|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tunamshukuru Mungu kwa kutupa kibali cha kupitia kitabu cha "Nahumu" Ni matumaini yangu kuna mengi tumejifunza/kufaidika na kutupa mwanga/kuelewa kwenye kitabu hiki... Leo tunapokwenda anza kupitia Kitabu cha"Habakuki"tunamuomba Mungu wetu akatupe kibali,macho ya rohoni na akili ya kuelewa katika kujifunza NENO lake... Ee Mungu tunaomba ukatuongoze...!!Tumshukuru Mungu wetu katika yote...Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana Mungu wa walio hai,Mungu mwenye huruma,Mungu wa upendo Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...
Asante kwa wema na fadhili zako kwetu Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!
Mikono yako iliniumba na kuniunda; unijalie akili nijifunze amri zako. Wakuchao wataniona na kufurahi, maana tumaini langu liko katika neno lako.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza, tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
Najua hukumu zako ni adili, ee Mwenyezi-Mungu, na kwamba umeniadhibu kwani wewe ni mwaminifu. Fadhili zako na zinipe faraja, kama ulivyoniahidi mimi mtumishi wako. Unionee huruma nipate kuishi, maana sheria yako ni furaha yangu.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomna ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe...
Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Yahwe ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona,masikio ya kusikia sauti yako na kuitii.. Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako,tukasimamie Neno lako,amri na sheria zako siku zote za maisha yetu... Ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu,ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....
Wenye kiburi waaibike kwa maana wamenifanyia hila, lakini mimi nitazitafakari kanuni zako. Wote wakuchao na waje kwangu, wapate kuyajua maamuzi yako. Moyo wangu na uzingatie masharti yako, nisije nikaaibishwa.
Tazama watoto wako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu kila mmoja na mahitaji yake Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipo kwenda kinyume nawe Yahweh tunaomba ukawape neema ya kuweza kujiombea,kufuata njia zako nazo zikawaweke huru... Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele... Amina...!!
Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,Baba wa Mbinguni aendelee kuwatendea sawasawa na mapenzi yake... Nawapenda. |
1Kauli ya Mungu aliyoiona nabii Habakuki.
Lalamiko la nabii
2“Ee Mwenyezi-Mungu, nitakulilia mpaka lini,
nawe usinisikilize na kunisaidia?
Kwa nini nalia: ‘Dhuluma’
nawe hutuokoi?
3Kwa nini wanifanya nishuhudie mabaya na taabu?
Uharibifu na ukatili vinanizunguka,
ugomvi na mashindano yanazuka.
4Hivyo sheria haina nguvu,
wala haki haitekelezwi.
Waovu wanawazunguka waadilifu,
hivyo hukumu hutolewa ikiwa imepotoshwa.”
Jibu la Mungu
5 Taz Mate 13:41 Mungu akasema:
“Yaangalie mataifa, uone!
Utastaajabu na kushangaa.
Maana ninatenda kitu ukiwa bado unaishi,
kitu ambacho ungeambiwa hungesadiki.
6Maana ninawachochea Wakaldayo,
taifa lile kali na lenye hamaki!
Taifa lipitalo katika nchi yote,
ili kunyakua makao ya watu wengine.
7Wao ni watu wa kuchukiza na kutisha;
wao hujiamulia wenyewe nini haki na adhama.
8“Farasi wao ni wepesi kuliko chui;
wakali kuliko mbwamwitu wenye njaa.
Wapandafarasi wao wanatoka mbali,
wanaruka kasi kama tai arukiavyo mawindo.
9“Wote wanakuja kufanya ukatili;
kwa nyuso kakamavu wanasonga mbele,
wanakusanya mateka wengi kama mchanga.
10Wanawadhihaki wafalme,
na kuwadharau watawala.
Kila ngome kwao ni mzaha,
wanairundikia udongo na kuiteka.
11Kisha wanasonga mbele kama upepo,
wafanya makosa na kuwa na hatia,
maana, nguvu zao ndizo mungu wao!”
Habakuki analalamika tena
12“Je, wewe si ndiwe Mwenyezi-Mungu,
tangu kale na kale?
Wewe ndiwe Mungu wangu, Mtakatifu wangu, usiyekufa
Ee Mwenyezi-Mungu, umewateua Wakaldayo watuhukumu;
Ewe Mwamba, umewaimarisha ili watuadhibu!
13Wewe ni mtakatifu kabisa, huwezi kutazama uovu,
huwezi kustahimili kamwe kuona mabaya.
Mbona basi wawaona wafanya maovu na kunyamaza,
kwa nini unanyamaza waovu wanapowamaliza
wale watu walio waadilifu kuliko wao?
14“Umewafanya watu kama samaki baharini,
kama viumbe vitambaavyo visivyo na kiongozi!
15Wakaldayo huwavua watu kwa ndoana,
huwavutia nje kwa wavu wao,
huwakusanya wote katika jarife lao,
kisha hufurahi na kushangilia.
16Kwa hiyo, wanazitambikia nyavu zao,
na kuzifukizia ubani;
maana kwa hizo huweza kuishi kwa anasa,
na kula chakula cha fahari.
17“Je, hawataacha kamwe kuvuta upinde wao?
Je, wataendelea tu kuwanasa watu,
na kuyaangamiza mataifa bila huruma?
Habakuki1;1-17
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe
No comments:
Post a Comment