|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu katika yote....
Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana Mungu wa walio hai,Mungu mwenye huruma,Mungu wa upendo Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...Asante kwa wema na fadhili zako kwetu Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!
Wewe, ee Mwenyezi-Mungu, ndiwe riziki yangu kuu; naahidi kushika maneno yako. Naomba radhi yako kwa moyo wangu wote; unionee huruma kama ulivyoahidi!
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako, Tukijinyenyekeza,tukijiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunamomba utusamehe dhambi zetu Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
Nimeufikiria mwenendo wangu, na nimerudi nifuate maamuzi yako. Bila kukawia nafanya haraka kuzishika amri zako. Waovu wametega mitego waninase, lakini mimi sisahau sheria yako.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomna ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe...
Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Yahwe ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona,masikio ya kusikia sauti yako na kuitii.. Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako,tukasimamie Neno lako,amri na sheria zako siku zote za maisha yetu... Ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu,ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....
Usiku wa manane naamka kukusifu, kwa sababu ya maagizo yako maadilifu. Mimi ni rafiki ya wote wakuchao, rafiki yao wanaozitii kanuni zako. Dunia imejaa fadhili zako, ee Mwenyezi-Mungu, unifundishe masharti yako.
Tazama watoto wako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu kila mmoja na mahitaji yake Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipo kwenda kinyume nawe Yahweh tunaomba ukawape neema ya kuweza kujiombea,kufuata njia zako nazo zikawaweke huru... Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele... Amina...!!
Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,Baba wa Mbinguni aendelee kuwatendea sawasawa na mapenzi yake... Nawapenda. |
Kuanguka kwa Ninewi
1Mwangamizi amekuja kukushambulia ee Ninewi.
Chunga ngome zako!
Weka ulinzi barabarani!
Jiweke tayari!
Kusanya nguvu zako zote!
2Mwenyezi-Mungu anamrudishia Yakobo fahari yake,
naam, anawapa tena Waisraeli fahari yao,
ingawa wavamizi hawakuwaachia kitu,
hata matawi yao ya mizabibu waliyakata.
3Ngao za mashujaa wake ni nyekundu,
askari wake wamevaa mavazi mekundu sana.
Magari yao ya farasi2:3 farasi: Kiebrania: Miberoshi. yanamulika kama miali ya moto,
yamepangwa tayari kushambulia;
farasi hawatulii kwa uchu wa kushambulia.
4Magari ya farasi yanatimua mbio barabarani,
yanakwenda huko na huko uwanjani.
Yanamulika kama miali ya moto!
Yanakwenda kasi kama umeme.
5Sasa anawaita maofisa wake,
nao wanajikwaa wanapomwendea;
wanakwenda ukutani himahima
kutayarisha kizuizi.
6Vizuizi vya mito vimefunguliwa,
ikulu imejaa hofu.
7Mji uko wazi kabisa,
watu wamechukuliwa mateka.
Wanawake wake wanaomboleza,
wanalia kama njiwa,
na kujipigapiga vifuani.
8Ninewi ni kama bwawa lililobomoka,
watu wake wanaukimbia ovyo.
“Simameni! Simameni!” Sauti inaita,
lakini hakuna anayerudi nyuma.
9“Chukueni nyara za fedha,
chukueni nyara za dhahabu!
Hazina yake haina mwisho!
Kuna wingi wa kila kitu cha thamani!”
10Mji wa Ninewi ni maangamizi matupu na uharibifu!
Watu wamekufa moyo, magoti yanagongana,
nguvu zimewaishia, nyuso zimewaiva!
11Limekuwaje basi hilo pango la simba,
hilo lililokuwa maficho ya wanasimba?
Pamekuwaje hapo mahali pa simba,
mahali pa wanasimba ambapo hakuna aliyeweza kuwashtua?
12Simba dume amewararulia watoto wake nyama ya kutosha,
akawakamatia simba majike mawindo yao;
ameyajaza mapango yake mawindo,
na makao yake mapande ya nyama.
13Tazama, mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nitapambana nawe: Nitayateketeza kwa moto magari yako ya farasi, nitawamaliza kwa upanga hao simba wako vijana, nyara ulizoteka nitazitokomeza kutoka nchini, na sauti ya wajumbe wako haitasikika tena.
Nahumu2;1-13
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe
No comments:
Post a Comment