Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label UK.. Show all posts
Showing posts with label UK.. Show all posts

Wednesday 9 May 2018

PICHA NA HABARI ZA USIKU WA WASATU, BIRMINGHAM, UINGEREZA, APRILI 28



Na Freddy Macha


Jumuiya ya wasanii Watanzania Uingereza (WASATU) ilichemsha supu, ukumbi wa Heartlands , Birmigham, Uingereza Jumamosi iliyopita. Makutano haya yalikuwa pia sehemu ya mchango mahususi kusaidia wasichana wanaopewa mimba kabla ya kuwa watu wazima, kitongoji cha Tengeru, Arusha. Fedha zilikusanywa na mjasiria mali mkazi wa Birmingham, Mtanzania Sia Travel. Sia alijaa mlangoni akihakikisha kila senti iiliyolipwa na wahudhuriaji watashiba chakula , sanaa usiku kucha na kuwafariji vigoli wetu.
WASATU iliyoundwa mwaka 2016 chini ya udhamini wa Balozi wetu Uingereza, Mhe Asha Rose Migiro, inakutanisha wasanii wa ala mbalimbali chini ya viongozi- mwanamuziki na mcheza sarakasi mwenye nidhamu ya hali yajuu, Fab Moses na mtangaza mapishi ya Kitanzania, Uingereza, Bi Neema Kitilya, aliyetulizana kama shingo ya twiga.
Mwaka jana, 2017, shughuli hii ilifanywa Northampton na asilimia 20 ya kipato iliwafikia Watanzania waliofikwa na maafa ya mafuriko ya maji.







Warembo wa kujitolea, walioonesha mavazi yaliyoandaliwa na kampuni ya “All Things African” (inayoendeshwa na Mtanzania, mchapa kazi, asiyejua uvivu kabila gani, Hamida Mbaga). Toka kushoto, Yvonne Waweru, Georgeous Katega, Victoire Koleilas, Maureen Tibenda

Viongozi wa WASATU – Neema Kitilya na Fab Moses wakijadiliana huku shughuli zikikwea minazi na kuta

Fahari ya Tanzania – imesambazwa meza ya bidhaa mseto na “All Things African”

Mcheza ngoma aliyepitia mitihani mikali na vikundi maarufu vya mila zetu- Kibisa na Muungano - Likiwa Ismail- akionesha SINDIMBA – bila aibu, staha wala wasiwasi.


Rama Sax akipuliza vitu. Zamani alipiga na Simba Wanyika akashiriki kurekodi wimbo wa “Sina Makosa”. Rama Sax ni pia mwimbaji mahiri

Baadhi ya vyakula vya Kitanzania

Msanii wa mapishi Neema John aliyechangia kazi njema na Neema Kitilya.

Wageni toka Tanzania na Uganda. Huyo Mganda (kushoto) ni mwanafunzi wa lugha ya Kiswahili

Mpiga Gitaa mkuu wetu, Jioni Ticha na kipande cha kuku baada ya kazi jukwaani. Alisafiri toka Leeds. Mbali sana na hapa

Watanzania wakichangamkia shughuli
Sia Travel akihamasika. Hakupitwa

Mwanamuziki Saidi Kanda,(aliyesimama) mbabe na mtukuzaji wa vyombo asilia vya muziki wa Kitanzania, akijumuika na Wabongo nadhif, waliokuwemo

Mwandishi na mwanamuziki, F Macha pamoja na wasanii Likiwa Ismail (ngoma) na Rama Sax.



Shukrani...
kwa habari na Matukio nitumie kupitia Email;rasca@hotmail.co.uk

"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.







Wednesday 18 April 2018

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA WATANZANIA NA WAINGEREZA ,LONDON


Picha na Habari za Freddy Macha

Ulikuwa mkutano mfupi uliokusudia kutoa shukrani kwa wafadhili na Watanzania London wanaosaidia nyumbani. Fadhila hupitia Jumuiya ya Waingereza na Watanzania (BTS) na kitengo chake cha TDT = shirika la Mfuko wa Maendeleo Tanzania. BTS ilianzishwa mwaka 1975, na mlezi wake sasa hivi ni Rais mstaafu Ali Mwinyi.

BTS ilimkaribisha Makamu wa Rais Mheshimiwa Suluhu Samia, aliyekuja London wiki hii kudhuruia mkutano wa Viongozi wa Jumuiya ya Madola.

Kawaida viongozi hutegemewa hotuba ndefu zenye maelezo yanayochosha masikio.

Mhe Suluhu alitua chuo kikuu cha lugha za Afrika na Mashariki ya Kati (SOAS) akasalimiana na kupeana mikono na wananchi wa pande zote mbili. Hiyo tu ilitosha kuonesha imani yake kwa wananchi wachapa kazi wa pande hizi mbili.

 Makamu wa Rais Mhe Suluhu Samia akizungumza na Dk Mohammed Hamza, kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Uingereza




 Balozi wetu Uingereza, Dk Asha Rose Migiro akiwa na Kaimu Balozi Uingereza Tanzania, Mhe Marc Thayre


 Mwenyekiti wa Jumuiya Ya Uingereza na Tanzania – BTS. Dk Andrew Coulson aliyefungua na kufunga kikao cha Brunei Gallery, SOAS.




 Baadhi ya Watanzania waliohudhuria. Kutoka kushoto, Kiondo Wilkins, Dk Alex Paurine, Simon Mzuwanda na Joe Warioba.