|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu katika yote....
Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana Mungu wa walio hai,Mungu mwenye huruma,Mungu wa upendo Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...Asante kwa wema na fadhili zako kwetu Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!
Mwenyezi-Mungu asema: “Piga kelele, wala usijizuie; paza sauti yako kama tarumbeta. Watangazie watu wangu makosa yao, waambie wazawa wa Yakobo dhambi zao. Siku hata siku wananijia kuniabudu, wanatamani kujua mwongozo wangu, kana kwamba wao ni taifa litendalo haki, taifa lisilosahau sheria za Mungu wao. Wananitaka niamue kwa haki, na kutamani kukaa karibu na Mungu.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako, Tukijinyenyekeza,tukijiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunamomba utusamehe dhambi zetu Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
“Nyinyi mnaniuliza: ‘Mbona tunafunga lakini wewe huoni? Mbona tunajinyenyekesha, lakini wewe hujali?’ “Ukweli ni kwamba wakati mnapofunga, mnatafuta tu furaha yenu wenyewe, na kuwakandamiza wafanyakazi wenu!
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomna ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe...
Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Yahwe ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona,masikio ya kusikia sauti yako na kuitii.. Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako,tukasimamie Neno lako,amri na sheria zako siku zote za maisha yetu... Ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu,ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....
Mnafunga, na kugombana na kupigana ngumi. Mkifunga namna hiyo maombi yenu hayatafika kwangu juu. Mfungapo, nyinyi mnajitaabisha; mnaviinamisha vichwa vyenu kama unyasi, na kulalia nguo za magunia na majivu. Je, huo ndio mnaouita mfungo? Je, hiyo ni siku inayokubaliwa nami?
Tazama watoto wako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu kila mmoja na mahitaji yake Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipo kwenda kinyume nawe Yahweh tunaomba ukawape neema ya kuweza kujiombea,kufuata njia zako nazo zikawaweke huru... Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele... Amina...!!
Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,Baba wa Mbinguni aendelee kuwatendea sawasawa na mapenzi yake... Nawapenda. |
1Watu wa Efraimu wananirundikia uongo,
na Waisraeli udanganyifu.
Watu wa Yuda, wananiasi mimi Mungu Mtakatifu.
2“Watu wa Efraimu wanachunga upepo
kutwa nzima wanafukuza upepo wa mashariki.
Wanazidisha uongo na ukatili,
wanafanya mkataba na Ashuru
na kupeleka mafuta Misri.”
3Mwenyezi-Mungu ana mashtaka dhidi ya Yuda;
atawaadhibu wazawa wa Yakobo kadiri ya makosa yao,
na kuwalipa kadiri ya matendo yao.
4Yakobo akiwa bado tumboni mwa mama yake,
alimshika kisigino kaka yake.
Na alipokuwa mtu mzima
alishindana na Mungu.
5Alipambana na malaika, akamshinda;
alilia machozi na kuomba ahurumiwe.
Huko Betheli, alikutana na Mungu,
huko Mungu aliongea naye.
6Mwenyezi-Mungu, wa majeshi,
Mwenyezi-Mungu, ndilo jina lake.
Lakini nyinyi mrudieni Mungu wenu.
Zingatieni upendo na haki,
mtumainieni Mungu wenu daima.
7“Efraimu ni sawa na mfanyabiashara
atumiaye mizani danganyifu,
apendaye kudhulumu watu.
8Efraimu amesema,
‘Mimi ni tajiri!
Mimi nimejitajirisha!
Hamna ubaya kupata faida.
Hata hivyo, hilo si kosa!’”
9Mwenyezi-Mungu asema, “Mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mungu wako;
mimi ndimi niliyekutoa nchini Misri!
Mimi nitakukalisha tena katika mahema,
kama ufanyavyo sasa kwa siku chache tu,
wakati wa sikukuu ya vibanda.
10Mimi niliongea na manabii;
ni mimi niliyewapa maono mengi,
na kwa njia yao natangaza mpango wangu.
11Huko Gileadi ni mahali pa dhambi;
huko Gilgali walitambika fahali,
kwa hiyo madhabahu zao zitakuwa marundo ya mawe kwenye mitaro shambani.”
12Yakobo alikimbia nchi ya Aramu
akiwa huko alifanya kazi apate mke,
akachunga kondoo ili apate mke.
13Kwa nabii Mwenyezi-Mungu aliwatoa Waisraeli nchini Misri,
na kwa nabii Mungu aliwahifadhi.
14Waefraimu wamemchukiza Mwenyezi-Mungu sana.
Lakini Mwenyezi-Mungu atawalipiza makosa yao,
atawaadhibu kwa mambo maovu waliyotenda.
Hosea12;1-14
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe
No comments:
Post a Comment