(Lifestyle)Jamii,Tamaduni ,Matukio,Maisha ya Waswahili. Wapendao Kiswahili/Waswahili,Marafiki wa Swahili na Waswahili, Na Mengineyo ya Karibu, Yahitajikayo Kujuzwa Waswahili.Karibuni sana!!!!!!!
Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Mahojiano/Burudani. Show all posts
Showing posts with label Mahojiano/Burudani. Show all posts
Kwa kuanzia kama hujawahi kumsikia Saidi Kanda sikiliza wimbo maarufu "Nasikitika " wa Remmy Ongala. Hizo ngoma kali zinapigwa na nguli huyu mzawa wa Bagamoyo.
Mwezi huu, Desemba 2017, Saidi Kanda yuko safarini Kenya na Tanzania kushughulikia muziki yake.
Anahesabiwa kati ya wapiga ngoma stadi ulimwenguni. Alitunukiwa tuzo ya kwanza ya shirika maarufu la WOMAD - mwaka 1989.
Sehemu ya pili ya mazungumzo na Mwanamuziki huyu wa Jadi- Mpiga ngoma mkali - Saidi Kanda- mkazi Uingereza- anazungumzia THAMANI ya Ngoma na vyombo vyetu asilia.
Mwaka 1989 shirika maarufu la muziki Uingereza , WOMAD, lilimtunuku Mtanzania Saidi Kanda tuzo la Mpiga Ngoma wa Kimataifa wa Mwaka duniani. Kuanzia hapo mzawa huyu wa Bagamoyo aliyezaliwa 1962, anahesabika mpiga ngoma wa nne kiufundi ulimwenguni chini ya magwiji hatari kama Airto Morreira (Brazil) na Changuito (Cuba) ...
Baada ya kusakata vituz na wanamuziki mbalimbali akiwemo marehemu Remmy Ongala, Kofi Olomide na msanii maarufu wa kimataifa, Grace Jones; leo Kanda anaongoza kikosi chake kikali cha "Mvula Mandondo" kutangaza albam yake ya kwanza, "Ambush"....
KWA SIMU TOKA LONDON inawaletea sehemu ya kwanza ya Sura Tano za mahojiano kumtathmini mtunzi huyu anayetetea (na kuhusudisha ), sana muziki wa kiasili wa Kitanzania nje na ndani ya Afrika Mashariki.
Machi 16 2017, Mubelwa Bandio na Viola walipata nafasi ya kufanya mazungumzo na Dj D-Ommy katika studio za Kilimanjaro Studios. Dj D-Ommy ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi nchini Marekani amezungumza mengi kuhusu maisha, kazi na tasnia nzima ya muziki. Pia akapata fursa kuzindua rasmi kifaa kipya cha kazi kwa studio yetu, Pioneer DDJ SZ2 Karibu utazame ukisikiliza
Karibu katika mahojiano kati ya Mubelwa Bandio na Jhiko Manyika a.k.a JhikoMan aliyejiunga nasi moja kwa moja kutoka Bagamoyo Tanzania Alizungumzia wimbo wake mpya wa Africa Arise, ambao amemshirikisha Peter Morgan wa kundi la Morgan Heritage. Amezungumza mengi kuuhusu Karibu usikilize hapa chini
Pia unaweza kurejea mahojiano kati yao wakati JhikoMan akiwa ziarani Ulaya mwaka 2014. Alizungumza mengi kuhusu muziki wa reggae Tanzania lakini pia aligusia "projects" mbalimbali ambazo ziko njiani kuja
JhikoMan akitumbuiza kwenye Tamasha la Majahazi 2013
Karibu katika mahojiano kati ya Kwanza Production na Jhiko Manyika a.k.a JhikoMan aliyejiunga nasi moja kwa moja kutoka Helsinki Finland mwishoni mwa mwezi Julai
Amezungumza mengi kuhusu ziara yake ya Ulaya iliyoanza mwezi wa nne, maonyesho aliyofanya, kazi alizorekodi na pia watu aliowashirikisha kwenye albamu yake mpya ijayo.
