|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu wetu katika yote...
Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetuAsante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu
Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni Neema yako yatutosha Mungu wetu..!
Heri watu wanaoishi bila kosa, wanaozingatia sheria ya Mwenyezi-Mungu. Heri wanaozingatia matakwa yake, wanaomtafuta kwa moyo wao wote,
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza, tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
watu wasiotenda uovu kamwe, bali daima hufuata njia zake. Ee Mungu, umetupatia kanuni zako ili tuzishike kwa uaminifu.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe
Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama inavyokupendeza wewe Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...
Laiti mwenendo wangu ungeimarika, kwa kuyafuata masharti yako! Nikizingatia amri zako zote, hapo kweli sitaaibishwa. Nitakusifu kwa moyo mnyofu, nikijifunza maagizo yako maadilifu. Nitayafuata masharti yako; usiniache hata kidogo.
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao Nuru yako ikaangaze katika maisha yao Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele Amina....!!!
Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana kwakuwanami/kunisoma Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea kama inavyompendeza yeye Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba ukae nanyi daima.... Nawapenda. |
Mika na wapinzani wake
1Ole wao wanaopanga kutenda maovu
wanaolala usiku wakiazimia uovu!
Mara tu kunapopambazuka,
wanayatekeleza kwani wanao uwezo.
2Hutamani mashamba na kuyatwaa;
wakitaka nyumba, wananyakua.
Huwadhulumu wenye nyumba na jamaa zao,
huwanyang'anya watu mali zao.
3Kwa hiyo, Mwenyezi-Mungu asema hivi:
“Ninapanga kuwaleteeni nyinyi maafa,
ambayo kamwe hamtaweza kuyakwepa.
Utakuwa wakati mbaya kwenu,
wala hamtaweza kwenda kwa maringo.
4Siku hiyo watu watawasimanga kwa wimbo,
watalia na kuomboleza kwa uchungu, wakisema:
‘Tumeangamia kabisa;
Mwenyezi-Mungu amechukua nchi yetu,
naam, ameiondoa mikononi mwetu.
Mashamba yetu amewagawia waliotuteka.’”2:4 waliotuteka: Makala ya Kiebrania: Waasi.
5Kwa hiyo hamtagawiwa sehemu yoyote ya ardhi
miongoni mwa watu wake Mwenyezi-Mungu.
Wapinzani wa nabii
6“Usituhubirie sisi.
Mambo kama hayo si ya kuhubiriwa.
Sisi hatutakumbwa na maafa!
7Je, yafaa kusema hivyo, wazawa wa Yakobo?
Je, Mwenyezi-Mungu ameacha uvumilivu wake?
Je, yeye hufanya mambo kama haya?”
Mika
Sivyo! Maneno yangu huwafaa watendao mambo mema.
8Lakini Mwenyezi-Mungu awaambia hivi:
“Nyinyi mnawavamia watu wangu kama adui.
Mnawanyang'anya mavazi yao watu watulivu;
watu wanaopita kwenda zao bila wasiwasi,
na wasio na fikira zozote za vita.
9Mnawafukuza wake za watu wangu
kutoka nyumba zao nzuri;
watoto wao mmewaondolea fahari yangu milele.
10Inukeni mwende zenu!
Hapa hamna tena pa kupumzika!
Kwa utovu wenu wa uaminifu
maangamizi makubwa yanawangojea!
11Kama mtu angetokea akatamka maneno matupu ya uongo
na kusema: ‘Nawatabirieni divai na pombe kwa wingi’,
mhubiri wa namna hiyo angependwa na watu hawa!
12“Lakini kweli nitawakusanya nyote enyi watu wa Yakobo,
naam, nitawakusanya enyi Waisraeli mliobaki,
niwalete pamoja kama kondoo katika zizi,
kama kundi kubwa la kondoo malishoni;
nanyi mtakuwa kundi la watu wengi.”
13Yule atakayetoboa njia atawatangulia,
nao watalivunja lango la mji na kutoka nje,
watapita na kutoka nje.
Mfalme wao atawatangulia;
Mwenyezi-Mungu mwenyewe atawatangulia.
Mika2;1-13
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe
No comments:
Post a Comment