"Swahili Na Waswahili"Burudika.
Showing posts with label Burudani. Show all posts
Showing posts with label Burudani. Show all posts
Saturday, 20 April 2019
Wednesday, 21 September 2016
Kipindi cha Reggae Time Pride Fm Sept 17 2016.....Mahojiano na Innocent Galinoma
Karibu katika kipindi cha REGGAE TIME ya Pride Fm Mtwara Tanzania.
Na leo, ni mazungumzo yangu na Innocent Galinoma ambaye alikuwa mkarimu sana kufika Kilimanjaro Studios kwa mahojiano.
Ni kuanzia saa tisa kamili alasiri kwa saa za Afrika Mashariki, mbili kamili kwa Marekani Mashariki
Jiunge nasi kupitia 87.8 Fm kwa mikoa ya kusini, ama www.878pridefm.com ama kupitia TuneIn, bofya tun.in/seTTx.
Na leo, ni mazungumzo yangu na Innocent Galinoma ambaye alikuwa mkarimu sana kufika Kilimanjaro Studios kwa mahojiano.
Ni kuanzia saa tisa kamili alasiri kwa saa za Afrika Mashariki, mbili kamili kwa Marekani Mashariki
Jiunge nasi kupitia 87.8 Fm kwa mikoa ya kusini, ama www.878pridefm.com ama kupitia TuneIn, bofya tun.in/seTTx.
Saturday, 22 August 2015
Mshumaa wa wiki.....Barry White
Mshumaa wa wiki ni kipengele kinachozungumzia kuhusu msanii ama kundi la muziki wa zamani katika kipindi cha Mishumaa ya Kale
Kipindi hiki hukujia kila Ijumaa kuanzia saa 11 jioni mpaka 1 usiku kwa saa za Marekani ya Mashariki
Kinatayarishwa na kurushwa na Vijimambo Radio na Kwanza Production, kwa ushirikiano na NesiWangu Media
Kipindi hiki hukujia kila Ijumaa kuanzia saa 11 jioni mpaka 1 usiku kwa saa za Marekani ya Mashariki
Kinatayarishwa na kurushwa na Vijimambo Radio na Kwanza Production, kwa ushirikiano na NesiWangu Media
Saturday, 7 March 2015
Wednesday, 19 November 2014
MISHUMAA YA KALE...Kipindi kipya kutoka VIJIMAMBO na KWANZA PRODUCTION
Photo Credits: Ye Olde Vivyl Shoppe |
Katika kipindi hiki, utaweza "kuruka majoka" na "kula mangoma" kwa kusikiliza nyimbo ziliotamba miaka ya zamani, kupata historia ya wasanii na vikundi mbalimbali na pia kusikiliza mazungumzo na maDj na wasanii mbalimbali wa zamani.
Ungana na MixMaster Dj Luke Joe kwenye "one and two" na Mubelwa Bandio nyuma ya kipaza sauti kwenye kipindi kipya cha MISHUMAA YA KALE kitakachokujia kila Ijumaa kuanzia saa 11 kamili jioni mpaka saa 1 kamili usiku kwa majira ya Marekani ya Mashariki (5:00pm - 7:00pm EST)
Ungana nasi kupitia www.kwanzaproduction.com
MixMaster DJ Luke Joe. Photo Credits: IskaJojo Studios |
Mubelwa Bandio |
Saturday, 26 April 2014
Chaguo La Mswahili Leo;R.Kelly-The Storm Is OverI Now,I'm Your Angel na Nyingine!!!!!!
Nawatakia Mapumziko mema...
"Swahili Na Waswahili" Pamoja Daima.
Tuesday, 1 January 2013
Mtazamo wa John Kitime katika muziki 2012!!!!!!!
