Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday, 10 January 2020

Kikombe Cha Asubuhi; Yeremia 30....


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu katika yote....

Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi
Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana
Mungu wa walio hai,Mungu  mwenye huruma,Mungu wa upendo
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...
Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu

Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!


Kisha, Mafarisayo wakaenda zao, wakashauriana jinsi ya kumnasa Yesu kwa maneno yake. Basi, wakawatuma wafuasi wao pamoja na wafuasi wa kikundi cha Herode. Wakamwuliza, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwaminifu, na kwamba wafundisha njia ya Mungu kwa uaminifu; humwogopi mtu yeyote, maana cheo cha mtu si kitu kwako.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,
tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako

Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote 
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema
ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe
na yule mwovu na kazi zake zote
Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu
ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....


Haya, tuambie maoni yako. Je, ni halali au la, kulipa kodi kwa Kaisari?” Lakini Yesu alitambua uovu wao, akawaambia, “Enyi wanafiki mbona mnanijaribu? Nionesheni fedha ya kulipia kodi.” Nao wakamtolea sarafu ya fedha.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomna ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe...


Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Yahwe ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona,masikio ya kusikia sauti yako na kuitii..
Baba wa Mbinguni  tunaomba ukatupe neema ya kufuata
njia zako,tukasimamie Neno lako,amri na sheria zako
siku zote za maisha yetu...
Ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu,ukatufanye chombo chema
ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....


Basi, Yesu akawauliza, “Sura na chapa hii ni ya nani?” Wakamjibu, “Ni ya Kaisari.” Hapo Yesu akawaambia, “Basi, ya Kaisari mpeni Kaisari, na ya Mungu mpeni Mungu.” Waliposikia hivyo wakashangaa; wakamwacha, wakaenda zao.
Tazama watoto wako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
kila mmoja na mahitaji yake
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipo kwenda kinyume nawe
Yahweh tunaomba ukawape neema ya kuweza kujiombea,kufuata njia zako nazo zikawaweke huru...
Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele...
Amina...!!


Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,Baba wa Mbinguni aendelee kuwatendea sawasawa na mapenzi yake...
Nawapenda.


Ahadi za Mungu kwa watu wote
1Neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Mwenyezi-Mungu: 2“Mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nasema hivi: Yaandike katika kitabu maneno yote niliyokuambia. 3Maana siku zaja ambapo nitawarudishia fanaka zao watu wangu wa Israeli na Yuda na kuwarudisha katika nchi niliyowapa wazee wao, nao wataimiliki. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
4Haya ndiyo mambo aliyosema Mwenyezi-Mungu kuhusu watu wa Israeli na Yuda:
5“Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi:
Kumesikika kilio cha hofu
sauti ya kutisha wala si ya amani.
6Jiulizeni sasa na kufahamu:
Je, mwanamume aweza kujifungua mtoto?
Mbona basi, namwona kila mwanamume
amejishika kiunoni kama mwanamke mwenye utungu
na nyuso zao zimegeuka rangi?
7Kweli, siku hiyo ni kubwa,
hakuna nyingine kama hiyo;
ni siku ya huzuni kwa watu wa Yakobo;
hata hivyo, wataokolewa humo.
8“Siku hiyo itakapofika, nasema mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, nitaivunja nira iliyo shingoni mwao na kukata minyororo yao. 9Nao hawatakuwa tena watumwa wa wageni, bali watanitumikia mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, na mfalme wa ukoo wa Daudi ambaye nitawateulia.
10“Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi:
Usiogope ee Yakobo mtumishi wangu,
wala usifadhaike, ee Israeli;
maana nitakuokoa huko mbali uliko,
na wazawa wako kutoka uhamishoni.
Utarudi na kuishi kwa amani,
wala hakuna mtu atakayekuogopesha.
11Maana mimi niko pamoja nawe, kukuokoa.
Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Nitayaangamiza kabisa mataifa yote,
ambayo nilikutawanya kati yao;
lakini wewe sitakuangamiza kabisa.
Nitakuadhibu kadiri unavyostahili
wala sitakuacha uende bila kukuadhibu.
Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
12“Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi:
Majeraha yako hayaponyeki,
vidonda vyako havitibiki.
13Hakuna atakayeshughulikia kisa chako,
jeraha lako halina dawa,
wewe hutaponyeshwa.
14Wapenzi wako wote wamekusahau;
hawajali chochote juu yako,
nimekupiga pigo la adui;
umeadhibiwa bila huruma,
kwa kuwa kosa lako ni kubwa,
dhambi zako ni nyingi mno.
15Mbona unalia juu ya jeraha lako?
Maumivu yako hayaponyeki.
Nimekutendea hayo yote,
kwa sababu kosa lako ni kubwa,
dhambi zako ni nyingi mno.
16Lakini wote wanaokuangamiza, wataangamizwa,
na maadui zako wote watachukuliwa uhamishoni;
wanaokuteka nyara, watatekwa nyara,
wanaokuwinda nitawawinda.
17“Nitakurudishia afya yako,
na madonda yako nitayaponya,
japo wamekuita ‘Aliyetupwa’,
‘Mji Siyoni usio na wa kuutunza!’”
18Mwenyezi-Mungu asema hivi:
“Nitazirudisha tena fanaka za maskani ya Yakobo,
na kuyaonea huruma makao yake;
mji utajengwa upya juu ya magofu yake,
na ikulu ya mfalme itasimama pale ilipokuwa.
19Humo zitatoka nyimbo za shukrani
na sauti za wale wanaosherehekea.
Nitawaongeza na wala hawatakuwa wachache;
nitawafanya waheshimiwe wala hawatadharauliwa.
20Watoto wao watakuwa kama walivyokuwa zamani,
jumuiya yao itaimarika mbele yangu,
nami nitawaadhibu wote wanaowakandamiza.
21Kiongozi wao atakuwa mmoja wao,
mtawala wao atatokea miongoni mwao.
Nitamleta karibu naye atanikaribia;
maana, nani anayethubutu kunikaribia kwa nguvu zake?
Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
22Nanyi mtakuwa watu wangu,
nami nitakuwa Mungu wenu.”
23Tazama, dhoruba kali kutoka kwa Mwenyezi-Mungu!
Ghadhabu imezuka,
kimbunga cha tufani
kitamlipukia mtu mwovu kichwani.
24Hasira ya Mwenyezi-Mungu haitarudi nyuma,
mpaka atakapotekeleza na kukamilisha
matakwa ya moyo wake.
Siku zijazo mtayaelewa vema mambo hayo.


Yeremia30;1-24

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: