|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje? Haleluyah ni siku/wiki/mwezi mwingine tena Mungu wetu ametuchagua na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Si kwamba sisi tumetenda mema sana wala si kwa nguvu zetu si kwa utashi wetu wala si kwa akili zetu si kwamba sisi ni wazuri mno si kwa uwezo wetu sisi kuwa hivi tulivyo leo hii Ni kwa rehema/neema zake ni kwa mapenzi yake Mungu wetu.... Tunamshukuru Mungu kwa kutupa kibali cha kupitia kitabu cha "MIKA" Ni matumaini yangu kuna mengi tumejifunza/kufaidika na kutupa mwanga/kuelewa kwenye kitabu hiki... Leo tunapokwenda anza kupitia Kitabu cha"NAHUMU"tunamuomba Mungu wetu akatupe kibali,macho ya rohoni na akili ya kuelewa katika kujifunza NENO lake... Ee Mungu tunaomba ukatuongoze...!! Tumshukuru Mungu wetu katika yote...
Ukumbuke ahadi yako kwangu mimi mtumishi wako, ahadi ambayo imenipa matumaini. Hata niwapo taabuni napata kitulizo, maana ahadi yako yanipa uhai.
Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana Mungu wa walio hai,Mungu mwenye huruma,Mungu wa upendo Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...
Asante kwa wema na fadhili zako kwetu Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!! Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza, tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
Wasiomjali Mungu hunidharau daima, lakini mimi sikiuki sheria yako. Ninapoyakumbuka maagizo yako ya tangu kale, nafarijika, ee Mwenyezi-Mungu.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomna ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe...
Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Yahwe ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona,masikio ya kusikia sauti yako na kuitii.. Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako,tukasimamie Neno lako,amri na sheria zako siku zote za maisha yetu... Ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu,ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....
Nashikwa na hasira kali, nionapo waovu wakivunja sheria yako. Masharti yako yamekuwa wimbo wangu, nikiwa huku ugenini. Usiku ninakukumbuka, ee Mwenyezi-Mungu, na kushika sheria yako. Hii ni baraka kubwa kwangu, kwamba nazishika kanuni zako.
Tazama watoto wako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu kila mmoja na mahitaji yake Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipo kwenda kinyume nawe Yahweh tunaomba ukawape neema ya kuweza kujiombea,kufuata njia zako nazo zikawaweke huru... Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele... Amina...!!
Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,Baba wa Mbinguni aendelee kuwatendea sawasawa na mapenzi yake... Nawapenda. |
1Kauli ya Mungu juu ya Ninewi. Kitabu cha maono ya Nahumu wa Elkoshi.
Ghadhabu ya Mungu dhidi ya Ninewi
2Mwenyezi-Mungu ni Mungu mwenye wivu, mlipiza kisasi;
Mwenyezi-Mungu hulipiza kisasi na ni mwenye ghadhabu;
Mwenyezi-Mungu hulipiza kisasi kwa adui zake,
huwaka ghadhabu juu ya adui zake.
3Mwenyezi-Mungu hakasiriki upesi, lakini amejaa nguvu,
Mwenyezi-Mungu kamwe hatawaachilia wenye hatia.
Apitapo Mwenyezi-Mungu, huzuka kimbunga na dhoruba;
mawingu ni vumbi litimuliwalo na nyayo zake.
4Huikaripia bahari na kuikausha,
yeye huikausha mito yote.
Mbuga za Bashani na mlima Karmeli hunyauka,
maua ya Lebanoni hudhoofika.
5Milima hutetemeka mbele yake,
navyo vilima huyeyuka;
dunia hutetemeka mbele yake,
ulimwengu na vyote vilivyomo.
6Nani awezaye kuikabili ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu?
Nani awezaye kustahimili ukali wa hasira yake?
Yeye huimwaga hasira yake iwakayo kama moto,
hata miamba huipasua vipandevipande.
7Mwenyezi-Mungu ni mwema,
yeye ni ngome ya usalama wakati wa taabu.
Yeye huwalinda wote wanaokimbilia usalama kwake.
8Adui wakiivamia nchi kama mafuriko, yeye huwaangamiza;
huwafuatia na kuwafukuza mpaka gizani.
9Mbona mnafanya mipango dhidi ya Mwenyezi-Mungu?
Yeye atawakomesha na kuwaangamiza,
wala mpinzani wake hataweza kuinuka tena.
10 1:10 maana ya aya hii katika Kiebrania si dhahiri.Watateketezwa kama kichaka cha miiba,
kama vile nyasi zilizokauka.
11Kwako kumetoka aliyepanga maovu dhidi ya Mwenyezi-Mungu
aliyefanya njama za ulaghai.
12Mwenyezi-Mungu awaambia hivi watu wake:
“Ingawa Waashuru ni wengi na wenye nguvu,
wao wataangushwa na kuangamizwa.
Ingawa nimewatesa nyinyi watu wangu,
sitawateseni tena zaidi.
13Sasa nitaivunja nira ya Ashuru shingoni mwenu,
na minyororo waliyowafungia nitaikatakata.”
14Mwenyezi-Mungu ameamuru hivi kuhusu Ninewi:
“Hutapata wazawa kulidumisha jina lako.
Sanamu zako za kuchonga na za kusubu,
nitazivunjavunja nyumbani mwa miungu yako.
Mimi nitakuchimbia kaburi lako,
maana wewe hufai kitu chochote.”
15Enyi watu wa Yuda tazameni:
Anakuja kutoka mlimani mtu anayeleta habari njema,
mjumbe ambaye anatangaza amani.
Adhimisheni sikukuu zenu, enyi watu wa Yuda,
timizeni nadhiri zenu,
maana waovu hawatawavamia tena,
kwani wameangamizwa kabisa.
Nahumu1;1-15
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe
No comments:
Post a Comment