Mwaka 2012 ndio huoo umetokomea, ni vizuri kuangalia
yaliyopita ili kujitayarisha na yajayo. Muziki wa nchi yetu ulitawaliwa na
muziki wa Bongoflava, Taarab, muziki wa bendi, matarumbeta, muziki wa Enjili,
na muziki wa kiasili. Si siri kuwa muziki wa Bongoflava ndio uliokuwa ukitawala
katika vyombo vya habari na sehemu nyingi za maonyesho ukifuatiliwa na muziki
wa Taarab na muziki wa enjili. Katika
muziki wote huu jambo lililokuwa wazi ni kuwa waimbaji ndio waliokuwa wakipewa
kipaumbele katika tasnia hii. Waimbaji
katika aina zote za muziki uliotajwa hapo juu ndio waliotajwa na kupewa sifa
kwa ubora wa muziki. Kumekuweko na mashindano kadhaa ambayo yote yamejikita
katika kutafuta vipawa vya waimbaji japo mara nyingi yamejitambulisha kama
mashindano ya kusaka vipaji mbalimbali. Hakuna ubishi muziki wa dansi na muziki
wa asili ndio muziki uliopewa muda mchache sana katika vyombo vya habari. Na
hata katika muziki huo, bendi ambazo zimejikita kufuata mipigo ya Kikongo
vilipewa nafasi zaidi ya bendi ambazo zimejichagulia njia nyingine za muziki
wao.
Kuna sababu kadhaa ambazo zimefanya muziki wa bongoflava
kuchukua nafasi zaidi katika vyombo vya habari, la kwanza ni uwingi wa kazi za
bongoflava zinazorekodiwa. Karibu kila mji una studio ya aina moja au nyingine,
na katika studio hizo kazi nyingi zaidi zinazorekodiwa ni aina hiyo ya muziki,
hivyo kutokana na uwingi wa kazi hizo ni wazi kabisa ndizo ambazo zitaendelea
kutawala anga la vyombo vya habari, na pia ni kutokana na mfumo wa vyombo vyetu
vyote kujikita katika mfumo wa aina fulani tu za muziki.
Kwa mtizamo wangu heka heka za muziki wa Enjili zilipungua
2012. Yale matamasha makubwa ya muziki huo yalipungua sana, na hata nyimbo za
kushtua jamii hazikuwa nyingi kama
ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Muziki wa Taarab haujaleta mabadiliko kimuziki, mengi
yaliyofanywa katika 2012 ni marudio tu ya ubunifu uliofanyika nyuma. Kama vile
uanzishwaji wa kucheza show katika taarab, upigaji wa gitaa na kuliachia pekee
yake kama ilivyokuwa kwa bendi kuachia gitaa la rhythm miaka kabla ya tisini na
zile video za kucheza mbele za viwanja vya hoteli. Kumekuweko tu ubunifu wa
misemo na mipasho, jambo tena ambalo limesababisha kuenziwa zaidi kwa waimbaji
tu katika fani hiyo pia.
Bendi ziko katika wakati mgumu, wakati wanamuziki wengi wa
bendi wakilalamika kuwa muziki wa bendi haupigwi, kumekuweko na jitihada ndogo
za bendi kurekodi nyimbo mpya, maelezo mengi yamekuwa ni kuhadithia enzi ambapo
muziki wa bendi ulitawala na kuona kama hiyo ni sababu tosha ya muziki huo
kurushwa hewani. Bendi chache zilizorekodi hazijaja na nyimbo zilizoweza kuteka umma wa wa Tanzania
na hivyo kusababisha muziki huu kukosekana katika anga za muziki. Matangazo
mengi ya muziki wa dansi yamekuwa ni kutangaza rap mpya au kupatikana kwa
msanii mpya, lakini kiujumla hakujakuwa na kitu kipya katika muziki wa bendi.
Muziki asili pia umekosekana kwenye vyombo vya habari kwa
kuwa si vikundi vingi vya muziki huu vyenye uwezo wa kulipia gharama za studio
ambao muziki huu unastahili kurekodiwa. Studio nyingi zimejengwa kwa ajili ya
muziki wa aina ya Bongoflava tu, zile studio za kuweza kuruhusu kundi la muziki
wa asili kurekodi gharama yake huwa ni kubwa sana.
Kundi la Makirikiri lilitakiwa kuwa elimu tosha kwa
wasanii wa muziki wa Kiasili, kuwa na muziki huo ukifuata taratibu nzuri ya
kurekodiwa unauza vizuri sana, bahati mbaya kuna vikundi sasa vimeacha muziki
na ngoma zao, vinaiga uchezaji wa
Makirikiri.
