|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu katika yote....
Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana Mungu wa walio hai,Mungu mwenye huruma,Mungu wa upendo Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...Asante kwa wema na fadhili zako kwetu Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!
Walipokwisha amua tusafiri mpaka Italia, walimweka Paulo pamoja na wafungwa wengine chini ya ulinzi wa Yulio aliyekuwa ofisa wa jeshi katika kikosi kiitwacho “Kikosi cha Augusto.”
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako, Tukijinyenyekeza,tukijiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunamomba utusamehe dhambi zetu Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
Tulipanda meli ya Adiramito iliyokuwa inasafiri na kupitia bandari kadhaa za mkoa wa Asia, tukaanza safari. Aristarko, mwenyeji wa Makedonia kutoka Thesalonike, alikuwa pamoja nasi.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomna ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe...
Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Yahwe ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona,masikio ya kusikia sauti yako na kuitii.. Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako,tukasimamie Neno lako,amri na sheria zako siku zote za maisha yetu... Ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu,ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....
Kesho yake tulitia nanga katika bandari ya Sidoni. Yulio alimtendea Paulo vizuri kwa kumruhusu awaone rafiki zake na kupata mahitaji yake.
Tazama watoto wako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu kila mmoja na mahitaji yake Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipo kwenda kinyume nawe Yahweh tunaomba ukawape neema ya kuweza kujiombea,kufuata njia zako nazo zikawaweke huru... Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele... Amina...!!
Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,Baba wa Mbinguni aendelee kuwatendea sawasawa na mapenzi yake... Nawapenda. |
Adhabu kwa sababu ya kujiamini
1Ole wenu nyinyi mnaostarehe huko Siyoni,
nanyi mnaojiona salama mlimani Samaria!
Nyinyi mwaonekana kuwa viongozi wa taifa maarufu
ambao Waisraeli wote huwategemea.
2Haya! Nendeni Kalne mkaangalie kila mahali,
tokeni huko mwende hadi mji ule mkubwa wa Hamathi,
kisha teremkeni hadi Gathi kwa Wafilisti.
Je, falme zao si bora kuliko zenu
na eneo lao si bora kuliko lenu?”
3Nyinyi mnajaribu kuifukuza siku mbaya.
Lakini mnauleta karibu utawala dhalimu.
4Ole wenu mnaolala juu ya vitanda vya pembe za ndovu
na kujinyosha juu ya masofa,
mkila nyama za wanakondoo na ndama!
5Nyinyi mnapenda kuimba ovyo na sauti ya vinubi
na kubuni ala mpya za muziki mkimwiga mfalme Daudi.
6Mnakunywa divai kwa mabakuli,
na kujipaka marashi mazuri mno.
Lakini hamhuzuniki hata kidogo
juu ya kuangamia kwa wazawa wa Yosefu.
7Kwa hiyo mtakuwa wa kwanza kwenda uhamishoni,
na karamu za wenye kustarehe zitatoweka.
8Bwana Mwenyezi-Mungu ameapa kwa nafsi yake;
Mwenyezi-Mungu, Mungu wa majeshi asema:
“Nachukizwa mno na kiburi cha wazawa wa Yakobo;
tena nayachukia majumba yao ya fahari.
Mji wao na vyote vilivyomo nitawapa adui zao.”
9Kama wakibaki watu kumi katika nyumba moja, wote watakufa. 10Na atakapokuja mjomba wa aliyekufa kuitoa maiti nje aichome, akamwuliza yeyote atakayekuwako ndani pembeni mwa nyumba, “Je kuna mtu mwingine pamoja nawe?” Naye atamjibu, “La! Hamna!” Naye atamwambia, “Nyamaza kimya! Tusilitaje hata jina la Mwenyezi-Mungu.”6:10 maana ya aya hii katika Kiebrania si dhahiri.
11Tazama! Mwenyezi-Mungu anatoa amri,
nalo jumba kubwa labomoka vipandevipande,
na nyumba ndogo kusagikasagika.
12Je, farasi waweza kupiga mbio miambani?
Je, watu huilima bahari kwa ng'ombe?
Lakini nyinyi mmeigeuza haki kuwa sumu,
na tunda la uadilifu kuwa uchungu.
13Nyinyi mnashangilia juu ya Lodebari,6:13 Lodebari: Matumizi ya jina hili katika Kiebrania ni kama neno lenye maana “kitu batili” au “upuuzi.”
na kusema mmeuteka Karnaimu6:13 Karnaimu: Maana ya jina la mji huu mdogo ni “pembe” nazo ni alama ya nguvu. kwa nguvu zenu wenyewe.
14Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi:
“Enyi Waisraeli,
kweli nitaleta taifa moja lije kuwashambulia,
nalo litawatesa nyinyi kuanzia Lebo-hamathi kaskazini,
hadi kijito cha Araba, upande wa kusini.”
Amosi6;1-14
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe
No comments:
Post a Comment