Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Mama na maisha. Show all posts
Showing posts with label Mama na maisha. Show all posts

Thursday, 7 April 2011

Maisha ni Kitendawili!!!!!!!!

Huyu amejikunyata na hana furaha kabisa.   Kuna kinacho Msibu Maishani!!!.
Huyu naye amejiinamia na rafiki wako pembeni,lakini haitaji maongezi nao.Kuna anachowaza!!!!!!!!

Hii ndiyo dunia yenye mengi Mazuri na Mabaya,yenye Kupendeza na Kuchukiza,yenye Raha na Karaha,yenye Hudhuni na Furaha,yenye Vicheko na Vilio,yenye Kupata na Kukosa, yenye Kutia moyo na Kuvunja moyo.!!!Mmmhhh!!Tunahitaji Upendo na Faraja. Wapendwa nini chanzo  cha  haya na mwishowake nini?..


Sunday, 3 April 2011

Mungu Wabariki kina Mama wote !!!!!!!!!!!!!!!




Leo ni siku ya MAMA  Uingereza.Nichukue fulsa hii ya kuwatakia Kheri,Baraka,Mafanikio,Heshima,Upendo,Fadhili.
Mama yangu Mpendwa na Wamama Wote pamoja na mimi mwenyewe.Sijutii kuwa mama na Asante sana Mumewangu Isaac na Wanaume/kina baba Wote. Pasipo    ninyi  tusingeitwa mama.Pia Poleni sana mliopoteza/Kufiwa na mama,Mungu awalaze mahali pema peponi.
Mpendwa kwa kazi hizo na nyingine nyingi kila siku za kina MAMA,Tusiposaidiana na kina BABA,kweli tutapata wakati wa kupumzika?karibuni sana kwa kuelimishana na kutakiana kheri,kupongezana na unaweza kutupa kumbukumbu zako siku ambayo unahisi ulimfurahisha sana mamayako na siku uliyo muudhi sana mama yako!!.Na unapenda kumwambia nini mama yako?.MAMA NI KIUNGO CHA FAMILIA!!!!!!!!!!!