kama chungu kitupu; aliumeza kama joka. Alijaza tumbo lake vitu vyake vizurivizuri, akautupilia mbali kama matapishi. Watu wa Yerusalemu na waseme: “Babuloni na ulipizwe ukatili uleule, tuliotendwa sisi pamoja na jamaa zetu! Babuloni ipatilizwe kwa umwagaji wa damu yetu.”
Tazama jana imepita ee Mungu wetu leo ni siku mpya na kesho ni siku nyingine Jehovah tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea Jehovah usitutie majaribu Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote Yahweh tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona
Kwakupigwa kwake sisi tumepata kupona....
Kwa hiyo asema hivi Mwenyezi-Mungu: “Nitawatetea kuhusu kisa chenu, na kulipiza kisasi kwa ajili yenu. Nitaikausha bahari ya Babuloni na kuvifanya visima vyake vikauke. Babuloni itakuwa rundo la magofu, itakuwa makao ya mbweha, itakuwa kinyaa na kitu cha kuzomewa; hakuna mtu atakayekaa huko.
Yahweh tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe
Baba wa Mbinguni tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote
za maisha yetu
Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu
Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu
Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...
Wababuloni watanguruma pamoja kama simba; watakoroma kama wanasimba. Wakiwa na uchu mkubwa nitawaandalia karamu: Nitawalewesha mpaka wapepesuke; nao watalala usingizi wa daima na hawataamka tena. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Mungu wetu tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu kila mmoja na mahitaji yake Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe Baba wa Mbinguni ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia zako wakasimamie Neno lako nalo likaweke huru Mungu wetu tunaomba ukasikie kuomba kwetu Mungu wetu ukawatendee sawasawa na mapenzi yako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele Amina...!!
Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea kama inavyompendeza yeye.... Nawapenda.
|
1Kwa ajili ya Siyoni sitakaa kimya,
kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia,
mpaka kuokolewa kwake kuchomoze kama umeme,
wokovu wake utokeze kama mwenge.
2Mataifa watauona wokovu wako,
wafalme wote watauona utukufu wako.
Nawe utaitwa kwa jina jipya,
jina atakalokupa Mwenyezi-Mungu mwenyewe.
3Utakuwa taji zuri mkononi mwa Mwenyezi-Mungu;
kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako.
4Hutaitwa tena: “Aliyeachwa”,
wala nchi yako haitaitwa: “Ukiwa”.
Bali utaitwa: “Namfurahia,”
na nchi yako itaitwa: “Aliyeolewa.”
Maana Mwenyezi-Mungu amependezwa nawe,
naye atakuwa kama mume wa nchi yako.
5Maana kama kijana mwanamume amwoavyo msichana,
ndivyo aliyekujenga62:5 aliyekujenga: Kiebrania: Wanao. atakavyokuwa mume wako.
Kama bwana arusi afurahivyo juu ya bibi arusi,
ndivyo Mungu atakavyofurahi juu yako.
6“Juu ya kuta zako ee Yerusalemu nimeweka walinzi,
usiku na mchana kamwe hawatakaa kimya.”
Enyi mnaomkumbusha Mwenyezi-Mungu ahadi yake,
msikae kimya;
7msimpe hata nafasi ya kupumzika,
mpaka atakapousimika mji wa Yerusalemu,
na kuufanya uwe fahari ulimwenguni kote.
8Mwenyezi-Mungu ameapa kwa mkono wake wa kulia,
naam, ameapa kwa mkono wake wenye nguvu akisema:
“Sitawapa tena maadui zako nafaka yako;
wala wageni hawatakunywa tena divai yako
ambayo umeitolea jasho.
9Bali nyinyi mliyoivuna nafaka hiyo,
mtaila na kunitukuza mimi Mwenyezi-Mungu.
Nyinyi mliochuma zabibu hizo,
mtakunywa divai yake katika nyua zangu takatifu.”
10Wakazi wa Yerusalemu, tokeni, tokeni nje ya mji,
watayarishieni njia watu wenu wanaorejea!
Jengeni! Jengeni barabara na kuondoa mawe yote!
Wekeni alama kwa ajili ya watu.
11 62:11 Taz Isa 40:10; Ufu 22:12 Mwenyezi-Mungu ametangaza duniani kote,
waambie watu wa Siyoni:
“Mkombozi wenu anakuja,
zawadi yake iko pamoja naye
na tuzo lake liko mbele yake.”
12Nyinyi mtaitwa: “Watu Watakatifu”,
“Watu waliokombolewa na Mwenyezi-Mungu.”
Na Yerusalemu utaitwa: “Mji aupendao Mungu”,
“Mji ambao Mungu hakuuacha.”
Isaya62;1-12
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.
No comments:
Post a Comment