Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Wa-Tanzania. Show all posts
Showing posts with label Wa-Tanzania. Show all posts

Saturday, 11 October 2014

[AUDIO]: DAKIKA 90 ZA DUNIA. Kumalizika kwa mkutano wa DICOTA 2014


Baraza la waTanzania waishio nchini Marekani (DICOTA) limemaliza mkutano wake wa mwaka Jumapili ya Oktoba 5 jijini Durham jimbo la North Carolina ambao kwa wengi waliohudhuria, wameonyeshwa kuridhishwa nao.
Mwenzangu Mubelwa Bandio, anayo taarifa kamili.




Hii ni sehemu ya ripoti za Kwanza Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).
Hii ilikuwa ripoti ya Oktoba 11, 2014

Saturday, 5 July 2014

Mahojiano ya Kwanza Production na Diamond Platnumz baada ya tuzo za BET‏


Diamond Platnumz na DMK kwenye utoaji tuzo za BET Los Angeles
Photo Credits: DMK Global Promotions' facebook page
Karibu katika mahojiano ya Kwanza Production na Damond Platnumz. Msanii mwenye mafanikio makubwa kutoka nchini Tanzania
Amejiunga nasi kwa njia ya simu punde baada ya kuhudhuria utoaji tuzo za BET ambako yeye alikuwa mmoja wa waliokuwa wakiwania tuzo hizo.
Kazungumza mengi kuhusu TUZO HIZO.
Alipopokea na alivyopokea uteuzi wake, aliloliona kwenye tuzo hizo, ulinganishaji wake katika utoaji tuzo hizi na za Tanzania / Afika, alichojifunza, faida ya kuja kushiriki hili na hata mikakati yake ijayo kuhakikisha kuwa muziki wa Tanzania unafika mbali zaidi.
SWALI jingine alilojibu ni kuwa....ni kweli kuwa ili muziki wa Tanzania ushinde tuzo ni lazima uwe na mahadhi ya Afrika Magharibi (kama muziki wake wa Number One) ama Afrika Kusini 
Amejiunga nasi kwa msaada wa promota Dickson Mkama almaarufu DMK ambaye pia ndiye meneja wa msanii huyo hapa nchini.
KARIBU





Wednesday, 2 July 2014

Mahojiano na Kwanza Production na NURU THE LIGHT‏


Photo Credits: Bongo Celebrity 
Karibu katika mahojiano kamini kati ya Kwanza Production na NURU THE LIGHT.
Msanii, Mjasiriamali, Mtangazaji, Blogger na Mwanaharakati ambaye amekuwa mkarimu sana kujiunga nasi moja kwa moja kutoka Stockholm Sweden
Kazungumza mengi ikiwa ni pamoja na alivyoanza muziki
Kisha akagusia kuhusu onyesho lake la kwanza kabisa jukwaani.
Na kama nilivyokuja kumtambua, ni mtu mwenye misimamo na anayejitambua, utamsikia msimamo wake awapo studio
Nikataka kujua pia, nini anaona kama tatizo kubwa kwenye muziki wetu?
Haya ni machache kati ya mengi aliyozungumza nami
JIUNGE NASI