Pengine watu watasema nimesahau muziki wa kwaya,
sijausahau, kwa kweli muziki huu umebaki
hasa kwenye muziki wa Enjili. Hapo zamani ulikuwa ukitumika sana kwenye
siasa na kampeni , lakini kwa mwaka 2012 hali imekuwa mbaya kwa muziki huu.
Pamoja na kuwa wengine wangeweza kusema tunasonga mbele
katika muziki, kwangu mimi naona tunarudi nyuma kitaaluma. Tasnia inaingiza
pesa nyingi zaidi, na hata kuna wasanii walioingiza pesa nyingi sana,
lakini kwangu hilo si kipimo cha
maendeleo katika tasnia hii.
Kama nilivyoanza kusema washika maikrofon wamekuwa ndio
alama ya muziki wa Tanzania. Muziki ni zaidi ya kuimba. Katika kuimba sauti
nzuri ya muimbaji ni muhimu, na ninashukuru kwa hilo tunao waimbaji wazuri
wengi sana, lakini ule muziki
unaomsindikiza muimbaji ni muhimu sana kwani ule hauna mipaka wala lugha, na
ndio unaoweza kutufungulia mlango wa soko la kimataifa. Wengi tunapenda sana
muziki wa kutoka Kongo, Nigeria, South Africa, pamoja na kuwa hatujui hata moja
wanaloliongelea tunaupenda muziki huo kutokana na mpangilio wa vyombo vyao.
Kutokujali wapigaji katika mfumo wa nchi yetu ndio unatupelekea kuwa watu wa ‘copy
and paste’ wa upigaji wa muziki wa nchi nyingine. Ukiorodhesha nyimbo zote
zilizotikisa nchi hii kwa mwaka 2012 utagundua asilimia kubwa ya muziki
uliotumika ulikuwa ni wa kunakili kutoka muziki wa nchi nyingine, Nigeria,
Congo na Afrika Kusini ndio wamekuwa waalimu wetu wakuu. Ushauri kwa maproducer
wa Bongoflava, kuangalia pia muziki wetu wa asili humu ndani ya nchi ili tuje
tumalize 2013 na kitu chetu ambacho Wanaigeria, Wakongo nao pia waige toka
kwetu. Inawezekana sana maana wimbo wa Weekend wa Afro70 uliwahi kuweko
katika kumi bora 1972, Nigeria.
Muziki wa Enjili pamoja na kuwa ndio unaotegemewa
kutufundisha maadili, ulikuwa na kasoro moja kubwa nayo ni kukosa maadili kwa
kucopy na kupaste. Nyimbo nyingi zilizokuwa maarufu na kuteka hisia za maelfu
ya watu zilikuwa ni kuiga moja kwamoja kutoka Afrika ya kusini. Najiuliza je
ndio kilichopunguza moto wa muziki huu 2012? Kulikuwa hakuna za kukopi?
Wanamuziki wa Enjili kama ilivyo kwa ushauri kuhusu Bongoflava, ni muda wa
kurudi nyuma na kutumia raslimali ya utamaduni iliyoko kuleta mabadiliko na
kukuza soko la muziki huo.
Tasnia ya muuziki wa Tanzania katika tafiti moja wapo
umeitwa ‘the radio-driven contemporary music industry’. Kwa maneno rahisi,
tasnia ambayo imekuwa inaendeshwa na radio. Radio zimekuwa na uwezo wa
kumpandisha na kumshusha mwanamuziki, kumtafutia soko, kumzibia soko na
kadhalika. Hali hii ikisindikizwa na rushwa ambayo imetapakaa katika jamii
yetu, unapata picha kuwa kungeweza kukawa na sura bora au tofauti ya muziki
hali isingekuwa ilivyo. Kuna ripoti za watu kutoa hongo nyimbo za wenzao
zisipigwe, hongo ili nyimbo zipigwe, visasi vya kuzuia nyimbo zisipigwe na
kadhalika. Na katika jamii ambayo imekuwa na kawaida ya kutegemea vyombo vya
habari kujua muziki gani mpya na mzuri, uwanja huu si uwanja ulio tambarare
hata kidogo. Bahati mbaya inaonekana wenye vyombo hivi wako mbali na ukweli
unaoendelea katika vyombo vyao au kwa kutokujua au kupuuza. Janga hili
limevikumba hata vyombo ambavyo vinaendeshwa na taasisi za dini. Wanamuziki wa muziki
wa Enjili nao pia wanalia kudaiwa rushwa na watangazaji wa radio za
Enjili!. Nakumbuka siku niliyopata
nafasi kuongea na kiongozi mmoja wa dini ambaye Kanisa lake linaendesha kituo
cha radio, nilipata mshangao baada mkuu huyo, kuanza kutetea watangazaji wake
badala ya kuamua kufanya uchunguzi wa tuhuma.
