Kwa miaka mingi imesikika mikutano ya vyama na vilivyodai kushirikisha Watanzania Uingereza. Ila mwaka huu Jumuiya mpya iliyoundwa (ATUK-" Association of Tanzania United Kingdom")- imeahidi kuweka chombo tofauti.
Akizindua hafla hiyo mjini Reading (tamka “redding”) Balozi Asha Rose Migiro, alisifu jitihada hasa za kitengo cha vijana waliosukuma kuelewana. Akahimiza kuwa serikali nzima kuanzia Mheshimiwa Rais, Wizara ya Mambo ya Nje na Ubalozi wako bega moja na ATUK.
Baadaye Joseph Warioba alieleza kuwa kitendo hiki kimefikiwa baada ya utafiti na mazungumzo ya muda mrefu kuhakikisha hakuna tena migongano. Tofauti ya sasa na zamani ni nini? Warioba alihimiza kuwa zamani wahusika waliendekeza maslahi binafsi na ulafi. ATUK tunaelezwa, inashirikisha Watanzania wa kila namna wakiwemo wataalamu, wafanyabiashara, wasomi, wasanii nk. Shughuli iliofanyika Jumamosi 23 Juni, 2018 – ulikusanya zaidi ya Watanzania, ndugu na marafiki zao zaidi ya 300 –kiasi kikubwa kinachodokeza matumaini makubwa.












Tazama mahojiano na habari zaidi BAADHI YA WALIOSHIRIKI - “Kwa Simu Toka London” ( KSTL)
- MAHOJIANO NA JOE WARIOBA
- MAHOJIANO NA DEVOTA HAULE KUHUSU UKEKETAJI
- MAHOJIANO NA DOKTA GIDEON MLAWA –MTAALAMU WA KISUKARI
- MJASIRIA MALI HAMISA MBAGA AKIZUNGUMZIA KUHUSU BIDHAA ZA KITANZANIA ULAYA
5. NDOGO NDOGO ZA KIJANA EDWARD “HUNGAZ” CHACHA KUHUSU UMOJA WA WATZ
https://www.youtube.com/watch?v=TWmuDqP3MIM
6. TATHMINI YA MJUMBE WA ATUK- MOHAMMED MWAUPETE
https://www.youtube.com/watch?v=w_HJjmaTbGU