Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Wakati wa Shida. Show all posts
Showing posts with label Wakati wa Shida. Show all posts

Saturday, 5 May 2012

SHIME TUSHIRIKIANE KUMSAIDIA MWENZETU;WIMBO,TANZANIA ALL STAR- MBONI YANGU.


Wimbo huu ni maalum kwa ndugu yetu msanii Sajuki ambae anahitaji mchango wako wako wa hali na mali kuokoa maisha yake. Sajuki anasumbuliwa na uvimbe tumboni na mwezi huu anahitajika kusafiri kwenda nchini India kwa matibabu.
Wimbo huu unatoka katika filamu aliyowahi kuifanya na mkwewe ya MBONI YANGU.Na wimbo huu upo ndani ya filamu hiyo aliuimba Wastara.Wimbo huu umerekodiwa kuhamasisha na kumchangia Sajuki. Kutoa ni moyo bado hujachelewa. Unaweza kutuma mchango wako kupitia AKIBA BANK A/C # 050000003047 A/C ni ya mke wake Sajuki, Wastara Juma au unaweza kutuma kupitia M PESA 0762189592.

Mimi na wewe tunahitajika katika hili.

Habari zaidi na Picha,utazipata. http://www.jestina-george.com

Sajuki na Mke wake Wastara.
Sajuki alivyokuwa na Alivyo sasa.


Pole sana utapona tuu.

Pamoja waungwana.

Tuesday, 27 March 2012

MWAKILISHI WA UNOPS NCHINI SIERA LEONE NDUGU OMARY MJENGA AKISALIMIANA NA RAIS KIKWETE WAKATI WA MAZISHI YA MKUU WA WILAYA YA LIWALE MAREHEMU VICTOR P. CHIWILE JANA KIBAHA.


Mmoja wa waombolezaji akimsalimia Rais Kikwete kwa kuibusi Pete yake, kulia ni Ndugu Omary Mjenga akishuhudia tukio hilo.
Rais akisalimiana na Ndugu Omary Mjenga jana walipokutana kwenye mazishi ya Mkuu wa Wilaya ya Liwale.
Ndugu Mjenga alikuwa Personal Secretary wa Rais Kikwete wakati alipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje kabla hajawa Rais.

Habari hii nimetumiwa na KapingaZ Blog. http://kapingaz.blogspot.co.uk/
Ahsante Sana.

Wednesday, 16 November 2011

Kuna Siku za Furaha na Siku za Vilio,Yote ni MaishaTusikate Tamaa!!!

                 Siku Ndugu zangu walipokuwa na Furaha.
                                        Mshumaa ulio Zimika.
                                            Mshumaa ulioZimika

Mungu awatie Nguvu katika wakati huu Mgumu na Sikuzote,Zaidi tudumishe Upendo,Umoja,Ushirikiano na Tusikate Tamaa,Wakati kama huu ndiyo utamjua Rafiki,Ndugu wa Kweli na Mengi Mema kwa Mabaya unaweza kuyasikia.Na niwakati kwa Waliopoteza Wazazi/Wapendwa wao Kuwakumbuka na Kulia tena,Nimeamini wanaosema Kilio hakiishi Utalia kila unapokumbuka.Nilitamani niwe nanyi lakini Mungu aliye nanyi ni Zaidi yetu sisi Tuliyo mbali.Mungu awalaze Mahali Pema Peponi Nduguzangu na Rafiki zangu,Jirani zangu na Wote waliotangulia.Sina Mengi ya Kusema bali nasema Asante Mungu.Wenu MWANAPENZA.