Amezungumzia IMANI ya RASTA na pia MUZIKI WA TANZANIA kwa ujumla
Diamond Platnumz na DMK kwenye utoaji tuzo za BET Los Angeles Photo Credits: DMK Global Promotions' facebook page
Karibu katika mahojiano ya Kwanza Production na Damond Platnumz. Msanii mwenye mafanikio makubwa kutoka nchini Tanzania Amejiunga nasi kwa njia ya simu punde baada ya kuhudhuria utoaji tuzo za BET ambako yeye alikuwa mmoja wa waliokuwa wakiwania tuzo hizo. Kazungumza mengi kuhusu TUZO HIZO. Alipopokea na alivyopokea uteuzi wake, aliloliona kwenye tuzo hizo, ulinganishaji wake katika utoaji tuzo hizi na za Tanzania / Afika, alichojifunza, faida ya kuja kushiriki hili na hata mikakati yake ijayo kuhakikisha kuwa muziki wa Tanzania unafika mbali zaidi. SWALI jingine alilojibu ni kuwa....ni kweli kuwa ili muziki wa Tanzania ushinde tuzo ni lazima uwe na mahadhi ya Afrika Magharibi (kama muziki wake wa Number One) ama Afrika Kusini Amejiunga nasi kwa msaada wa promota Dickson Mkama almaarufu DMK ambaye pia ndiye meneja wa msanii huyo hapa nchini. KARIBU
Karibu katika mahojiano kamini kati ya Kwanza Production na NURU THE LIGHT. Msanii, Mjasiriamali, Mtangazaji, Blogger na Mwanaharakati ambaye amekuwa mkarimu sana kujiunga nasi moja kwa moja kutoka Stockholm Sweden Kazungumza mengi ikiwa ni pamoja na alivyoanza muziki Kisha akagusia kuhusu onyesho lake la kwanza kabisa jukwaani. Na kama nilivyokuja kumtambua, ni mtu mwenye misimamo na anayejitambua, utamsikia msimamo wake awapo studio Nikataka kujua pia, nini anaona kama tatizo kubwa kwenye muziki wetu? Haya ni machache kati ya mengi aliyozungumza nami JIUNGE NASI
Katika NJE NDANI wiki hii, mbali na habari kutoka Afrika, utasikia mahojiano yangu na NURU THE LIGHT. Msanii, Mjasiriamali, Mtangazaji, Blogger na Mwanaharakati ambaye amekuwa mkarimu sana kujiunga nami kutoka Stockholm Sweden Kazungumza mengi mema Jiunge nami, MUBELWA BANDIO Jumamosi (June 28) katika NJE NDANI ya Kwanza Production na Border Radio kuanzia saa sita mpaka saa nane mchana kwa saa za Marekani ya mashariki kupitia www.kwanzaproduction.com ama www.bordermediagroup.com
Anna Mwalagho. Photo Credits Anna Mwalagho Facebook page
Karibu katika mahojiano mafupi na ya moja kwa moja kati ya msanii Anna Mwalagho na Kwanza Production kwenye kipindi cha NJE-NDANI Jumamosi Juni 14, 2014 Amezungumzia tamasha kubwa linaloendelea ambalo atatumbuiza pamoja na kikundi chake kwa siku tatu
Tamasha hilo linaandaliwa kwa ushirikiano wa watu wa Oman na maktaba ya sanaa za waAfrika hapa Washington DC Karibu usikilize
Siku chache kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia la Soka huko Brazil, mambo mengi yamekuwa yakizungumzwa kuhusu maandalizi ya michuano hiyo.
