Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 9 June 2020

Kikombe Cha Asubuhi; Amosi 3...

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante  Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu


Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni

Neema yako yatutosha  Mungu wetu..!

“Kama vile mwizi aonavyo aibu akishikwa, ndivyo Waisraeli watakavyoona aibu; wao wenyewe, wafalme wao, wakuu wao, makuhani wao na manabii wao.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,
tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako

Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa  Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

Hao huuambia mti: ‘Wewe u baba yangu,’ na jiwe: ‘Wewe ndiwe uliyenizaa;’ kwa maana wamenipa kisogo, wala hawakunielekezea nyuso zao. Lakini wakati wa shida husema: ‘Inuka utuokoe!’
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe



Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu  wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo 

Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...

“Lakini iko wapi miungu yako uliyojifanyia? Iinuke basi, kama inaweza kukusaidia, wakati unapokuwa katika shida. Ee Yuda, idadi ya miungu yako ni sawa na idadi ya miji yako!
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba
 ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!


Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....

Nawapenda.

1Enyi Waisraeli, sikilizeni neno Mwenyezi-Mungu alilosema dhidi yenu, enyi taifa zima alilolitoa nchini Misri:
2“Kati ya mataifa yote ulimwenguni,
ni nyinyi tu niliowachagua.
Kwa hiyo nitawaadhibu nyinyi,
kwa sababu ya uovu wenu wote.”
Jukumu la nabii
3Je, watu wawili huanza safari pamoja,
bila ya kufanya mpango pamoja kwanza?
4Je, simba hunguruma porini
kama hajapata mawindo?
Je, mwanasimba hunguruma pangoni mwake
kama hajakamata kitu?
5Je, mtego bila chambo
utamnasa ndege?
Je, mtego hufyatuka
bila kuguswa na kitu?
6Je, baragumu ya vita hulia mjini
bila kutia watu hofu?
Je, mji hupatwa na janga
asilolileta Mungu?
7Hakika, Bwana Mwenyezi-Mungu hafanyi kitu
bila kuwafunulia watumishi wake manabii nia yake.
8Simba akinguruma,
ni nani asiyeogopa?
Bwana Mwenyezi-Mungu akinena,
ni nani atakataa kuutangaza ujumbe wake?
Kuangamizwa kwa Samaria
9Tangazeni katika ikulu za Ashdodi,
na katika ikulu za nchi ya Misri:
“Kusanyikeni kwenye milima
inayoizunguka nchi ya Samaria,
mkajionee msukosuko mkubwa
na dhuluma zinazofanyika humo.”
10Mwenyezi-Mungu asema hivi:
“Watu hawa wameyajaza majumba yao
vitu vya wizi na unyang'anyi.
Hawajui kabisa kutenda yaliyo sawa!
11Kwa hiyo, adui ataizingira nchi yao,
atapaharibu mahali pao pa kujihami,
na kuziteka nyara ikulu zao.”
12Mwenyezi-Mungu, asema hivi: “Kama vile mchungaji ampokonyavyo simba kinywani miguu miwili tu au kipande cha sikio la kondoo, ndivyo watakavyonusurika watu wachache tu wa Israeli wakaao Samaria, ambao sasa wanalalia vitanda vizuri na matandiko ya hariri.”3:12 vitanda vizuri na matandiko ya hariri: Maana katika Kiebrania si dhahiri.
13Bwana Mungu wa majeshi asema hivi:
“Sikilizeni, mkawaonye wazawa wa Yakobo:
14Siku nitakapowaadhibu Waisraeli
kwa sababu ya makosa yao,
nitayaharibu pia madhabahu ya mji wa Betheli.
Nitazikata pembe3:14 pembe: Hizi zilikuwa alama ya usalama.za kila madhabahu
na kuziangusha chini.
15Nitaziharibu nyumba zote mjini na vijijini;
nitazibomoa nyumba zilizopambwa kwa pembe,
majumba makubwamakubwa hayatasalia hata moja.
Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”


Amosi3;1-15

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe

No comments: