Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 3 March 2020

Kikombe Cha Asubuhi; Ezekieli 10...


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante  Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu


Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni

Neema yako yatutosha  Mungu wetu..!

Yeye, kwa asili alikuwa daima Mungu; lakini hakufikiri kwamba kule kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kungangania kwa nguvu. Bali, kwa hiari yake mwenyewe, aliachilia hayo yote, akajitwalia hali ya mtumishi, akawa sawa na wanadamu, akaonekana kama wanadamu.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,
tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako

Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa  Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....



Alijinyenyekesha na kutii mpaka kufa, hata kufa msalabani. Kwa sababu hiyo Mungu alimkweza juu kabisa, akampa jina lililo kuu kuliko majina yote.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe



Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu  wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo 

Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...

Ili kwa heshima ya jina la Yesu, viumbe vyote mbinguni, duniani na kuzimu, vipige magoti mbele yake, na kila mtu akiri kwamba Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba
 ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!


Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....

Nawapenda.


Utukufu wa Mwenyezi-Mungu unaondoka hekaluni
1 Kisha nikaona kwamba katika lile anga juu ya vichwa vya viumbe wenye mabawa kulikuwa na kitu kinachofanana na johari ya rangi ya samawati, umbo lake kama kiti cha enzi. 210:2 Taz Ufu 8:5 Mungu akamwambia yule mtu aliyevaa mavazi ya kitani, “Nenda katikati ya magurudumu yaliyo chini ya viumbe wenye mabawa, ukaijaze mikono yako makaa ya moto ulioko katikati yao na kuyatawanya juu ya mji.” Nikamwona akienda.
3Wale viumbe wenye mabawa walikuwa wamesimama upande wa kusini wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu yule mtu alipoingia ndani; wingu likaujaza ua wa ndani. 4Utukufu wa Mwenyezi-Mungu ukapaa juu kutoka kwa wale viumbe wenye mabawa ukaenda kwenye kizingiti cha nyumba hiyo, na lile wingu likaijaza nyumba, na ua ukajaa mngao wa utukufu wa Mwenyezi-Mungu. 5Mlio wa viumbe wenye mabawa uliweza kusikika hata kwenye ua wa nje, kama sauti ya Mwenyezi-Mungu wa majeshi anapoongea.
6Mwenyezi-Mungu alipomwamuru yule mtu aliyevaa mavazi ya kitani achukue moto toka katikati ya magurudumu yaliyokuwa chini ya viumbe wenye mabawa, yule mtu alikwenda na kusimama pembeni mwa gurudumu mojawapo. 7Kiumbe mmoja akanyosha mkono wake kuchukua moto uliokuwa katikati ya viumbe wenye mabawa, akatwaa sehemu yake na kuutia mikononi mwa yule mtu aliyevaa mavazi ya kitani; naye alipoupokea, akaenda zake. 8Viumbe wenye mabawa hao walionekana kuwa kitu kama mkono wa binadamu chini ya mabawa yao.
9 10:9-13 Taz Eze 1:15-21 Niliangalia, nikaona kulikuwa na magurudumu manne, gurudumu moja pembeni mwa kila kiumbe chenye mabawa. Magurudumu hayo yalimetameta kama jiwe la zabarajadi. 10Yote manne yalionekana kuwa ya namna moja, na kila gurudumu lilionekana kama liko ndani ya gurudumu lingine. 11Yaliweza kwenda pande zote bila kugeuka; kule lilikoelekea gurudumu la kwanza yote yalifuata. 1210:12 Taz Ufu 4:8 Miili ya hao viumbe, migongo yao, mikono na mabawa yao, pamoja na magurudumu, vyote vilijaa macho pande zote. 13Niliambiwa kuwa magurudumu yale yanaitwa, “Magurudumu Yanayozunguka.”
14 10:14 Taz Eze 1:10; Ufu 4:7 Kila kiumbe mwenye mabawa alikuwa na nyuso nne: Uso wa kwanza ulikuwa wa fahali, uso wa pili ulikuwa wa mwanadamu, uso wa tatu ulikuwa wa simba na uso wa nne ulikuwa wa tai. 15Viumbe wenye mabawa wakainuka juu. Hawa ndio wale viumbe hai niliowaona karibu na mto Kebari. 16Viumbe hao walipokwenda, magurudumu nayo yalikwenda kando yao. Viumbe walipokunjua mabawa yao ili kupaa juu, magurudumu nayo yalikwenda pamoja nao. 17Waliposimama, magurudumu nayo yalisimama; hao walipopaa juu, magurudumu nayo yalipaa pamoja nao. Roho ya hao viumbe ilikuwa pia katika magurudumu hayo.
18Kisha utukufu wa Mwenyezi-Mungu ulitoka kwenye kizingiti cha nyumba, ukaenda na kusimama juu ya wale viumbe. 19Viumbe wakakunjua mabawa yao, wakapaa juu, mimi nikiwa nawaona na yale magurudumu yalikuwa kando yao. Wakasimama mbele ya lango la mashariki la nyumba ya Mwenyezi-Mungu, na utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwa juu yao.
20Hawa walikuwa wale viumbe hai niliowaona chini ya Mungu wa Israeli karibu na mto Kebari, nami nikatambua kuwa ni viumbe wenye mabawa. 21Kila mmoja wao alikuwa na nyuso nne na mabawa manne; na chini ya kila bawa kulikuwa na kitu kama mkono wa binadamu. 22Vilevile nilizitambua nyuso zao: Zilikuwa zilezile nilizokuwa nimeziona kule kwenye mto Kebari. Kila kiumbe alikwenda mbele, moja kwa moja.

Ezekieli10;1-22

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: