|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu wetu katika yote...
Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetuAsante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu
Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni Neema yako yatutosha Mungu wetu..!
Basi, Yesu akawauliza, “Je, nyinyi hamwelewi mfano huu? Mtawezaje basi, kuelewa mfano wowote? Mpanzi hupanda neno la Mungu. Watu wengine ni kama walio njiani ambapo neno lilipandwa. Lakini mara tu baada ya kulisikia, Shetani huja na kuliondoa neno hilo lililopandwa ndani yao.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza, tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti, Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
Watu wengine ni kama zile mbegu zilizopandwa penye mawe. Mara tu walisikiapo hilo neno hulipokea kwa furaha. Lakini haliwaingii na kuwa na mizizi ndani yao; huendelea kulizingatia kwa kitambo tu, na wakati taabu au udhalimu vinapotokea kwa sababu ya hilo neno, mara wanakata tamaa. Watu wengine ni kama zile mbegu zilizoanguka penye miti ya miiba. Huo ni mfano wa wale wanaosikia hilo neno,
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe
Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama inavyokupendeza wewe Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...
lakini wasiwasi wa ulimwengu huu, anasa za mali na tamaa za kila namna huwaingia na kulisonga hilo neno, nao hawazai matunda. Lakini wengine ni kama zile mbegu zilizopandwa katika udongo mzuri. Hawa hulisikia hilo neno, wakalipokea, wakazaa matunda: Wengine thelathini, wengine sitini na wengine mia.”
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao Nuru yako ikaangaze katika maisha yao Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele Amina....!!!
Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana kwakuwanami/kunisoma Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea kama inavyompendeza yeye Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba ukae nanyi daima.... Nawapenda. |
Kuomba huruma
1Ukumbuke ee Mwenyezi-Mungu, mambo yaliyotupata!
Utuangalie, uone jinsi tulivyoaibishwa!
2Nchi yetu imekabidhiwa wageni,
nyumba zetu watu wengine.
3Tumekuwa yatima, bila baba,
mama zetu wameachwa kama wajane.
4Maji yetu tunayapata kwa fedha,
kuni zetu kwa kuzinunua.
5Tunalazimishwa kufanya kazi kama punda,
tumechoka lakini haturuhusiwi kupumzika.
6Wamisri na Waashuru tumewanyoshea mikono,
ili tupate chakula cha kutosha.
7Wazee wetu walitenda dhambi na hawapo tena;
nasi tunateseka kwa sababu ya makosa yao.
8Watumwa ndio wanaotutawala,
wala hakuna wa kutuokoa mikononi mwao.
9Chakula chetu twapata kwa kuhatarisha maisha yetu,
maana wauaji wanazurura huko mashambani.
10Ngozi zetu zawaka moto kama tanuri
kwa sababu ya njaa inayotuchoma.
11Wanawake wetu wanashikwa kwa nguvu mjini Siyoni,
binti zetu katika vijiji vya Yuda.
12Wakuu wetu wametungikwa kwa mikono yao;
wazee wetu hawapewi heshima yoyote.
13Vijana wanalazimishwa kusaga nafaka kwa mawe,
wavulana wanayumbayumba kwa mizigo ya kuni.
14Wazee wameacha kutoa mashauri yao,
vijana wameacha kuimba.
15Furaha ya mioyo yetu imetoweka,
ngoma zetu zimegeuzwa kuwa ombolezo.
16Fahari tuliyojivunia imetokomea.
Ole wetu kwa kuwa tumetenda dhambi!
17Kwa ajili hiyo tumeugua moyoni,
kwa mambo hayo macho yetu yamefifia.
18Maana mlima Siyoni umeachwa tupu,
mbweha wanazurura humo.
19Lakini wewe Mwenyezi-Mungu watawala milele,
utawala wako wadumu vizazi vyote.
20Mbona umetuacha muda mrefu hivyo?
Mbona umetutupa siku nyingi hivyo?
21Uturekebishe ee Mwenyezi-Mungu, nasi tukurudie,
uturudishie fahari yetu kama zamani.
22Au, je, umetukataa kabisa?
Je, umetukasirikia mno?
Maombolezo5;1-22
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.
No comments:
Post a Comment