|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Haleluyah ni siku/wiki nyingine tena Mungu wetu ametuchagua na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Si kwamba sisi tumetenda mema sana wala si kwa nguvu zetu si kwa utashi wetu wala si kwa akili zetu si kwamba sisi ni wazuri mno si kwa uwezo wetu sisi kuwa hivi tulivyo leo hii Ni kwa rehema/neema zake ni kwa mapenzi yake Mungu wetu....
Tumshukuru Mungu wetu katika yote...
Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari kwa majukumu yetu Sifa na Utukufu tunakurudshia Mungu wetu....!!
“Tangu zamani wewe ulivunja nira yako, ukaikatilia mbali minyororo yako, ukasema, ‘Sitakutumikia’. Juu ya kila kilima kirefu na chini ya kila mti wa majani mabichi, uliinamia miungu ya rutuba kama kahaba. Lakini mimi nilikupanda kama mzabibu mteule, mzabibu wenye afya na wa mbegu safi; mbona basi umeharibika, ukageuka kuwa mzabibu mwitu?
Tazama jana imepita ee Mungu wetu leo ni siku mpya na kesho ni siku nyingine Jehovah tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea Jehovah usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote Yahweh tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona
Kwakupigwa kwake sisi tumepata kupona....
Hata ukijiosha kwa magadi, na kutumia sabuni nyingi, madoa ya uovu wako bado yatabaki mbele yangu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. “Unawezaje kusema, ‘Mimi si najisi; sijawafuata Mabaali?’ Tazama ulivyotenda dhambi kule bondeni; angalia ulivyofanya huko! Wewe ni kama mtamba wa ngamia, akimbiaye huko na huko;
Yahweh tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe
Baba wa Mbinguni tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote
za maisha yetu
Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu
Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu
Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...
kama pundamwitu aliyezoea jangwani. Katika tamaa yake hunusanusa upepo; nani awezaye kuizuia hamu yake? Amtakaye hana haja ya kujisumbua; wakati wake ufikapo watampata tu. Israeli, usiichakaze miguu yako wala usilikaushe koo lako. Lakini wewe wasema: ‘Hakuna tumaini lolote. Nimeipenda miungu ya kigeni, hiyo ndiyo nitakayoifuata.’
Mungu wetu tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu kila mmoja na mahitaji yake Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe Baba wa Mbinguni ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia zako wakasimamie Neno lako nalo likawaweke huru Mungu wetu tunaomba ukasikie kuomba kwetu Mungu wetu ukawatendee sawasawa na mapenzi yako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele Amina...!!
Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea kama inavyompendeza yeye.... Nawapenda.
|
Moabu
1Mwenyezi-Mungu asema hivi:
“Watu wa Moabu wametenda dhambi tena na tena,
kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu.
Wamemkosea heshima marehemu mfalme wa Edomu
kwa kuichoma moto mifupa yake
ili kujitengenezea chokaa!
2Basi, nitaishushia moto nchi ya Moabu,
na kuziteketeza kabisa ngome za mji wa Keriothi.
Wanajeshi watakapopaza sauti zao na kupiga tarumbeta,
watu wa Moabu watakufa katika makelele hayo ya vita.
3Isitoshe, nitamuua mtawala wa Moabu,
pamoja na viongozi wote wa nchi hiyo.
Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Yuda
4Mwenyezi-Mungu asema hivi:
“Watu wa Yuda wametenda dhambi tena na tena,
kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu.
Wamepuuza sheria zangu,
wala hawakufuata amri zangu.
Wamepotoshwa na miungu ileile waliyoihudumia wazee wao.
5Basi, nitaishushia moto nchi ya Yuda,
na kuziteketeza kabisa ngome za Yerusalemu.”
Hukumu ya Mungu juu ya Israeli
6Mwenyezi-Mungu asema hivi:
“Waisraeli wametenda dhambi tena na tena,
kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu.
Wamewauza watu waaminifu
kwa kuwa hawakuweza kulipa madeni yao;
na kuwauza watu fukara
wasioweza kulipa deni la kandambili.
7Huwanyanyasa na kuwakandamiza wanyonge,
na maskini huwabagua wasipate haki zao.
Mtu na baba yake hulala na mjakazi yuleyule,
hivyo hulitia unajisi jina langu takatifu.
8Popote penye madhabahu,
watu hulalia nguo walizotwaa kwa maskini
kama dhamana ya madeni yao;
na katika nyumba ya Mungu wao
hunywa divai waliyotwaa kwa wadeni wao.
9“Hata hivyo, enyi watu wangu,
kwa ajili yenu, niliwaangamiza kabisa Waamori
ambao walikuwa wakubwa kama mierezi,
wenye nguvu kama miti ya mialoni.
Naam, niliwaangamiza, matawi na mizizi.
10Niliwatoeni kutoka nchi ya Misri,
nikawaongoza kupitia jangwani miaka arubaini,
mpaka mkaichukua nchi ya Waamori kuwa yenu.
11Niliwateua baadhi ya wana wenu wawe manabii,
na baadhi ya vijana wenu wawe wanadhiri.
Je, enyi Waisraeli,
haya nisemayo si ya kweli?
Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
12Lakini nyinyi mliwafanya wanadhiri wanywe divai,
na kuwaamuru manabii wasitoe unabii.
13“Sasa basi, nitawagandamiza mpaka chini,
kama gari lililojaa nafaka.
14Hata wapiga mbio hodari hawataweza kutoroka;
wenye nguvu wataishiwa nguvu zao,
na askari watashindwa kuyaokoa maisha yao.
15Wapiga upinde vitani hawatastahimili;
wapiga mbio hodari hawataweza kujiokoa,
wala wapandafarasi hawatayanusurisha maisha yao.
16Siku hiyo, hata askari hodari
watatimua mbio bila chochote.
Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Amosi2;1-16
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe
No comments:
Post a Comment