Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Mahojiano/Waswahili/Watanzania. Show all posts
Showing posts with label Mahojiano/Waswahili/Watanzania. Show all posts

Monday, 27 March 2017

Mahojiano na Dj D - Ommy ndani ya Kilimanjaro Studios U.S.A



Machi 16 2017, Mubelwa Bandio na Viola walipata nafasi ya kufanya mazungumzo na Dj D-Ommy katika studio za Kilimanjaro Studios.

Dj D-Ommy ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi nchini Marekani amezungumza mengi kuhusu maisha, kazi na tasnia nzima ya muziki.

Pia akapata fursa kuzindua rasmi kifaa kipya cha kazi kwa studio yetu, Pioneer DDJ SZ2

Karibu usikilize

Tuesday, 30 August 2016

Mahojiano na Prof Julius Nyang'oro katika kipindi cha JUKWAA LANGU


Profesa Julius Nyang'oro ni Mwalimu, mtaalam wa sayansi ya siasa na mwanasheria.

Amekuwa mwalimu tangu mwaka 1977 nchini Tanzania na hapa nchini Marekani.

Ni mwandishi wa vitabu zaidi ya 14, vingi vikiigusia Tanzania kwa namna moja ama nyingine. Moja ya vitabu alivyoandika, na ambavyo vilimtambulisha zaidi kwa jamii ya waTanznia, ni kumhusu Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete. Ambapo ameandika vitabu viwili kumhusu.

Prof Nyang'oro alikuwa mkarimu sana kuungana nasi kwenye kipindi cha JUKWAA LANGU Jumatatu ya Agosti 29, 2016 kuzungumzia mambo mbalimbali kuihusu Tanzania akiwa mwandishi, mwalimu, mtaalamu wa mausala ya siasa na
mwanasheria

KARIBU




Tuesday, 21 June 2016

Mahojiano na Makala Jasper kuhusu Tuzo ya National Geographic Society for Leadership



Makala Jasper ni Mkurugenzi Mwandamizi wa Shirika lisilo la kiserikali la Mpingo Conservation & Development Initiative (MCDI).

Juni 16, 2016, alitunukiwa tuzo ya National Geographic Society/Buffett Award for Leadership in African Conservation, akiwa ni mshindi miongoni ma washiriki 30 kutoka barani Afrika.

Tuzo hiyo imetokana na kazi anayofanya pamoja na wananchi katika Vijiji mbalimbali mkoani Lindi.
MCDI huwezesha wanakijiji kutumia rasilimali za misitu kujenga uchumi na kutunza mazingira.

Katika miradi inayofanyika chini ya MCDI, wananchi wameweza kujiendeleza na kujenga shule, hospitali, kununua chakula cha dharura na kutoa misaada kwa vijiji vingine.

Tuzo ya National Geographic Society/Buffet Award ni ya pili kupokelewa na Bw. Jasper.

Ya kwanza ilikuwa Whitley Fund for Nature Award aliyopokea nchini Uingiereza tarehe 27 Aprili, 2016.

Karibu umsikilize

Tuesday, 29 December 2015

Kipindi cha JUKWAA LANGU Dec 28 2015 (FULL)


Photo Credits: govtech.com

Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu Tanzania ya sasa na ile tuitakayo.
Wiki hii ni ya mwisho kwa mwaka 2015, hivyo kipindi hiki kimeangaza baadhi ya yaliyotokea katika siasa za Tanzania.
Studioni alikuwepo Dj Luke Joe, Said Mwamende na Mama Jessica Mushala.
Na kama kawaida, kwa njia ya simu tukaungana na wasikilizaji wengi ndani na nje ya Marekani
KARIBU

Monday, 28 December 2015

Mahojiano na msanii Hashim Kambi Washington DC


Hashim Kambi ni msanii wa filamu nchini Tanzania.
Alikuwa mkarimu sana kupita studio zetu za Kilimanjaro hapa Beltsville Maryland na kuzungumza nasi


Tuesday, 8 December 2015

Mahojiano na DC Paul Makonda katika kipindi cha JUKWAA LANGU Dec 7 2015




Kipindi cha JUKWAA LANGU hukujia kila Jumatatu kuanzia saa 11 jioni kwa saa za Marekani ya Mashariki kuijadili Tanzania ya sasa na ile tuitakayo

Katika kipindi hiki, tumeungana na Mhe Paul Makonda. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jiji Dar Es Salaam ambaye mbali na mambo mengine, ameeleza "ya moyoni" kuhusu tofauti iliyopo kati ya utendaji wa Rais wa awamu ya nne Mhe Jakaya Kikwete (aliyemteua katika wadhifa huo) na Rais wa sasa Dk John Magufuli. Kabla ya hapo aligusia namna alivyoteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya, na kwanini anaamini inastahili kuwepo namna nzuri zaidi ya kuteua watu katika nafasi kama yake.

