Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Uchaguzi/Tanzania. Show all posts
Showing posts with label Uchaguzi/Tanzania. Show all posts

Wednesday, 11 November 2015

Mahojiano na Liberatus Mwang'ombe katika kipindi cha JUKWAA LANGU


Liberatus Mwang'ombe katika moja ya mikutano yake jimboni Mbarali
Katika kipindi cha JUKWAA LANGU wiki hii tulipata fursa kuongea na aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Mbarali kupitia CHADEMA Liberatus Mwang'ombe ambaye ameeleza mengi kuhusu uchaguzi ulivyokuwa, aliyojifunza, analotaka kufanya kuhusu matokeo na hata kwa wana-diaspora wengine wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali Tanzania


[AUDIO]: Kipindi cha Jukwaa Langu Nov 9 2015 (Full show)


Katika kipindi cha JUKWAA LANGU tulipata fursa kumhoji
aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Mbarali kupitia CHADEMA Liberatus
Mwang'ombe.
Pia, tuliangalia (mbali na mambo mengine), mwanzo wa awamu ya tano ya utawala wa Tanzania, na matarajio ya wengine.
Tunaizungumzia TANZANIA ya sasa na ile ijayo....hasa tutakayo.

Tuambie.......
1: Je! Ni lipi unalokumbuka zaidi kuhusu uongozi wa Rais Jakaya Kikwete?
2: Unazungumziaje namna Rais Magufuli alivyoanza wiki ya kwanza ofisini?
Na nini ungependa viwe vipaumbele kwa uongozi huu??
3: Una matumaini na matarajio gani na bunge la 11 litakalosimikwa rasmi hivi karibuni?

Wednesday, 4 November 2015

Kipindi cha JUKWAA LANGU Nov 2, 2015 (Full Show)


Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali yaihusuyo Tanzania.
Wiki hii, tumeangalia zaidi kuhusu mustakabali wa Tanzania baada ya UCHAGUZI MKUU 2015