Umefika muda wa radio kuanza kujigawa kimuziki. Ni
kichekesho mji kuwa na vituo vya radio 30 halafu vyote vinapiga aina hiyohiyo
ya muziki, wakati kuna aina mbalimbali za watu. Ajabu ni kuwa wenye radio
wanajua kuwa katika nchi nyingine unaweza kukuta radio iliyoamua kupiga aina
fulani tu ya muziki, Jazz Radio, Country music Radio, Classic Music Radio,
lakini hilo limekuwa gumu kwao kutekeleza hapa. Kuwe na utofauti, Wasikilizaji
tuko wa aina tofauti.
Vyombo vya habari viijitahidi kupata wataalamu husika wa
aina tofauti za muziki, muziki unaviingizia vyombo hivyo mabilioni ya fedha,
vyombo vya habari viupe heshima yake.
Bila muziki hakuna radio.
Magazeti yamekuwa mstari wa mbele katika kutangaza aina mbalimbali
za wasanii na sanaa. Pamoja na hongera kwa kazi nzuri lakini bado kuna nafasi
kubwa ipo tupu, hakuna wataalamu wa uandishi wa habari za muziki. Hivyo habari
nyingi za muziki zinaandikwa na waandishi kama wapenzi wa muziki na si wataalam
wa uandishi wa muziki, jambo ambalo liko tofauti na uandishi wa michezo kwa
mfano soka. Unaweza ukasoma habari ya soka ambapo mwandish atakueleza nafasi za
wachezaji, kama ni faulo, ni nini kilisababisha, na kama ni goli lilikuwa ni la
kichwa au kona au penalty, hili haliko katika muziki. Utaambiwa tu bendi ilipagawisha, au msanii fulani ateka
nyoyo za wapenzi, na maelezo ya juu juu kama yale, kunahitajika kuanzishwa
mafunzo ya elimu ya uandishi wa kazi za sanaa. Hili litapunguza hata vurugu
kama zilizotawala mwaka huu ya wapiga picha kufikia hata kulala chini ili
tu wapate picha ya nguo za ndani za msanii na hayo ndio kuwa maelezo makuu ya
onyesho zima la muziki.
Ikiwa kulikuwa na mchango wa serikali katika muziki, basi
ulikuwa mdogo au ulikuwa ni kwa shughuli maalumu lakini si kwa kutengeneza
mazingira ya kuwezesha unafuu kwa wanamuziki kwa ujumla. Idara ya Utamaduni
imeendelea kupata bajeti ndogo ambayo imefanya Baraza La Sanaa La Taifa
kuendelea kubaki Dar es Salaam tu, likibangaiza kuweko kwa kutegemea kutoa vibali
mbalimbali kwa wasanii, na nguvu zake kuonekana Dar es Salaam tu. Na kwa kuwa
hakuna Maafisa Utamaduni Mkoa, na Maafisa Utamaduni Wilaya na Manispaa wako
chini ya serikali za mitaa hivyo kuwa wizara tofauti na Waziri wa Utamaduni,
nguvu za serikali katika utamaduni ni 0. COSOTA chombo ambacho shughuli yake
ilikuwa ni kulinda hakimiliki za wasanii na ambacho kilikuwa chini ya wasanii,
kwa kinyemela kabisa kimerudishwa katika mikono ya serikali, lakini bado
kinakusanya mirabaha 'kwa niaba ya wasanii' huku kukiwa na bodi isiyo na
uwakilishi wa wasanii kuanzia 2007. Swali utakusanyaje pesa kwa iaba yangu
lakini huniruhusu kujua ni kiasi gani umekusanya, unazitumiaje na ukiulizwa
unakuwa mkali!!!!!!? Kuna wasanii wamekuwa wakidai kurudishiwa COSOTA, ushauri wangu
wasanii wakae wajipange na kuelewa vizuri sheria ya Hakimiliki kabla ya
kujitwishwa zigo hilo la miba.