Na kabla ya hayo yote, alizungumzia migogoro mbalimbali inayoendelea wilayani mwake kama wa kiwanda cha Urafiki, kubomolewa kwa nyumba za thamani, mgogoro wa Coco Beach nk.

Na kama ilivyo desturi, akapokea maswali na ushauri toka kwa wasikilizaji wetu

KARIBU

Monday, 20 April 2015

Mahojiano na Linda Bezuidenhout (LB) Pt I


Karibu katika sehemu ya kwanza ya mahojiano na mbunifu wa kimataifa wa mitindo mwenye asili ya Tanzania, Linda Bezuidenhout
Ameeleza mengi ikiwa ni pamoja na historia yake kwa ufupi, safari yake kwenda nje ya nchi, alivyorejea na kuanza harakati zake za mitindo
Nani alimfanya ashawishike na fani hii?
Maisha yake kimahusiano je?
Familia yake sasa na inavyokabiliana na kazi zake?
KARIBU

Sunday, 19 April 2015

Katika kipindi cha "HUYU NA YULE" kesho (Jumatatu), usikose kujua UNDANI wa maisha ya Linda‏


NI MENGI AMEZUNGUMUZA AMBAYO MIMI NA WEWE HATUKUYAJUA
Kesho Jumatatu katika kipindi cha huyu na yule cha mahojiano na mwanamitindo mbunifu wa LB kutoka Atlanta, Georgia atakapoelezea historia yake yenye milima na mabonde historia ya maisha yake yenye huzuni na furaha wakati mwingine Linda akitokwa na machozi kwa kukumbuka maisha aliyopitia. Je Mume wake Mali walijuana nae wapi? na mengine mengi kuhusu maisha yake ikiwemo kampuni yake ya LB na malengo yake ya kupeperusha bendera ya Tanzania anga za kimataifa. USIKOSE mahojiano yaliyofanywa na mwakilishi wa Vijimambo na kwanza production Michigan Alpha Igogo ambae alitaka kujua undani wa maisha ya mwanadada Linda


Alpha Igogo akifanya mahojiano na Linda jijini Atlanta
Maswali yalikua moto Linda akipumua na kumkumbatia Alpha Igogo baada ya mahojiano kufikia mwisho

Monday, 16 March 2015

NesiWangu Show...Albinism


Karibu katika kipindi cha NesiWangu.

Katika kipindi hiki, Harriet Shangarai amezungumza na wanaharakati wa masuala ya Albinism. Sehemu ya kwanza ni mazungumzo na Daisy Makwaia wa Albino Charity Organization na sehemu ya pili ni mazungumzo yao na mwanaharakati mwenye Albinism Babu Sikare wa Afrobino Ltd

Karibu


Monday, 9 March 2015

Mazungumzo na Mhe Samuel Sitta......Wizara na Kugombea Urais


Karibu katika sehemu hii ya pili ya mazungumzo na Mhe. Samuel Sitta (Mb)

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba ya Jamhuri ya Muungano waTanzania mwaka 2014.

Aliketi nasi kuzungumzia kuhusu kazi zake kama Waziri wa Uchukuzi na pia nia yake ya kugombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu (2015)

Karibu


Monday, 2 March 2015

Mazungumzo na Mhe Samuel Sitta (Pt I).......KATIBA


Karibu katika sehemu hii ya kwanza kati ya mbili za mazungumzo na Mhe. Samuel Sitta (Mb)
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba ya Jamhuri ya Muungano waTanzania mwaka 2014.
Aliketi nasi kuzungumzia zaidi suala hili la Katiba hii pendekezwa, na mchakato mzima wa kuipata
Karibu