Kuna malalamiko na maandamano nchini humo ambavyo kwa hakika vinaleta taswira isiyo njema kuhusu maandalizi ya michuano hiyo
Kutaka kujua mengi, Kwanza Production imefanya mahojiano na Halifa Ramadhan. Mtanzania mwenye maskani yake nchini Brazil ambaye amezungumzia mengi kuhusu maandalizi ya fainali za kombe la dunia na pia maisha ya nchini humo kwa ujumla.
KARIBU UUNGANE NASI
Kwa maoni ama ushauri tuandikie kupitia kwanzaproduction at gmail.com
Karibu katika mahojiano ya Kwanza Production na Dekula Kahanga "Vumbi" Vumbi ambaye anamiliki Dekula Band nchini Sweden Amezungumzia mambo mengi ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa albamu yake mpya ya Shujaa Mamadou Ndala iliyozinduliwa Aprili 23 na 24 huko Sweden. Pia, ametoa ushauri kwa wasanii wa Afrika Mashariki wanaotaka kufanya muziki nchi za Scandinavia KARIBU UUNGANE NASI
Kwa maoni na ama ushauri usisite kuwasiliana nasi kupitia kwanzaproduction at gmail.com
Hivi karibuni Jamii Production ilipata nafasi ya kuhojiana na mmoja wa wanamuziki waliojipatia umaarufu katika ucharazaji gitaa nchini Tanzania Dekula Kahanga aliye maarufu kwa jina la Vumbi. Mahojiano haya "mepesi" yamegusa mambo mbalimbali kuhusu maisha yake kimuziki Amehojiana na Jamii Production akiwa Sweden yalipo makazi yake ya sasa KARIBU UUNGANE NASI Kwa maoni, ushauri, nk usisite kutuandikia jamiiproduction@gmail.com
--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"
Dj Luke akiwa studio na Mubelwa Bandio wa Jamii Production
Karibu katika mahojiano na Dj mkongwe kutoka Tanzania na mmiliki wa blog ya Vijimambo Lucas Mkami a.k.a Dj Luke Joe Dj Luke ambaye makazi yake kwa sasa ni Maryland nchini Marekani ameeleza mengi kuhusu kazi zake hizi. Katika mahojiano haya, ameeleza historia yake katika kuchezesha muziki, aliyemvutia kuingia katika kazi ya uDj, mafanikio ya Dj, changamoto zake, ku-blogu na mengine mengi. Karibu Uuungane nasi
--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"
Muendelezo wa 147 Critics;leo tunamsikiliza mdau na mwanamuziki muhimu kwenye Tasnia ya Muziki wa kizazi kipya Dully Sykes.Ufahamu wake kuhusiana na marekebisho ya sheria ya ushuru wa bidhaa Sura 147 yanayogusa Muziki na Filamu. Tumsikilize Critics 147: Dully Sykes (4) Akiwa ni mtu wa nne kuelezea maoni yake kupitia Video;
Muendelezo wa mahojiano na wadau mbalimbalikuhusiana namabadiliko ya sheria ya Ushuru wa Bidhaa Sura ya
Muendelezo wa 147 Critics.leo tunamsikiliza mdau na mwanamuziki muhimu kwenye Tasnia ya Muziki
wa kizazi kipya Judith D.M Wambura a.k.a Lady Jay Dee,Ufahamu wake kuhusiana na marekebisho
ya sheria ya ushuru wa bidhaa Sura 147,yanayogusa Muziki na Filamu.
Tusikilize 147:Judith D.M Wambura a.k.a Lady Jay Dee Akiwa ni mtu wa tatu kuelezea maoni yake kupitia Video;
Judith Daines Wambura Mbibo akielezea mitazamombali mbali kuhusiana na uwekaji STAMP kwenye kazi za sanaa ya Muziki na Filamu. Huu ukiwa ni muendelezo wa kuwahoji wadau mbalimbali kuhusiana na mabadiliko hayo ya sheria ya ushuru wa bidhaa. Kwa maelezo zaidi ingia;TheImageProfession "Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.