Katika miezi 6 ya mwisho ya 2012 kumejitokeza spidi kali
ya Mamlaka ya Ukusanyaji wa Mapato kutengeneza mazingira ya kukusanya mapato
kutokana na mauzo ya kazi za muziki na filamu. Kimsingi kulipa kodi ni wajibu
wa kila mwananchi na wasanii ni wananchi pia, lakini taratibu zake ndio
zinanipa utata, hasa pale ambapo kwa muda mrefu imekuwa ikitangazwa kuwa njia
hii itasaidia wasanii kwa kupunguza kuibiwa.
Sentensi hii inaonyesha wazi anaeiongelea aidha hajui mfumo wa biashara
ya kazi muziki, au kwa makusudi anapotosha ili kuficha kitu. Wasanii wengi huwa
wamekwishalipwa kwa kazi ambazo zimesambaa na ziko barabarani zinaibiwa,
wanaoibiwa ni wasambazaji. Hivyo kulinda kazi hizo unamlinda msambazaji si
msanii. Pia kuanza kukusanya kodi kwa kazi hizi kumepewa jina ‘kurasmishwa kwa kazi ya usanii’, kuna mabilioni wasanii
wanatakiwa walipwe na watumiaji wa kazi za sanaa, kama radio na TV, mapromota,
waajiri na kadhalika hakuna anaeliongelea hilo wala hakuna anaetamka
takwimu hizo. Kuna kazi ya kurudisha mitaala ya masomo ya sanaa mashuleni,
kurudisha vyuo vya walimu wa sanaa, kurudisha maafisa utamaduni kuwa chini ya
Wizara ya Utamaduni kuwawezesha kufanya kazi zao kadri ya sera ya Utamaduni, na
mengine mengi ya aina hiyo ndio ningeona kurasimisha kazi za sanaa, lakini
kukusanya kodi tu kwa kazi ambazo hata hivyo mikataba yake mingi inautata na
kuita urasimishaji si sahihi.
Katika nchi nyingi critics au watu ninaoweza kuwaita
kiswahili wakosoaji, huwa ni muhimu katika maendeleo ya sanaa, watu hawa hupata
heshima kutokana na kuweza kuangalia mapungufu katika kazi za sanaa na
kuyasema, jambo ambalo hupelekea wasanii kujirekibisha na kutengeneza kazi bora
zaidi. Hapa kwetu kutoa ushauri ni kutafuta matusi, toka kwa wasanii wenye kazi
husika, vyombo vya habari na hata sehemu ya jamii, umefika muda wahusika
kuchukua uchambuzi kama changa moto za kuboresha kazi.
Niliyoyataja hapa yote yako wazi ninachotegemea ni kuona
2013, hatua zinaanza kupigwa kurekibisha, ili wanamuziki wa nchi hii nao wapate
nafasi sawa na wengine wa nchi nyingine.
John Kitime
31.12.2012
Sinza, Dar es Salaam
"Swahili Na Waswahili" Pamoja Sana.
Saturday, 22 December 2012
Music Festival 2012:Banana Zorro & B Band!!!!!!
B Band chini ya kiongozi mmiliki Banana Zoro ikitoa burudani ya moja kwa moja kwenye Tamasha kubwa la muziki wa dansi Tanzania lililofanyika kwa siku mbili tarehe 28 na 29 Septembe ,2012 ambalo lilishirikisha bendi mbalimbali maarufu katika viwanja vya Leaders, Dar es Salaam.
B Band chini ya kiongozi mmiliki Banana Zoro ikitoa burudani ya moja kwa moja kwenye Tamasha kubwa la muziki wa dansi Tanzania lililofanyika kwa siku mbili tarehe 28 na 29 Septembe ,2012 ambalo lilishirikisha bendi mbalimbali maarufu katika viwanja vya Leaders, Dar es Salaam.
"Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.
Tuesday, 6 November 2012
Ngoma Africa Band growing stronger and stronger in Europe !!!
Ngoma Africa Band, a German based Tanzanian band is now one of the oldest and most successful Africans bands in Germany.
Many African bands in Europe hardly survive for more than a year. Yet Ngoma Africa Band, founded by Ebrahim Makunja aka Ras Makunja in 1993, is still growing stronger.
The band plays "Bongo Dance", which is a unique combination of traditional and modern Tanzanian rhythms with Soukous and Rumba. All theirs songs are in Kiswahili.
Ngoma Africa Band has released several successful hits including "Mama Kimwaga" (Sugar Mummy), "Anti-Corruption Squad" and "Apache wacha Pombe" (Stop over drinking).
In 2010 Ngoma Africa Band released a single in praise of Tanzania's President Jakaya Kikwete. The song titled "Jakaya Kikwete 2010" praises Mr. Kikwete's good leadership skills and commitment to fight corruption.
On 12th August 2012, Ngoma Africa Band received the International Diaspora Award (IDA) at the International African Festival Tubingen 2012, Germany, for their hard work in promoting East African music throughout Europe.
Ms. Susan Muyang Tatah, CEO of the International African Festival Tubingen 2012 said Ngoma Africa Band was also chosen for the Award because of their creative performance on stage. It's difficult to resist dancing at their concerts, she said.
This year the band released a new CD titled "Bongo Tambarare" featuring "Supu ya Mawe" and "Uhuru wa Habari". The new release is already dominating air waves in Tanzania.
"Supu ya Mawe" advices the listeners to work hard and be patient while pursuing their objectives in life. It also appeals for generosity towards the needy.
"Uhuru wa Habari" praises African journalists who are bold enough to speak out the truth in environments where freedom of speech is quite limited.
Ngoma Africa Band is famous for staging thrilling shows in festivals in different parts of Europe. The band's joyful female dancers, wearing traditional costumes and dancing vigorously to their tunes, always leave fans asking for more.
Ngoma Africa Band is composed of talented young musicians including soloist Christian Bakotessa aka Chris-B, Said Vuai, Matondo Benda, Jonathan Sousa, A-Jay, Richard Makutima, Bedi Beraca "Bella" and Jessy Ouyah.
For further information about Ngoma Africa Band and to listen to their music, please visit
Ngoma Africa Band has released several successful hits including "Mama Kimwaga" (Sugar Mummy), "Anti-Corruption Squad" and "Apache wacha Pombe" (Stop over drinking).
In 2010 Ngoma Africa Band released a single in praise of Tanzania's President Jakaya Kikwete. The song titled "Jakaya Kikwete 2010" praises Mr. Kikwete's good leadership skills and commitment to fight corruption.
On 12th August 2012, Ngoma Africa Band received the International Diaspora Award (IDA) at the International African Festival Tubingen 2012, Germany, for their hard work in promoting East African music throughout Europe.
Ms. Susan Muyang Tatah, CEO of the International African Festival Tubingen 2012 said Ngoma Africa Band was also chosen for the Award because of their creative performance on stage. It's difficult to resist dancing at their concerts, she said.
This year the band released a new CD titled "Bongo Tambarare" featuring "Supu ya Mawe" and "Uhuru wa Habari". The new release is already dominating air waves in Tanzania.
"Supu ya Mawe" advices the listeners to work hard and be patient while pursuing their objectives in life. It also appeals for generosity towards the needy.
"Uhuru wa Habari" praises African journalists who are bold enough to speak out the truth in environments where freedom of speech is quite limited.
Ngoma Africa Band is famous for staging thrilling shows in festivals in different parts of Europe. The band's joyful female dancers, wearing traditional costumes and dancing vigorously to their tunes, always leave fans asking for more.
Ngoma Africa Band is composed of talented young musicians including soloist Christian Bakotessa aka Chris-B, Said Vuai, Matondo Benda, Jonathan Sousa, A-Jay, Richard Makutima, Bedi Beraca "Bella" and Jessy Ouyah.
For further information about Ngoma Africa Band and to listen to their music, please visit
By Stephen Ogongo Ongong'a
Subscribe to:
Posts (Atom)