|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu wetu katika yote...
Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetuAsante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu
Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni Neema yako yatutosha Mungu wetu..!
Umenitendea vema mimi mtumishi wako, kama ulivyoahidi, ee Mwenyezi-Mungu. Unifundishe akili na maarifa, maana nina imani sana na amri zako.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza, tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti, Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
Kabla ya kuniadhibu nilikuwa nikikosea, lakini sasa nashika neno lako. Wewe ni mwema na mfadhili; unifundishe masharti yako.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe
Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama inavyokupendeza wewe Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...
Wenye kiburi wanasema uongo juu yangu, lakini mimi nashika kanuni zako kwa moyo wote. Mioyo yao imejaa upumbavu, lakini mimi nafurahia sheria yako. Nimefaidika kutokana na taabu yangu, maana imenifanya nijifunze masharti yako. Sheria uliyoweka ni bora kwangu, kuliko mali zote za dunia.
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao Nuru yako ikaangaze katika maisha yao Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele Amina....!!!
Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana kwakuwanami/kunisoma Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea kama inavyompendeza yeye Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba ukae nanyi daima.... Nawapenda. |
1Ole wako mji wa mauaji!
Umejaa udanganyifu mtupu na nyara tele,
usiokoma kamwe kuteka nyara.
2Sikia! Mlio wa mjeledi,
mrindimo wa magurudumu,
vishindo vya farasi
na ngurumo za magari!
3Wapandafarasi wanashambulia,
panga na mikuki inametameta;
waliouawa hawana idadi,
maiti wengi sana;
watu wanajikwaa juu ya maiti!
4Ninewi! Wewe umekuwa kama malaya.
Umewashawishi watu, ewe binti wa uchawi,
uliyeyafanya mataifa kuwa watumwa kwa umalaya wako,
na watu wa mataifa kwa uchawi wako.
5Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema nitapambana nawe;
nitalipandisha vazi lako hadi kichwani,
niyaache mataifa yauone uchi wako,
tawala ziikodolee macho aibu yako.
6Nitakutupia uchafu,
na kukutendea kwa dharau,
na kukufanya uwe kioja kwa watu.
7Kisha wote watakaokuona watakukimbia wakisema,
“Ninewi umeangamizwa,
ni nani atakayeuombolezea?
Nani atakayekufariji?”
8Je, wewe Ninewi, ni bora kuliko Thebesi,
mji uliojengwa kando ya mto Nili?
Thebesi ulizungukwa na maji,
bahari ilikuwa boma lake,
maji yalikuwa ukuta wake!
9Kushi ilikuwa nguvu yake;
nayo Misri pia, tena bila kikomo;
watu wa Puti na Libia waliusaidia!
10Hata hivyo, ulichukuliwa mateka,
watu wake wakapelekwa uhamishoni.
Hata watoto wake walipondwapondwa
katika pembe ya kila barabara;
watu wake mashuhuri walinadiwa,
wakuu wake wote walifungwa minyororo.
11Ninewi, nawe pia utalewa;
utamkimbia adui na kujaribu kujificha.
12Ngome zako zote ni za tini za mwanzo;
zikitikiswa zinamwangukia mlaji kinywani.
13Tazama askari wako:
Wao ni waoga kama wanawake.
Milango ya nchi yako ni wazi mbele ya adui zako;
moto umeyateketeza kabisa makomeo yake.
14Tekeni maji muwe tayari kuzingirwa;
imarisheni ngome zenu.
Pondeni udongo kwa kuukanyagakanyaga,
tayarisheni tanuri ya kuchomea matofali!
15Lakini huko pia moto utawateketezeni,
upanga utawakatilia mbali;
utawamaliza kama nzige walavyo.
Ongezekeni kama nzige,
naam, ongezekeni kama panzi!
16Wafanyabiashara wako waliongezeka kuliko nyota;
lakini sasa wametoweka kama panzi warukavyo.
17Wakuu wako ni kama panzi,
maofisa wako kama kundi la nzige;
wakati wa baridi wanakaa kwenye kuta,
lakini jua lichomozapo, huruka,
wala hakuna ajuaye walikokwenda.
18Ewe mfalme wa Ashuru, wachungaji wako wamelala,
waheshimiwa wako wamesinzia.
Watu wako wametawanyika milimani,
wala hakuna yeyote wa kuwakusanya.
19Hakuna wa kuyapa nafuu majeraha yako,
vidonda vyako ni vya kifo.
Wote wanaosikia habari zako wanashangilia.
Maana ni nani aliyeuepa ukatili wako usio na kikomo?
Nahumu3;1-19
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe
No comments:
Post a Comment