- Ukifuata
kila linalosemwa na wanasayansi utashindwa kuishi. Leo watasema kunywa
kahawa kunapunguza msongo wa mawazo. Kesho watasema kunywa kahawa huko
huko kunaongeza shinikizo la damu na uwezekano wa kupata pigo la kiharusi. Leo watasema hiki na kesho watasema kile ali mradi ni vurugu tupu. Kibaya zaidi ni ukimya wao kuhusu nini cha kufanya hasa pale tafiti zao zinapotoa matokeo yanayokinzana.
- Kwa
vile nyingi ya tafiti hizi hufanyika huko Ulaya na Marekani, Waafrika
inabidi kuyapokea matokeo ya tafiti hizi kwa uangalifu sana kwani huwa
hayazingatii mazingira yetu na mtindo wetu wa maisha (japo sasa
tunajitahidi sana kuwaiga kwa kila kitu).
- Utafiti
uliofanywa mwaka jana na wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Queenesland
unaonyesha kwamba kuangalia runinga kwa watu wenye umri wa miaka 25 na
kuendelea kuna madhara makubwa kiafya na kunapunguza muda wa kuishi.
Utafiti huu unaonyesha kwamba kwa kila saa moja unayoitumia ukiangalia runinga basi unajipunguzia dakika 22 katika maisha yako. Hii ni sawa na kuvuta sigara mbili.
- Wanasayansi
hawa wanasema kwamba tatizo hasa siyo kuangalia tv bali madhara ya
kukaa mahali pamoja kwa muda mrefu ambako kunasababisha magonjwa ya
moyo, kisukari, kunenepeana na matatizo mengine ya kiafya
yanayosababishwa na mtindo wa maisha ya kubweteka (sedentary lifestyle).
Kufanya mazoezi, hata kama ni dakika 15 tu kwa siku ni jambo la muhimu
na kumeonyeshwa kuwa na faida nyingi za kiafya ikiwemo kuongeza siku tatu katika maisha yako.
Kusoma zaidi habari hii ingia kwa Blog ya kaka Matondo[MMN]http://www.matondo.blogspot.com
Ahsante kaka Matondo.