|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tunamshukuru Mungu kwa kutupa kibali cha kupitia kitabu cha "YOELI" Ni matumaini yangu kuna mengi tumejifunza/kufaidika na kutupa mwanga/kuelewa kwenye kitabu hiki... Leo tunapokwenda anza kupitia Kitabu cha"AMOSI"tunamuomba Mungu wetu akatupe kibali,macho ya rohoni na akili ya kuelewa katika kujifunza NENO lake... Ee Mungu tunaomba ukatuongoze...!!Tumshukuru Mungu wetu katika yote... Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana Mungu wa walio hai,Mungu mwenye huruma,Mungu wa upendo Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...
Asante kwa wema na fadhili zako kwetu Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!
“Je, Israeli ni mtumwa, ama amezaliwa utumwani? Mbona basi amekuwa kama mawindo? Simba wanamngurumia, wananguruma kwa sauti kubwa. Nchi yake wameifanya jangwa, miji yake imekuwa magofu, haina watu.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza, tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
Isitoshe, watu wa Memfisi na Tahpanesi, wameuvunja utosi wake. Israeli, je, hayo yote si umejiletea mwenyewe, kwa kuniacha mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, niliyekuwa ninakuongoza njiani? Na sasa itakufaa nini kwenda Misri, kunywa maji ya mto Nili? Au itakufaa nini kwenda Ashuru, kunywa maji ya mto Eufrate?
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomna ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe...
Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Yahwe ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona,masikio ya kusikia sauti yako na kuitii.. Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako,tukasimamie Neno lako,amri na sheria zako siku zote za maisha yetu... Ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu,ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....
Uovu wako utakuadhibu; na uasi wako utakuhukumu. Ujue na kutambua kuwa ni vibaya mno kuniacha mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, na kuondoa uchaji wangu ndani yako. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimesema.
Tazama watoto wako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu kila mmoja na mahitaji yake Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipo kwenda kinyume nawe Yahweh tunaomba ukawape neema ya kuweza kujiombea,kufuata njia zako nazo zikawaweke huru... Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele... Amina...!!
Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,Baba wa Mbinguni aendelee kuwatendea sawasawa na mapenzi yake... Nawapenda.
|
Nabii Amosi
1Maneno ya Amosi, mmojawapo wa wachungaji wa mji wa Tekoa. Mungu alimfunulia Amosi mambo haya yote kuhusu Israeli miaka miwili kabla ya lile tetemeko la ardhi, wakati Uzia alipokuwa mfalme wa Yuda, na Yeroboamu mwana wa Yoashi, alipokuwa mfalme wa Israeli. 2Amosi alisema hivi:
Mwenyezi-Mungu ananguruma kutoka mlima Siyoni,
anavumisha sauti yake kutoka Yerusalemu,
hata malisho ya wachungaji yanakauka,
nyasi mlimani Karmeli zinanyauka.
Hukumu ya Mungu kwa mataifa jirani ya Israeli
Damasko
3Mwenyezi-Mungu asema hivi:
“Watu wa Damasko wametenda dhambi tena na tena;
kwa hiyo, sitaacha kuwaadhibu;
waliwatendea watu wa Gileadi ukatili mbaya.
4Basi, nitaishushia moto ikulu ya mfalme Hazaeli,
nao utaziteketeza kabisa ngome za mfalme Ben-hadadi.
5Nitayavunjavunja malango ya mji wa Damasko,
na kuwang'oa wakazi wa bonde la Aweni,
pamoja na mtawala wa Beth-edeni.
Watu wa Aramu watapelekwa uhamishoni Kiri.
Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Filistia
6Mwenyezi-Mungu asema hivi:
“Watu wa Gaza wametenda dhambi tena na tena,
kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu.
Walichukua mateka watu kabila zima,
wakawauza wawe watumwa kwa Waedomu.
7Basi, nitazishushia moto kuta za mji wa Gaza,
nao utaziteketeza kabisa ngome zake.
8Nitawang'oa wakazi wa mji wa Ashdodi,
pamoja na mtawala wa Ashkeloni.
Nitanyosha mkono dhidi ya Ekroni,
nao Wafilisti wote waliosalia wataangamia.
Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Tiro
9Mwenyezi-Mungu asema hivi:
“Watu wa Tiro wametenda dhambi tena na tena,
kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu.
Walichukua mateka kabila zima hadi Edomu,
wakaukiuka mkataba wa urafiki waliokuwa wamefanya.
10Basi, nitazishushia moto kuta za mji wa Tiro,
na kuziteketeza kabisa ngome zake.”
Edomu
11Mwenyezi-Mungu asema hivi:
“Watu wa Edomu wametenda dhambi tena na tena,
kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu.
Waliwawinda ndugu zao1:11 ndugu zao: Waisraeli walikuwa wazawa wa Yakobo, nduguye Esau, wazee wao Waedomu. Waisraeli kwa mapanga,
wakaitupilia mbali huruma yao yote ya kindugu.
Hasira yao haikuwa na kikomo,
waliiacha iwake daima.
12Basi, nitaushushia moto mji wa Temani,
na kuziteketeza kabisa ngome za Bosra.”
Amoni
13Mwenyezi-Mungu asema hivi:
“Watu wa Amoni wametenda dhambi tena na tena,
kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu.
Katika vita vyao vya kupora nchi zaidi,
waliwatumbua wanawake waja wazito nchini Gileadi.
14Basi, nitazishushia moto kuta za mji wa Raba,
na kuziteketeza kabisa ngome zake.
Siku hiyo ya vita patakuwa na makelele mengi,
nayo mapambano yatakuwa makali kama tufani.
15Mfalme wao na maofisa wake,
wote watakwenda kukaa uhamishoni.
Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Amosi1;1-15
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe
No comments:
Post a Comment