Muendelezo wa 147 Critics ambapo leo tunamsikiliza mdau muhimu na makini kwenye Muziki wa Dansi na kwa
upande mwingine kwenye Filamu akielezea kuhusiana na marekebisho ya sheria ya ushuru wa bidhaa Sura 147
yanayogusa Muziki na Filamu.
Tusikilize 147 Critics:John F Kitime (2) akiwa ni mtu wa pili kuelezea maoni yake.
Msikilize vyema John F Kitime uweze kufahamu vyema yale anayoyajuwa na anayodhani ni muhimu kuwa sawa katika mabadiliko ya sheria hii!
Mahojiano haya na Ndg John F Kitime yametokana na -C. Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147 Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato itaanza kurasimisha biashara ya bidhaa za muziki na filamu kwa nia ya kuhakikisha kwamba uasili wake unatambulika na hivyo kuzuia vitendo vya kudurufu kazi za sanaa (piracy of artists work) hali ambayo inadumaza ukuaji wa sanaa na vipaji hapa nchini. Aidha, Mamlaka ya Mapato itaweka stampu kwenye bidhaa hizo ili uuzaji wa kazi hizo uwe rasmi na kuwawezesha wasanii kupata kipato stahili kutokana na kazi zao. Vilevile hatua hii itaiingizia serikalimapato. kwa Maelezo zaidi ingia;TheImageProfession "Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.
Mfululizo wa 147 Critics ambayo ni mahojiano ya wadau wa Filamu na Muziki yaliyofanywa na TFCA-
Tanzania Film Critics Association(On line Platform) kuhusiana na marekebisho ya sheria ya ushuru wa bidhaa Sura 147
ambayo yatapelekea kuanzia mwezi wa January 2013 bidhaa zote za Filamu na Muziki zilizopo hapa Tanzania kuwekewa
Stamp/Sticker kwa ajili ya Kurasimisha,Kumpatia kipato halali msanii na Kukusanya mapato ya serikali yanayotokana na
uuzaji wa kazi husika.
Sheria hii ina changamoto nyingi ambazo kama hazitatatuliwa zinaweza kuifanya sheria husiaka isfikie malengo yake,Je
wadau wanasemaje kuhusiana na hilo?
Tusikilize 147 Critics : Dr. Vicensia Shule (1) akiwa ni mtu wa kwanza kutupa maoni yake kupitia Video hii;
Mahojiano haya yametokana na -C. Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147 98. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho katika Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147 kama ifuatavyo:- ii. Mheshimiwa Spika, kumekuwa na kilio cha muda mrefu cha wasanii kudurufiwa kazi zao za sanaa na kukosa maslahi kwa kazi wanazofanya. Ili kutatua tatizo hili, Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato itaanza kurasimisha biashara ya bidhaa za muziki na filamu kwa nia ya kuhakikisha kwamba uasili wake unatambulika na hivyo kuzuia vitendo vya kudurufu kazi za sanaa (piracy of artists work) hali ambayo inadumaza ukuaji wa sanaa na vipaji hapa nchini. Aidha, Mamlaka ya Mapato itaweka stampu kwenye bidhaa hizo ili uuzaji wa kazi hizo uwe rasmi na kuwawezesha wasanii kupata kipato stahili kutokana na kazi zao. Vilevile hatua hii itaiingizia serikali mapato. 80 Kwa kuwa yanahitajika maandalizi ya kutosha ikiwa ni pamoja na kurekebisha sheria na kanuni mbalimbali, utekelezaji wa hatua hii utaanza rasmi tarehe 1 Januari, 2013.
Tunaangalia uelewa wa wadau kuhusiana na hili na nini kifanyike ili kuweza kuboresha sheria husiaka ili iendane na taratibu na miongozo itakayoweza kuleta ukombozi wa kweli.
Kujua Zaidi Ungana na mwenzangu;TheImageProfession "Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.