|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu wetu katika yote...
Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetuAsante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu
Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni Neema yako yatutosha Mungu wetu..!
Msiambatane na watu wasioamini. Je, wema na uovu vyapatana kweli? Mwanga na giza vyawezaje kukaa pamoja? Kristo anawezaje kupatana na Shetani? Mwaamini ana uhusiano gani na asiyeamini?
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza, tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti, Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
Hekalu la Mungu lina uhusiano gani na sanamu za uongo? Maana sisi ni hekalu la Mungu aliye hai. Kama Mungu mwenyewe alivyosema: “Nitafanya makao yangu kwao, na kuishi kati yao. Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.”
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe
Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama inavyokupendeza wewe Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...
Kwa hiyo Bwana asema pia: “Ondokeni kati yao, mkajitenge nao; msiguse kitu najisi, nami nitawapokea. Mimi nitakuwa Baba yenu, nanyi mtakuwa wanangu, waume kwa wake, asema Bwana Mwenye Nguvu.”
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao Nuru yako ikaangaze katika maisha yao Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele Amina....!!!
Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana kwakuwanami/kunisoma Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea kama inavyompendeza yeye Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba ukae nanyi daima.... Nawapenda. |
Upendo wa Mungu wapita hasira yake
1“Israeli alipokuwa mtoto, nilimpenda,
Kutoka Misri nilimwita mwanangu.
2Lakini kadiri nilivyozidi kuwaita,
ndivyo walivyozidi kwenda mbali nami;
waliendelea kuyatambikia Mabaali,
na kuvifukizia ubani vinyago vya miungu.
3Mimi ndiye niliyemfundisha Efraimu kutembea!
Mimi mwenyewe niliwachukua mikononi mwangu;
lakini hawakutambua kuwa mimi ndiye niliyewatunza.
4Niliwaongoza kwa kamba za huruma
naam, kwa kamba za upendo;
kama baba amwinuaye mtoto mpaka shavuni mwake,
ndivyo nami nilivyokuwa kwao.
Mimi niliinama chini na kuwalisha.
5Basi, watarudi nchini Misri;
watatawaliwa na mfalme wa Ashuru,
kwa sababu wamekataa kunirudia.
6“Upanga utavuma katika miji yao,
utavunjavunja miimo ya malango yake
na kuwaangamiza katika ngome zao.
7Watu wangu wamepania kuniacha mimi,
wakiitwa waje juu,
hakuna hata mmoja anayeweza.11:7 maana ya mistari hii miwili katika Kiebrania si dhahiri.
8Ewe Efraimu, nawezaje kukuacha?
Nawezaje kukutupa ewe Israeli?
Nitawezaje kukufanya kama mji wa Adma?
Nitawezaje kukutenda kama Seboimu!
Nazuiwa na moyo wangu;
huruma yangu imezidi kuwa motomoto.
9Nitaizuia hasira yangu kali;
sitamwangamiza tena Efraimu,
maana mimi ni Mungu, wala si binadamu.
“Mimi ndimi Mtakatifu miongoni mwenu,
nami sitakuja kuwaangamiza.
10“Watanifuata mimi Mwenyezi-Mungu ningurumaye kama simba;
nitakaponguruma watanijia toka magharibi wakitetemeka.
11Watakuja kutoka Misri wakitetemeka kama ndege,
wataruka kutoka Ashuru kama hua
nami nitawarudisha makwao;
mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
12Watu wa Efraimu wananirundikia uongo,
na Waisraeli udanganyifu.
Watu wa Yuda, wananiasi mimi Mungu Mtakatifu.
Hosea11;1-12
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe
No comments:
Post a Comment