Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Ibada/Maombelezo. Show all posts
Showing posts with label Ibada/Maombelezo. Show all posts

Monday, 2 November 2015

[PICHA]: MISA YA MAREHEMU MAMA GREN JUDICA MOSHI Washington DC


Ndugu, jamaa na marafiki mbalimbali, jana (Novemba mosi 2015) walijumuika na wanafamilia katika misa na kusherehekea maisha ya Mama Gren Judica Moshi iliyofanyika hapa Washington DC

Watoto wawili wa Marehemu Donald na James Moshi, na ndugu wengine, waliungana kwa misa hiyo iliyofanyika alasiri na kufatiwa na chakula cha pamoja

Mchungaji kiongozi wa Kanisa la The Way of the Cross Gospel Ministries Ferdnand Shideko, akiwakaribisha watu waliohudhuria misa hiyo

Mch John Kadyolo akifungua misa kwa maombi

 Wanafamilia

Sunday, 1 November 2015

IBADA YA KUMBUKUMBU YA MAREHEMU GODFREY MNGODO, COLUMBUS, OHIO


Pr. Mwakabonga akiongoza ibada ya kumbukumbu ya marehemu Godfrey Mbiu
Mngodo iliyofanyika siku ya Jumamosi Octoba 31, 2015 Columbus, Ohio nchini
Marekani na kuhudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki wakiwemo wafanyakazi wa
kituo cha utangazaji Sauti ya Amerika idhaa ya Kiswahili (VOA). Marehemu
Godfrey Mbiu Mngodo aliaga Dunia Tarehe 11 Septemba, 2015 Dar es Salaam na
kuzikwa Tanga. Godfrey Mbiu Mngodo amefanya kazi katika sehemu
mbalimbali kama Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD), Voice of America,
wizarani na kituo cha Channel Ten ameacha watoto 10 na wajukuu 14. PICHA NA
KWANZA PRODUCTION/VIJIMAMBO
Mmoja ya mtoto wa marehemu Michael Mngodo akiwa na mwanae Alvin
wakifuatilia ibada ya kumbukumbu ya mpendwa baba yake marehemu Godfrey Mbiu
Mngodo iliyofanyika siku ya Jumamosi Octoba 31, 2015 Columbus, Ohio nchini
Marekani.
Familia ya Mngodo ikifuatilia Ibada.
Pr. Mwakaboma akifanya maombi kwa wanafamilia.
Michael Mngodo akisoma wasifu wa mpendwa baba yake. Kulia ni mtoto wake
Alvin.
Ndugu, jamaa na marafiki wakifuatilia ibada. Kwa Picha zaidi bofya HAPA

Monday, 5 October 2015

Ibada ya kumuombea Mama Kateng'anyenyi iliyofanyika Silver Spring MD






Broadcast live streaming video on Ustream





Broadcast live streaming video on Ustream



Padri Lehandly Kimario akiongoza ibada ya kumuombea mpendwa dada, mama na bibi yetu Bettisheba Pole Ketang'enyi iliyofanyika siku ya Jumapili Octoba 4, 2015 Silver Spring, Maryland nchini Marekani.


Mtoto wa marehemu Felicia Simms akisoma wasifu wa marehemu katika ibada ya kumuombea mpendwa dada, mama, bibi Bettisheda Pole Keteng'enyi iliyofanyika siku ya Jumapili  Octoba 4, 2015 Silver Spring, Maryland nchini Marekani.

Kwa picha zaidi bofya HAPA