|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu katika yote....
Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana Mungu wa walio hai,Mungu mwenye huruma,Mungu wa upendo Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...Asante kwa wema na fadhili zako kwetu Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!
Nitawashusha chini kama kondoo wa kuchinjwa, kama vile kondoo dume na beberu. Ajabu kutekwa kwa Babuloni; mji uliosifika duniani kote umechukuliwa! Babuloni umekuwa kinyaa kati ya mataifa!
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
Bahari imefurika juu ya Babuloni, Babuloni imefunikwa mawimbi yaliyochafuka. Miji yake imekuwa kinyaa, nchi ya ukavu na jangwa, nchi isiyokaliwa na mtu yeyote, wala kupitika na binadamu yeyote.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomna ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe...
Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Yahwe ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona,masikio ya kusikia sauti yako na kuitii.. Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako,tukasimamie Neno lako,amri na sheria zako siku zote za maisha yetu... Ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu,ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....
Nitamwadhibu mungu Beli huko Babuloni, nitamfanya akitoe alichokimeza. Mataifa hayatamiminika tena kumwendea. Ukuta wa Babuloni umebomoka. “Tokeni humo enyi watu wangu! Kila mtu na ayasalimishe maisha yake, kutoka hasira kali ya Mwenyezi-Mungu.
Tazama watoto wako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu kila mmoja na mahitaji yake Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipo kwenda kinyume nawe Yahweh tunaomba ukawape neema ya kuweza kujiombea,kufuata njia zako nazo zikawaweke huru... Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele... Amina...!!
Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,Baba wa Mbinguni aendelee kuwatendea sawasawa na mapenzi yake... Nawapenda. |
Mungu awaadhibu maadui za watu wake
1Ni nani huyu ajaye kutoka Edomu,
anayefika kutoka Bosra na mavazi ya madoa mekundu?
Ni nani huyo aliyevaa mavazi ya fahari,
anatembea kwa nguvu zake kubwa?
Ni mimi Mwenyezi-Mungu
ninayetangaza ushindi wangu;
nami ni mwenye nguvu ya kuokoa.
2Lakini mbona nguo yako ni nyekundu,
nyekundu kama ya mtu anayekamua zabibu?
3Naam, nimekamua zabibu peke yangu,
wala hakuna mtu aliyekuja kunisaidia.
Nimeyakanyaga mataifa kwa hasira yangu,
niliyapondaponda kwa ghadhabu yangu.
Nguo zangu zimejaa madoa ya damu yao,
imeyachafua kabisa mavazi yangu.
4Niliamua kuwa siku ya kulipiza kisasi imefika;
wakati wa kuwakomboa watu wangu umefika.
5Nilitazama na hapakuwa na wa kunisaidia;
nilishangaa hapakuwa na wa kuniunga mkono.
Lakini nilijipatia ushindi kwa mkono wangu,
ghadhabu yangu ilinihimiza.
6Kwa hasira yangu niliwaponda watu,
niliwalewesha kwa ghadhabu yangu;
damu yao niliimwaga chini ardhini.”
Wema wa Mungu kwa Israeli
7Nitasimulia fadhili za Mwenyezi-Mungu;
nitataja matendo yake yote yastahiliyo sifa,
kwa sababu ya yote aliyotutendea,
wema wake mkuu aliowapa Waisraeli kwa huruma yake,
kadiri ya wingi wa fadhili zake.
8Maana alisema juu yao:
“Hakika, hawa ni watu wangu;
watoto wangu ambao hawatanidanganya.”
Basi yeye akawa Mwokozi wao.
9Katika taabu zao zote,
hakumtuma mjumbe63:9 … hakumtuma mjumbe … au Malaika; Yeye aliwaokoa. Yeye Mwenyewe alitaabika walipotaabika, akamtuma malaika wake awaokoe. mwingine kuwasaidia,
ila yeye mwenyewe alikuja kuwaokoa.
kwa upendo na huruma yake aliwakomboa.
Aliwabeba na kuwachukua tangu zamani.
10Lakini wao walikuwa wakaidi,
wakaihuzunisha roho yake takatifu.
Basi, Mungu akageuka, akawa adui yao;
yeye mwenyewe akapigana nao.
11Ndipo walipokumbuka63:11 walipokumbuka: Kiebrania: Alipozikumbuka. siku za zamani,
wakati wa Mose mtumishi wa Mwenyezi-Mungu.
Wakauliza, “Yuko wapi sasa Mwenyezi-Mungu,
aliyewaokoa wachungaji wa kundi lake baharini?
Yuko wapi yule aliyeiweka roho yake takatifu kati yao,
12ambaye kwa mkono wake wenye nguvu
alifanya maajabu kwa njia ya Mose,
akapasua bahari na kuwaongoza watu wake,
na kujipatia jina la milele?
13Aliwaongoza katikati ya vilindi vya bahari,
wakapita humo kama farasi bila kujikwaa.
14Kama ng'ombe wapelekwavyo malishoni bondeni,
ndivyo roho ya Mungu ilivyowapumzisha watu wake.
Ndivyo ee Mungu ulivyowaongoza watu wako,
nawe ukajipatia jina tukufu.”
Sala ya kuomba msaada
15Ututazame kutoka mbinguni ee Mungu, uone,
utuangalie kutoka makao yako matakatifu na matukufu.
Iko wapi bidii yako kwa ajili yetu na nguvu yako?
Usiache kutuonesha upendo wako.63:15 Usiache … upendo wako: Tafsiri ya neno kwa neno: Upendo na huruma yako vimezuiwa visionekane kwetu.
16Maana wewe ndiwe Baba yetu;
Abrahamu, mzee wetu, hatujali,
naye Israeli hatutambui;
lakini wewe, ee Mwenyezi-Mungu, ni Baba yetu.
Wewe umeitwa tangu kale: “Mkombozi wetu.”
17Ee Mwenyezi-Mungu, mbona unatukosesha njia zako?
Mbona unatufanya kuwa wakaidi hata tusikuogope?
Rudi ee Mungu kwa ajili ya watumishi wako,
makabila ambayo daima yalikuwa mali yako.
18Kwa kitambo tu sisi watakatifu wako tulimiliki nchi,
lakini maadui zetu wakaja wakaharibu maskani yako.63:18 aya 18 makala ya Kiebrania si dhahiri.
19Tumekuwa kama watu ambao hujawatawala kamwe,
kama watu ambao hawakujulikana kwa jina lako.
Isaya63;1-19
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.
No comments:
Post a Comment