|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu katika yote....
Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana Mungu wa walio hai,Mungu mwenye huruma,Mungu wa upendo Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...Asante kwa wema na fadhili zako kwetu Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!
kwa ujumbe wa kweli na kwa nguvu ya Mungu. Uadilifu ndiyo silaha yetu kila upande. Tuko tayari kupata heshima na kudharauliwa, kulaumiwa na kusifiwa. Twadhaniwa kuwa waongo, kumbe twasema kweli;
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako, Tukijinyenyekeza,tukijiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunamomba utusamehe dhambi zetu Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
kama wasiojulikana, kumbe twajulikana kwa wote; kama waliokufa, lakini mwonavyo, sisi ni hai kabisa. Ingawa tumeadhibiwa, hatukuuawa; ingawa tunayo huzuni, twafurahi daima; ingawa tu maskini, twatajirisha watu wengi; twaonekana kuwa watu tusio na chochote, kumbe tuna kila kitu.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomna ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe...
Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Yahwe ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona,masikio ya kusikia sauti yako na kuitii.. Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako,tukasimamie Neno lako,amri na sheria zako siku zote za maisha yetu... Ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu,ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....
Ndugu Wakorintho, tumezungumza nanyi kwa unyofu; mioyo yetu iko wazi kabisa. Kama mnaona kuna kizuizi chochote kile, kizuizi hicho kiko kwenu nyinyi wenyewe, na si kwa upande wetu. Sasa nasema nanyi kama watoto wangu: Wekeni mioyo yenu wazi kama nasi tulivyofanya.
Tazama watoto wako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu kila mmoja na mahitaji yake Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipo kwenda kinyume nawe Yahweh tunaomba ukawape neema ya kuweza kujiombea,kufuata njia zako nazo zikawaweke huru... Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele... Amina...!!
Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,Baba wa Mbinguni aendelee kuwatendea sawasawa na mapenzi yake... Nawapenda. |
Kuharibiwa kwa vitu vya ibada vya Israeli
1Waisraeli walikuwa kama mzabibu mzuri,
mzabibu wenye kuzaa matunda.
Kadiri matunda yalivyozidi kuongezeka,
ndivyo walivyozidi kujijengea madhabahu.
Kadiri nchi yao ilivyozidi kustawi,
ndivyo walivyozidi kupamba nguzo zao za ibada.
2Mioyo yao imejaa udanganyifu.
Sasa ni lazima wawajibike kwa hatia yao.
Mwenyezi-Mungu atazibomoa madhabahu zao
na kuziharibu nguzo zao.
3Wakati huo watasema:
“Hatuna tena mfalme,
kwa kuwa hatumchi Mwenyezi-Mungu;
lakini, naye mfalme atatufanyia nini?”
4Wanachosema ni maneno matupu;
wanaapa na kufanya mikataba ya bure;
haki imekuwa si haki tena,
inachipua kama magugu ya sumu shambani.
5Wakazi wa Samaria watatetemeka
kwa sababu ya ndama wa huko Betheli.
Watu wake watamwombolezea ndama huyo,
hata makuhani wanaomwabudu watamlilia;
kwani fahari ya ndama huyo imeondolewa.
6Kinyago hicho kitapelekwa Ashuru,
kama ushuru kwa mfalme mkuu.
Watu wa Efraimu wataaibishwa,
Waisraeli watakionea aibu kinyago chao.
7Mfalme wa Samaria atachukuliwa,
kama kipande cha mti juu ya maji.
8Mahali pa kuabudia vilimani pa Aweni,
dhambi ya Waisraeli, pataharibiwa.
Miiba na magugu vitamea katika madhabahu zao.
Nao wataiambia milima, “Tufunikeni”
na vilima, “Tuangukieni!”
Israeli atavuna alichopanda
9Enyi Waisraeli,
nyinyi mmetenda dhambi tangu kule Gibea,
na bado mnaendelea.
Hakika vita vitawaangamiza hukohuko Gibea.
10Nitawajia watu hawa wapotovu na kuwaadhibu;
watu wa mataifa watakusanyika kuwashambulia,
watakapoadhibiwa kwa ajili ya dhambi zao nyingi.
11Efraimu ni ndama aliyefundishwa vizuri,
akapenda kupura nafaka.
Lakini sasa shingo yake nzuri nitaifunga nira.
Yuda atalima kwa jembe yeye mwenyewe,
naam, Yakobo atakokota jembe la kupalilia.
12Pandeni wema kwa faida yenu,
nanyi mtavuna upendo;
limeni mashamba yaliyoachwa,
maana wakati wa kunitafuta mimi Bwana umefika
nami nitawanyeshea baraka.
13Lakini nyinyi mmepanda uovu,
nyinyi mmevuna dhuluma;
mmekula matunda ya uongo wenu.
Wewe Israeli ulitegemea nguvu zako mwenyewe,
na wingi wa askari wako.
14Kwa hiyo msukosuko wa vita utawajia watu wako;
ngome zako zote zitaharibiwa,
kama Shalmani alivyoharibu Beth-arbeli vitani,
kina mama wakapondwa pamoja na watoto wao.
15Ndivyo itakavyokuwa kwenu enyi watu wa Betheli,
kwa sababu ya uovu wenu mkuu.
Kutakapopambazuka mfalme wa Israeli atawatokomeza.
Hosea10;1-15
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe
No comments:
Post a Comment